Skip to main content

MSONGO WA MAWAZO UNAVYOATHIRI MWILI WAKO, NA NJIA ZA KUWEZA KUPUNGUZA MSONGO WA MAWAZO NA KURUDISHA MWILI KATIKA HALI YA KAWAIDA.


Moja ya sababu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzorota kwa afya na kusababisha vifo vingi ni msongo wa mawazo .

NAMNA MSONGO WA MAWAZO UNAVOATHIRI MWILI
Pale mwili unavokutana na hali ya tofauti aidha kitu cha kutisha au kinacholeta mawazo ndani ya mda mfupi na tofauti hiyo ikashindwa kutambuliwa haraka na ubongo mfano pale unapokutana na samba au mnyama yeyote mkali usiyemtegemea,  basi mwili hutoa kichocheo kinachoitwa cortisol ambacho kinamwagwa kwenye damu ili kuuandaa mwili aidha kupigana au kukikimbia hcho kitu.
Mapigo ya moyo yanaongezeka, mapafu yanachukua kiwango kikubwa cha hewa, na mzunguko wa damu pia unaongezeka baadhi ya sehemu za kinga yako inazidiwa na mzigo mkubwa kwa mda hivo kutoa nafasi kwa viumbe adui kushambulia mwili wako kirahisi.
Pale msongo wa mawazo unapokuwa mkubwa ndipo kinga yako ya mwili inavozidi kutohisi uwepo wa kichocheo cha cortisol ( yaani kwa lugha rahisi ni kwamba msongo wa mawazo unapunguza kwa kiasi kikubwa makali ya kinga yako ya mwili), kwa sababu kitazalishwa kwa wingi zaidi ili kuandaa mwili kupambana, na hivyo madhara yanyotokana na kutofanya kazi kiusahii kwa kinga ya mwili ndivyo yataongezeka zaidi.

Ovary ni mfuko wa mayai ya kike, yaani mahali ambapo mayai ya kike huzalishwa.polycstic ovary syndrome au PCOS kwa kifupi ni ugonjwa unaosababishwa na kuvurugika kwa vichocheo vya kike unaowapata zaidi wanawake walioko katika kipindi cha kuzaa. Wanawake wenye PCOS huwa na ovary zilizotanuka na zenye vimbe za majimaji ndani yake. Hedhi isiyokatika au isiyo na mpangilio maalumu, uotaji wa nywele kwa kasi, Kitambi na nyama uzembe, hizi ni dalili ambazo zinaweza kutokea kwa mwanamke mwenye PCOS. Msongo wa mawazo husababisha mwili kutoa vichocheo kama androstenedione ambacho ni kisababishi cha awali cha tatizo cha kujaa majimaji mifuko ya mayai kwa wanawake.

MSONGO WA MAWAZO KUPITILIZA UNAVOBADILI VICHOCHEO VYA KIUME VILIVYOPO NDANI YA MWANAMKE.
Licha ya msongo wa mawazo kusababisha uzalishaji mkubwa wa vichocheo ndani ya mwili wa mwanamke pia vichocheo hivyo huanza kupambana na hali hiyo ya msongo wa mawazo. Hapa ieleweke kwamba msongo wa mawazo siyo kisababishi pekee cha PCOS , tatizo hilo linaweza pia kusababishwa na ulaji mbaya usiozingatia sheria za lishe bora, kutokufanya mazoezi, matumizi makubwa ya wanga na sukari na pia vyakula vilivyosindikwa na kwa ujumla mtindo mibovu na hatarishi ya kimaisha.

KWANINI MSONGO WA MAWAZO HUSABABISHA UZITO MKUBWA NA KITAMBI
Kuongezeka ovyo kwa uzito,kitambi na nyama uzembe ni tatizo linalohusiana na ,msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo unabadili jinsi mafuta yanavohifadhiwa ndani ya mwili kwa sababu ya kubadilika kwa vichocheona kemikali  mbalimbali zinavyozalishwa na mwili pale ambapo unakuwa na stress. Kwa mfano tafiti zinasema kuwa stress kupitiliza husababisha uzalishaji wa protini inayoitwa  betatrophin ambayo ni kizuizi kwa vimeng’enya ambvyo huvunjavunja mafuta yaliyohifadhiwa kwenye mwili.

