Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2016

MADHARA YA PUNYETO NA TIBA YAKE

MAELEZO  YA AWALI KUHUSU TATIZO LA UPIGAJI PUNYETO Watu wengi sana wanataka kufahamu jinsi gani wafanye ili kuachana na kitendo cha upigaji punyeto. Punyeto ni tendo la mtu la kuamsha hisia za mapenzi au msisimko ambao unampelekea mtu huyu kufikia kilele cha kujimalizia tamaa zake! Bila kufanya tendo halisi, hutumia fikra zake katika picha za zinazoitwa za ngono au picha zozote zinazoweza kulifanikisha tendo hilo, movie n.k. Kilele cha yote anafikia mahali anajimalzia tamaa zake mwenyewe!. Nimekuwa nikiona baadhi ya watu wanaosema wameelimika wakipingana wao kwa wao katika suala zima la kupiga punyeto! Wako wanaotetea kutokana na elimu yao na wanasema kwa ujasiri mkubwa kwamba "kupiga punyeto ni sehemu ya maisha ya mwanadamu" Ina maana katika maisha ya mwanadamu upigaji punyeto inaelezwa ni kama tendo la lazima mpaka inafikia mahali wanasema ni sehemu ya maisha (Maisha) ya mwanadamu. Nimekuwa nikipata kesi nyingi sana juu ya madhara yatokanayo na punyeto. Aslimia 60

KUVURUGIKA KWA HOMONI ZA KIKE NA SULUHISHO LAKE

Kuvurugika kwa homoni za kike ni suala pana linalojumuisha vyanzo vingi, kama mtindo wa Maisha (lifestyle), umri kwenda, sababu za kimazingira kama msongo wa mawazo. Sababu zote hizi zinaathiri uzalishaji na ufanyaji kazi wa vichocheo ama homoni zako. Napenda niseme tu kwamba moja ya sababu kubwa iliyonigusa kuandika elimu hii juu ya kuvurugika kwa homoni za kike ni ukubwa wa tatizo kwani tatizo hili limekuwa ni tatizo ambalo kila mwanamke analo na wengi wao wametumia kila mbinu ya kuondoa tatizo na wameshindwa. Basi leo utajifunza jinsi gani unavyohangaika kuangamiza sisimizi kwa kutumia bunduki na ni uharibifu wa miundo mbinu katika uhalisia kwani hukuzaliwa na matatizo hayo, ulikuwa mwenye afya tele na unayefurahia hedhi yako bila tatizo. MAMBO YANAYO ASHIRIA UNA TATIZO KATIKA HOMONI ZAKO ZA KIKE 1. Kuwa na hedhi ya muda mrefu Zaidi ya siku 7 unatumia Zaidi ya pedi 2 2. Kuwa na hedhi yenye kuambatana na maumivu Makali sana 3. Kuwa na hedhi yenye kuambatana na kichefu chefu

TIBA ASILI KWA VIDONDA VYA TUMBO NA KUONDOA MADHARA YA TINDIKALI AU KIUNGULIA.

MAELEZO YA UTANGULIZI KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO Kwanza kabisa katika mada hii napenda tufahamu kwamba miili yetu imeumbwa ikiwa na vimeng’enyaji ambavyo husaidia kuvunja vunja chakula ili kiweze kusagwa, vimeng’enyaji hivi vipo kuanzia mdomoni na njia yote ambapo chakula kinapita hadi kwenye utumbo mdogo ambapo ufyonzaji wa viini lishe hufanyika. Moja ya kimeng’enyaji  kinachopatikana tumboni ni asidi ama tindikali  inayoitwa hydrochloric acid ( HCL) .Asidi hii humwagwa juu ya chakula ili kurahisisha usagaji wa chakula tumboni. Kupanda kwa tindikali ni tatizo kubwa kiafya, ambalo linathiri watu wengi sana Nafkiri mpenzi msomaji kuna wakati umewah kupatwa na hii hali kwamba unapocheua basi unaona kama kuna maji maji yenye uchachu yanapanda kutoka tumboni adi kwenye koromeo, kitendo hichi ndicho tunaita KIUNGULIA. Hapo zamani  ilifahamika kwamba tatzo hili hutokana na wingi wa tindikali tumboni ndio maana wagonjwa hupewa dawa zinazohuisha asidi hiyo. NINI KINACHOSABABISHA KIUN

MSONGO WA MAWAZO UNAVYOATHIRI MWILI WAKO, NA NJIA ZA KUWEZA KUPUNGUZA MSONGO WA MAWAZO NA KURUDISHA MWILI KATIKA HALI YA KAWAIDA.

Moja ya sababu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzorota kwa afya na kusababisha vifo vingi ni msongo wa mawazo . NAMNA MSONGO WA MAWAZO UNAVOATHIRI MWILI Pale mwili unavokutana na hali ya tofauti aidha kitu cha kutisha au kinacholeta mawazo ndani ya mda mfupi na tofauti hiyo ikashindwa kutambuliwa haraka na ubongo mfano pale unapokutana na samba au mnyama yeyote mkali usiyemtegemea,  basi mwili hutoa kichocheo kinachoitwa cortisol ambacho kinamwagwa kwenye damu ili kuuandaa mwili aidha kupigana au kukikimbia hcho kitu. Mapigo ya moyo yanaongezeka, mapafu yanachukua kiwango kikubwa cha hewa, na mzunguko wa damu pia unaongezeka baadhi ya sehemu za kinga yako inazidiwa na mzigo mkubwa kwa mda hivo kutoa nafasi kwa viumbe adui kushambulia mwili wako kirahisi. Pale msongo wa mawazo unapokuwa mkubwa ndipo kinga yako ya mwili inavozidi kutohisi uwepo wa kichocheo cha cortisol ( yaani kwa lugha rahisi ni kwamba msongo wa mawazo unapunguza kwa kiasi kikubwa makali ya kinga ya

JINSI YA KUONGEZA UFANISI WA VICHOCHEO VYA KIUME (TESTOSTERONE) NA KUKINGA DHIDI YA MATATIZO YATOKANAYO NA KUKUA KWA TEZI DUME KWA KUTUMIA VYAKULA HIVI VI 5

Maelezo ya utangulizi. Kichocheo cha testosterone, japo huusishwa zaidi na upande wa mwananume ni muhimu kwa afya ya pande zote mbili yaani mwanamke na mwanamme pia.kadiri umri unavoenda mbele basi kiwango cha uzalishaji wa kichocheo cha testerone kupungua, kupungua kwa kichocheo hiki kunaambatana na ukuaji wa tezi dume (prostate gland),kupotea kwa nywele na pia saratani mfano saratani ya tezi dume. .KAZI KUBWA YA KICHOCHEO HIKI NI KUONGEZA MSUKUMO NA HAMU YA TENDO LA NDOA , KUIMARISHA MISULI NA MIFUPA MWILINI. NINI KINAHITAJIKA ILI KUZALISHA KICHOCHEO CHA TESTOSTERONE? Ili kuhakikisha uzalishaji wa kichocheo cha kiume unafanyika, mwili unahitaji virutubisho au viini lishe mbalimbali, baadhi ya viini lishe hivyo ni madini ya ZINC na vitamin D3,  vitamini D inaweza kuzalishwa na mwili pale ngozi yako inapokutana na mwanga wa jua, hapa nazungumzia mwanga wa asubuhi wakati jua ndo linachomoza na pia lile jua la jion karibia na kuzama, hivyo utakubaliana na mimi kuwa wengi wet