Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2018

Kisonono ni nini ?, je kuna Tiba ya kisonono ?

Nini maana ya kisonono, je naweza kupata tiba sahihi ya kisonono?  Soma makala jii upate kujifunza na kupata ueewa juu ya tatizo la kisonono ambalo limeathiri watu wengi sana kwa sasa hasa vijana wa kiume. Kisonono au kwa lugha ya kitaalamu Gonorrhea ni moja ya ugonjwa wa ngono ambao huambukizwa baada ya mtu mmoja mwenye ugonjwa kukutana kimwili mtu mwingine mzima. Kisonono mara nyingi husababisha maumivu makali na dalili zingine mbaya kwenye via vya uzazi na sehemu zingine kama, sehemu ya haja kubwa, macho na pia maumivu ya viungo. Ugonjwa huu wa kisonono huweza kuwapata watu wa jinsia zote wanawake kwa wanaume huku tafiti zikionesha kwamba wanaume ndio wanaoongoza kuambukizwa kuliko wanawake. Nnini husababisha kinonono au Gonorrhea?? Ugonjwa huu wakuambukizwa kwa njia ya ngono husababishwa na bacteria wanaoitwa Neisseria gonorrhoeae. Na hivo pale watu wanapokutana kingono bacteria hawa huweza kusambaa kwenda kwa mtu mwingine kutokana na msuguano wa viungo laini vya uzazi,