NAMNA YA KUPUNGUZA ATHARI ZITOKANAZO NA MSONGO WA MAWAZO
Stress ni kitu kisichoepukika kwenye maisha ya kawaida, lakini ni muhimu kufahamu na kuelewa namna ambavyo unashugulika na tatizo hilo ndivyo itakavoamua matokeo yake kiafya aidha mazuri au mabovu. Msongo wa mawazo huisha pale tu kisababishi au hatari inapopita na kutoweka.
Kuna njia nyingi ambazo unaweza kutumia ili kupunguza msongo wa mawazo. Hvyo ni jukum lako kuangalia njia gani inafiti kwako na uweze kuikazania.
Moja ya njia hizo ni kuhakikisha unapata usingizi wa kutosha na kupumzisha mwili, mwili unapokosa usingizi wa kutosha basi unapunguza uwezo wa kukabiliana na msongo wa mawazo na hivyo kuongeza hatari ya kuugua  magonjwa ya moyo . njia zingine unazoweza kutumia ni hizi hapa
1.       kushugulisha mwili mara kwa mara
2.       kufanya mazoezi mepesi ya mwili
3.       kubadilishana mawazo na watu wanaokuzunguka
4.       tenga mda kufanya vitu vinavyokupa furaha
5.       kusikiliza musiki na kufurahi.
   Njia mbaya za kuondoa msongo wa mawazo
   Hebu tazama njia ambazo baadhi ya watu hutumia, njia ambazo hupunguza tatizo kwa muda mfupi na kulifanya tatizo kuwa kubwa zaidi baadaye:
·         Kuvuta sigara
·         Kunywa pombe sana
·         Kula sana au kula kidogo
·         Kukaa kwenye TV au kompyuta, saa nyingi sana
·         Kujitenga na marafiki, familia na shughuli
·         Kutumia vidonge
·         Kulala sana
·         Kuahirisha mambo
·         Kujishughulisha saa zote kuepuka matatizo
·         Kuwatulia wengine msongo wao (kubwatuka, kufoka, kupigana)
   Jifunze njia nzuri za kuondoa msongo wa mawazo
   Sasa chukua nafasi hii kujifunza baadhi ya njia nzuri ambazo unaweza kuzitumia kukabilina na msongo wa mawazo. Kuna njia nyingine nyingi tu lakini zote zinakudai uanze kufanya mabadiliko kimatendo. Kwa sababu kila mmoja wetu yupo tofauti na atakichukulia tofauti kinapotokea kitu cha kusababisha msongo wa mawazo, hakuna namna moja tunayoweza kusema ufanye linapotokea jambo fulani, hivyo basi itabidi ufanya utafiti na kuona ni njia zipi zinaleta mabadiliko kwako. Zingatia kile unachokimudu na utakochoona kuwa kinachokusaidia.
   Kimsingi kuna njia kuu mbili; kubadili mazingira ya chanzo cha msongo ambapo unaweza kukikwepa au kukibadilisha na pili kubadilisha jinsi hatua unazochukua ambapo unaweza kubalika ili uendane nacho au kukabaliana nacho. Tutazielezea njia hizo za kuukabili msongo wa mawazo hapa chini:

