MAELEZO YA UTANGULIZI KUHUSU UGONJWA WA GOUT
Gout ni aina ya ugonjwa wa arthrits ambao anaambatana na maumivu makali kwenye joint, kuvimba kutokana na mrundikano wa uric asidi ambayo hujikusanya na kufanya kama jiwe gumu kwenye joint. Hapo zamani gout ulijulikana kama ugonjwa wa wafalme (a disease of Kings) kutokana na unywaji wao wa pombe na vyakula vya kukidhi raha zao. Mfalme Henry wa VIII wa Uingereza ni mmoja ya wafalme waliougua ugonjwa huu. Alexander the great, Christopher columbus, Sir Isaack newton ni baadhi ya watu maarufu ambao waliugua ugonjwa wa Gout.kibaya zaidi ni kwamba namba ya watu wanaougua ugonjwa huu kwa sasa inaongeza taratibu haijalishi unatoka familia ya kitajiri ama laa.
GOUT NI NINI HASA
Huu ndio ugonjwa wa joints ambao huwashambulia sana na kuwapa
maumivu makali wanaume. Wanawake pia huweza kuathirika na ugonjwa huu hasa
baada ya kukoma hedhi. Ugonjwa huu huleta maumivu makali ya ghafla, hasa kwenye
sehemu linapoanzia dole gumba la mguu. Dalili za ugonjwa huanza kuonekana pale
uric acid, tindikali ambayo huzalishwa na mwili katika ufanyaji kazi wake
(ambayo haina manufaa kwa mwili) hubakia katika viungo vya mwili na katika
majimaji ya mwili. Uric acid iliyoganda (tophi) huweza kujikusanya na kubaki
chini ya ngozi inayozunguka joints, huweza pia kujikusanya ndani ya figo na
kusababisha kidney stones (namna ya kokoto ndogo ndani ya figo)
Gout
inaweza kusababisha madhara ya kudumu kwenye maungio ya mifupa na figo. Endapo
hatua za kuutibu ugonjwa huu hazitachukuliwa kwa muda mrefu (miaka 10 au
zaidi), madhara ya kudumu humtokea mgonjwa
Chanzo Cha Gout Ni Nini?
Gout kutokea kimsingi pale tindikali aina ya uric (uric
acid) inapozidi kiwango katika mwili wa binadamu hali ambayo kiutaalamu huitwa
hyperuricemia. Tindikali hii ni matokeo ya kuvunjwavunjwa na mwili kwa aina
fulani za chakula kama nyama, nyama ya kuku na chakula cha baharini. Tindikali
hii kwa kawaida huchanganyika na damu na mwisho hutolewa nje ya mwili pamoja na
mkojo kupitia figo. Tindikali hii ikitengenezwa kwa wingi mno au isipotolewa
nje ya mwili kwa kiwango kinachosatahili, ile inayobakia huganda na kukaa
kwenye maeneo ya joints na kusababisha maumivu kwenye joints hizo na maeneo
yaliyo karibu. Kuna mazingira ambayo hupelekea hali hii ya uzidifu wa tindikali
ya uric katika mwili na mwishowe gout kutokea nayo ni:
·
Jinsia: Wanaume huzalisha tindikali ya uric kwa kiwango kikubwa
zaidi kuliko wanawake, viwango vya uzalishaji kwa wanawake vikikaribia vile vya
wanaume pale tu wanapokoma hedhi.
·
Urithi: Kuzaliwa kwenye familia yenye historia ya gout kunakufanya
uwe kwenye hatari kubwa zaidi ya kuupata ugonjwa huu.
·
Mtindo wa maisha: Unywaji wa pombe huzuia utolewaji wa
uric acid nje ya mwili na ulaji wa chakula chenye purine kwa wing
husababisha kiwango cha tindikali ya uric kuwa kikubwa mwilini.
·
Madini ya lead: Kuwa karibu na madini haya kwa muda
mrefu kumeonyesha kuhusika na aina
fulani za gout.
·
Madawa: Baadhi a madawa yameonekana kuongeza kiwango cha uric acid
mwilini.
·
Matatizo ya kiafya: Kama figo hazifanyi kazi vizuri kiwango
cha uric acid mwilini kitapanda. Matatizo mengine ya kiafya yanayochangia
ni high blood pressure (hypertension), kisukari na hypothyroidism.
DALILI ZA GOUT
Ugonjwa wa gout huanza ghafla na mara nyingi katikati ya
usiku. Ugonjwa huanza kwa kuleta maumivu makali kwenye maungio ya mifupa
na mara nyingine kuambatana na uvimbe. Gout mara nyingi hushambulia maungio
makubwa ya dole gumba la mguu lakini pia huweza kushambulia maungio ya mikono,
ankles, viwiko vya mikono na vidole.
TIBA YA GOUT
Matatizo yaliyo mengi ya gout
huondolewa kwa kutumia dawa. Nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs),
colchicine au corticosteroids hutumika kuondoa maumivu kwenye eneo
lililoathirika na gout, japo mgonjwa atakuwa mteja wa dawa hizi mika yote.
Upande wa pili ni dawa za asili zinafanya vizuri sana
katika kutibu tatizo hili bila kukuletea madhara kwenye mwili. Ila hakikisha tu
unatafuta kituo sahihi chenye dawa zenye ubora mkubwa. Mtindo wa maisha unaweza
kusaidia katika kupunguza makali ya ugonjwa huu au kuzuia usikupate. Yafaa
kufanya yafuatayo:
– Kunywa maji mengi, lita 2-4 kwa siku
– Kutokunywa pombe
– Kuweka uzito wa mwili kwenye
kiwango kinachofaa
– Kupata mlo uliokamilika
(balanced diet)
– Kutotumia vyakula vyenye
purines kwa wingi ama nyama nyekundu (vinavyozalisha uric acid kwa wingi). Vyakula vya kula kwa
kiasi kidogo ni maharage na njegele zilizokaushwa, nyama pori, uyoga na
maini.
Kama tayari unaumwa basi usipate hofu unaweza kufika
ofsini kwetu ukapata huduma kwa kutumia vidonge vya mimea na ushauri pia namna
ya kutibu tatizo hili.
Gharama za dawa na virutubisho ni Tsh 150,000/= Pekee.
Bofya hapa Kuchati na Daktari kwa whatsapp
Upate maelekezo ya kufika ofisini Ambapo utapata huduma ya dawa za mimea zisizo na kemikali .
kama upo mkoani basi usihofu maana utatumiwa dawa baada ya kufanya malipo.
Comments
Post a Comment
TUANDIKIE UJUMBE MFUPI, JUU YA TATIZO LAKO, JINSIA, UMRI, NA MAHALI UNAKOPATIKANA