Nini maana ya kisonono, je naweza kupata tiba sahihi ya kisonono?
Soma makala jii upate kujifunza na kupata ueewa juu ya tatizo la kisonono ambalo
limeathiri watu wengi sana kwa sasa hasa vijana wa kiume.
Kisonono au
kwa lugha ya kitaalamu Gonorrhea ni moja ya ugonjwa wa ngono ambao huambukizwa
baada ya mtu mmoja mwenye ugonjwa kukutana kimwili mtu mwingine mzima. Kisonono
mara nyingi husababisha maumivu makali na dalili zingine mbaya kwenye via vya
uzazi na sehemu zingine kama, sehemu ya haja kubwa, macho na pia maumivu ya
viungo. Ugonjwa huu wa kisonono huweza kuwapata watu wa jinsia zote wanawake
kwa wanaume huku tafiti zikionesha kwamba wanaume ndio wanaoongoza kuambukizwa
kuliko wanawake.
Nnini
husababisha kinonono au Gonorrhea??
Ugonjwa huu
wakuambukizwa kwa njia ya ngono husababishwa na bacteria wanaoitwa Neisseria
gonorrhoeae. Na hivo pale watu wanapokutana kingono bacteria hawa huweza
kusambaa kwenda kwa mtu mwingine kutokana na msuguano wa viungo laini vya
uzazi, hapa utafahamu ya kwamba aina zote za ngono husambaza maambukizi ya
kisonono aina hizi ni kama
·
Ngono
ya kawaida kupitia uke (vaginal intercourse)
·
Ngono
kupitia njia ya haja kubwa (anal sex)
·
Na
ngono kupitia mdomo (oral sex)
Baceteria hawa wa Neisseria
Gonorrhoeae huwa kuambukizwa pia kwa kugusa mahali au kiungo kilichoathirika
mfano kugusa uke, uume, mdomo au sehemu ya haja kubwa ambayo tayari imeathirika
na kisonono. Habari njema ni kwamba Bacteria hwa hawawezi kuishi nje ya mwili
wa binadamu kwa Zaidi ya sekunde kadhaa, hivo hutaweza kupata maambukizi haya
kwa kutumia vyoo vya uma au kuchangia nguo na mgonjwa wa kisonono, Lkini
wanawake wenye kisonono huweza kuwaambukiza watoto wanaozaliwa wakati wa
kujifungua.
DALILI ZA KISONONO
Kwa mtu kuanza kuugua kisonono
huchukua walau siku 2 mpaka 5 tangu kuambukizwa ili kuanza kuona dalili mbaya,
lakini wakati mwingine yaweza kuchukua mpaka siku 30 hasa kwa wanawae kuanza
kuona dalili za ugonjwa, Dalili hizi zinaonesha una kisonono na unahitaji
kumwona dactari mapema
Dalili za kisonono kwa wanawake ni kama
v Maumivu wakati wa kukojoa
v Kuwasha kwa sehemu ya haja kubwa, na
kutoa majimaji mazito kila mara
v Kutokwa na uchafu ukeni kusiko
kawaida wakati na baada ya tendo la ndoa
v Kuvurugika kwa hedhi ama hedhi
kuchukua siku nyingi Zaidi
v Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
v Kupata homa mara kwa mara na
kujisikia mwili kuchoka sana
Dalili za kisonono kwa wanaume;
kwa upande wa wanaume dalili hujitokeza mapema Zaidi na hivo wanakuwa wa
kwanza katika kutafuta tiba na ushauri wa kiafya, maana tatizo husababisha
kuumwa sana homa kali, dalili zingine ni kama
v Kutokwa na uchafu mithili ya maziwa
na njano
v Maumivu makali wakati wa kukojoa na
mkojo wa mara kwa mara
v Kuwasha kwa sehemu za uume na haja
kubwa
v Kwa wagonjwa wachache hutokea macho
kuwa mekundu.
Namna gani unaweza kujizuia kupata kisonono?
Hili ni swali ambao yawezekana kila
mmoja wetu anajiuliza jinsi gani
ajikinge ii kuepuka madhara ya kisonono ambayo ni makubwa Zaidi. Njia rahisi za
ya uhakika kutoapata kisonono ni kuacha kabisa kujiusisha na ngono. Najua ni
vigumu kwa watu wote lakini ndio njia ya uhakika Zaidi, watu wasioshiriki ngono
mara kwa mara pia wapo kwene hatari ndogo Zaidi ya kupata kisonono. Kuepuka
ngono kabisa ni jambo gumu kutokana na kwamba mahusiano mengi hasa ya mke na
mume yanaimarika kwa kufanya Ngono,
ngono ni kiungo muhimu katika kuimarisha mahusiano ya mke na mume. Hivo ili
kupunguza hatari ya kupata kisonono hakikisha unafanya ngono salama na kuwa na
mpenzi mmoja mwaminifu.
Makundi ya watu waliopo katika hatari Zaidi ya kupata kisonono ni
- · Wenye umri mdogo
- · Wanaofanya ngono mara kwa mara na wapenzi wapya
- · Wanaofanya ngono na mtu mwenye mpenzi mwingine
- · Wenye wapenzi wengi (michepuko)
- · Wanaume wanaofanya ngono kinyume na maumbile na wanaume wenza
- Kujihusisha na ngono chini ya umri wa miaka 25
- · Waliowahi kuugua kisonono kwa kipindi cha nyuma
- · Wenye magonjwa mengine ya ngono kama vile Ukimwi
Unataka kuishi bila ya maambukizi ya kisonono? Fuata njia hizi salama
1. Tumia condom kwa kila tendo la ndoa:
husaidia kuzuia bacteria kupenya kwa mtu mwingine wakati wa ufanyaji wa ngono
2. Hakikisha mpenzi wako mpya anafanyiwa
vipimo kabla hamjaanza mahusiano ili kpunguza hatari ya kupata maambukizi
3. Usifanye ngono na mpenzi wako kama
anaonyesha kuwa na dalili za kisonono, mfano kupata maumivu wakati wat endo, au
kutoa majimaji mazito ya kijani na njano yenye harufu, au kujitokeza kwa
malengelenge kwenye uume au uke,.unapoona dalili hizi basi wewe na mpenzi wako
acheni kufanya ngono kwa muda mpaka mtakapofanya vipimo na kupata tiba kwa
ugonjwa huu.
4. Fanya vipimo mara kwa mara walau mara
moja kwa mwaka ili kugundua maambukizi mapema na kutibu mapema
MUHIMU KWA WAJAWAZITO WENYE KISONONO
Kama wewe ni
mjamzito na umegundulika una kisonono basi wasiliana na Daktari wako ili aweze
kukuanzishia tiba inayofaa ambayo haitaleta madhara kwa mtoto aliyeko tumboni.
Kisonono huweza kusababisha matatizo
makubwa kwa kichanga cha tumbo hivo inashauriwa kutibu ugonjwa huu
mapema iwezekanavyo ili kupunguza hatari kwa mtoto.
Kisonono
kinatibika vizuri kama mgonjwa atafuata utaratibu wa tiba kwa usahihi. Kumbuka
ni muhimu kucheza salama na kuepuka ngono nzembe ili kujizuia na maambukizi ya
kisonono
Comments
Post a Comment
TUANDIKIE UJUMBE MFUPI, JUU YA TATIZO LAKO, JINSIA, UMRI, NA MAHALI UNAKOPATIKANA