        1. Kukwepa Vyanzo Vya Msongo Wa Mawazo: 
     Si rahisi kukwepa kila chanzo cha msongo wa mawazo na ni vibaya kukwepa chanzo cha msongo wa mawazo ambacho inabidi ukikabili. Ukiwa makini utashangaa kuona uwingi wa vyanzo vya msongo ambavyo unaweza kuvikwepa.
  •     Jifunze kusema hapana: Tambua uwezo wako wa kimwili na kikazi na zingatia kufanya kazi kulingana na uwezo ulio nao. Kuchukua majukumu zaidi ya uwezo ni chanzo cha kujipa msongo wa mawazo.  
  •     Wakwepe watu wanaoklsababishia msongo: Kama kuna mtu anakusababishia msongo wa mawazo kila wakati, punguza muda wa kukutana naye au vunja kabisa mahusiano naye.
  •      Dhibiti mazingira mabovu: Kama habari za jioni za kwenye TV zinakukera, zimisha hiyoTV na kama msongamano wa magari kwako ni kero, chukua njia nyingine isiyo na msongamano hata kama ni ndefu zaidi.
  •     Kwepa mada zinazokupa maudhi: Kama mada za dini au siasa hukupa maudhi, acha kushiriki kwenye mada hizo. Kama kila siku unalumbana na watu fulani kuhusu mada fulani, acha kuanzisha mada hizo au tafuta kisingizio cha kuondoka mada hizo zinapoanzishwa.
  •     Chunguza ratiba yako: Itazame kwa kina ratiba yako, majukumu yako na kazi ulizojipangia kwa siku. Kama mambo ni mengi mno, yagawanye kwenye makundi ya yale ambayo ni lazima yafanywe na yale ambayo ni muhimu kufanyika. Yale ambayo si ya lazima sana yaweke chini kabisa kwenye ratiba au yaondoe kabisa.

              2. Badili Mazingira ya chanzo: 
     Kama inashindikana kukwepa chanzo cha msongo wa mawazo, badilisha mazingira yake. Jaribu kufikiria ni nini cha kufanya ili chanzo hicho kisijitokeze tena hapo baadaye, hii inamaanisha kubadili namna yako ya mawasiliano au namna unavyoendesha shughuli zako.
  •     Onyesha hisia zako: Kama kuna kitu au mtu anakukera, mweleze wazi kabisa kwa njia ya kistaarabu. Kama husemi, unajenga chuki na kuiacha hali ikibaki pale pale.
  •      Usilee matatizo: Usilikalie lile linalokukera, liseme wazi na chukua hatua mara moja ya kulizuia. Kama una kazi muhimu ya kufanya na rafiki yako mpenda hadithi anaingia, mwambie wazi kuwa una kazi muhimu na kwamba unampa dakika kadhaa tu za mazungumzo.
  •     Tumia muda wako vizuri: Kushindwa kutumia muda wako vizuri ni chanzo kikubwa cha kupata msongo wa mawazo. Unapokuwa umechelewa kukamilisha jambo lako, utalifanya bila utulivu na utakosa umakini. Lakini ukiwa na mpango mzuri wa muda wako, utafanya kila kitu mbele yako kiufanisi na bila kupatwa na msongo wa mawazo.

         3. Badilika Kuendana Na Chanzo: 
          Kama huwezi kukibadili chanzo cha msongo wa mawazo, wewe badili mtazamo wako kuhusu              chanzo hicho:
  •     Kitazame chanzo kwa mazuri yake: Kitazame chanzo cha kero kwako kwa kutazama mazuri ambayo yanaweza kupatikana  kutokana na chanzo hicho. Badala ya kulalamika na kukasirika         kutokana na foleni ya magari, chukulia kuwa huo ndio muda mwafaka kwako kujipumzika au kusikiliza muziki unaaoupenda ndani ya gari yako.
  •     Kuwa na mtazamo wa jumla: Litazame jambo linalokukera kisha jiulize kama ni jambo litakalokusumbua kwa muda gani, mwezi mmoja, mwaka na jee mwisho wa siku ni madhara gani yatakayotokea. Kama ni suala la mpito tu, elekeza nguvu zako kwenye mambo mengine.
  •      Rekebisha viwango vyako: Moja ya sababu ya kujipa msongo wa mawazo ni kutaka kila kitu kiende sawa kwa kiwango cha hali ya juu. Usijiweke kwenye mtego wa kushindwa kwa kujiwekea viwango vya juu kiufanisi. Jiwekee viwango vinavyowezekana kwako na kwa  wenzako na jifunze kukubali matokeo ambayo hayakufika kiwango lakini siyo mabaya.
  •     Yakumbuke mazuri yako: Msongo wa mawazo ukikunyemelea,chukua muda kidogo kushukuru kwa yale yaliyo mazuri katika maisha yako, ikiwa ni pamoja na vipawa nyako vizuri na vyenye nguvu. Hili litakusaidia kukupa mtazamo tofauti wa mambo yaliyo       mbele yako.
      4. Kubaliana Na Yale Ambayo Huwezi Kuyakabili: 
      Vyanzo vingine vya msongo wa mawazo huwezi kuvibadili wala kuvizuia. Huwezi kukizuia kifo cha mtu wa karibu yako, wala ugonjwa mkubwa, au mporomoko wa uchumi wa nchi. Hapa inafaa kukubaliana na hali ingawa ni vigumu, lakini ni bora kuchukua msimamo huo kuliko kugombana na kitu usichoweza kukibadili.
  •    Usijaribu kudhibiti kisichowezekana: Vitu vingi sana katika maisha yetu vipo nje ya uwezo wetu – hasa tabia za watu wengine. Kuliko kung’anga’nia na kugombana nao wabadili tabia, fikiria zaidi namna unavyoweza kuepukana na matatizo yao.
  •    Tazama upande wa pili: Unapokumbana na vikwazo vikubwa, chukulia kuwa ni nafasi ya kujifunza na kukomaa. Kama ni maamuzi yako mwenyewe ndiyo yaliyokusababishia matatizo, chukua nafasi hiyo kutafakari na kujifunza kwa maamuzi yako ya baadaye.
  •     Jifunze kusamehe: Lazima ukubali kuwa tunaishi katika ulimwengu wenye mapungufu mengi na kwamba binadamu kufanya makosa ni kawaida. Usiwe na hasira na chuki, jifunze kusamehe na kuendelea na mambo mengine.
    5. Pumzisha Na Burudisha Mwili Wako
      Mwili wako utapata uwezo mkubwa zaidi wa kukabiliana na msongo wa mawazo endapo utaulea kwa kupata muda wa kuupumzisha na kuuburudisha. Katika kuulea mwili wako unaweza kufanya yafuatayo:
·         Fanya matembezi
·         Pumzika kwenye bustani au sehemu zenye mazingira ya asili
·         Mkaribishe rafiki nyumbani
·         Pata kikombe cha chai au kahawa
·         Jishughulishe kwenye bustani
·         Soma kitabu kizuri
·         Sikiliza muziki
·         Angalia vichekesho
·         Cheza na mnyama uliyemfuga
    
       Kuulea mwili ni jambo la lazima na si jambo la kujifurahisha tu. Katika kuyafanya hayo, jipangie kabisa ratiba yako na usimruhusu mtu au vitu vingine kuvuruga ratiba yako, huu ni muda wako wa kuurudishia nguvu mwili wako. Jichanganye na marafiki wenye mawazo mazuri, hao watakusaidia kuondokana na madhara yanayotokana na kuwa na msongo wa mawazo. Jaribu kuwa ni mtu wa kufurahisha na kufurahia mambo kwani kicheko ni dawa ya kuondoa msongo wa mawazo kwa njia nyingi.
        6. Mazoezi Na Chakula Kizuri
      Unaweza kuongeza uwezo wako wa kukabiliana na msongo wa mawazo kwa kujenga afya ya mwili wako.
          HITIMISHO
     Mpenzi msomaji kama tayari umeshaathirika kutokana na msongo wa mawazo basi tumeweza kutengeneza kirutubisho  chenye vidonge 60 vilivyotengenezwa kiasilia kabisa ambacho kitakusaidia mambo haya
1.       kuongeza kinga ya mwili na kusaidia kurudisha mwili katika hali ya kawaida
2.       kupunguza athari za msongo wa mawazo na pia kuongeza usingizi kiafya
3.       kuondoa sumu mwilini zinazozalishwa kutokana na msongo wa mawazo, kuzua saratani na magonjwa ya moyo
4.       kuongeza ufanisi kwenye tendo la ndoa

Mafuta ya Lavender Kwa tiba ya Msongo wa mawazo

Kwa miaka ya hivi karibuni mafuta ya lavender yamekuwa ni kitu adimu na cha kuaminika zaidi kutokana na uwezo wake kukukinga dhidi ya matatizo ya neva.

Matumizi: Kupunguza msongo wa mawazo na kutengeneza usingizi mzuri. Weka mafuta ya lavender kwenye kopo la kupuliza (diffuser) kisha pulizia kwenye chumba cha kulala. Unaweza kupuliza jioni katika eneo la kupumzika kabla ya kwenda kitandani, pia unaweza kupaka kwenye ngozi nyuma ya masikio na ukapakaa kwenye mto wako. Hakikisha unapata mafuta mwali (ambayo hayana kemikali na hayajachanganywa na viambata sumu).

Mafuta haya asili yanapatikana ofsini kwetu kwa ujazo wa Ml 30, Gharama ya Tsh 20,000/=

Bofya hapa kuchati na Muhudumu kwenye Whatsapp uweze kupata mafuta yako ya Lavender.

au Piga simu namba 0746672914
Ofisi zetu zipo Magomeni Mwembechai,


Usiache kusoma makala yetu inayofuata: Jinsi Msongo wa mawazo na lishe mbovu inavopekelea kuvurugika kwa homoni na ugumba.





Comments

Popular posts from this blog

KUTOKWA NA UCHAFU UKENI, CHANZO NA TIBA YAKE

Uke wa mwanamke hufanya kazi ya kutoa njia kati ya sehemu ya nje ya mwili na viungo vya uzazi vya ndani vya mwanamke. Hali ya kawaida ya majimaji yaliyomo katika uke wa mwanamke huwa ni ya tindikali ili kuzuia maambukizi ya vijidudu wa kuleta maradhi. Hali hii ya utindikali huletwa na bacteria waishio katika uke wa mwanamke. Bacteria hawa ni wa kawaida na hawana madhara kwa mwili. Uke ulio katika hali nzuri hutoa majimaji haya ili kujisafisha. Majimaji haya yanayotengenezwa katika uke na kwenye eno la cervix hufanya kazi ya kuondoa seli zilizokufa na bacteria waharibifu nje ya mwili na huu ndio uchafu wa kawaida ambao mwanamke hutoa ukeni. Kutoa uchafu huu sehemu za siri ni njia ya kuusafisha uke na kuzuia maambukizi ya magonjwa. Kitu cho chote ambacho kitaharibu uwiano wa utengeneaji wa majimaji haya ndani ya uke kinaweza kujenga mazingira ya maambukizi katika uke. Uchafu Wa Sehemu Za Siri  Wa Kawaida Wanawake wote hutoa uchafu sehemu za siri. Kiwango cha uchafu unaotoka, ra

JINSI YA KUONGEZA UFANISI WA VICHOCHEO VYA KIUME (TESTOSTERONE) NA KUKINGA DHIDI YA MATATIZO YATOKANAYO NA KUKUA KWA TEZI DUME KWA KUTUMIA VYAKULA HIVI VI 5

Maelezo ya utangulizi. Kichocheo cha testosterone, japo huusishwa zaidi na upande wa mwananume ni muhimu kwa afya ya pande zote mbili yaani mwanamke na mwanamme pia.kadiri umri unavoenda mbele basi kiwango cha uzalishaji wa kichocheo cha testerone kupungua, kupungua kwa kichocheo hiki kunaambatana na ukuaji wa tezi dume (prostate gland),kupotea kwa nywele na pia saratani mfano saratani ya tezi dume. .KAZI KUBWA YA KICHOCHEO HIKI NI KUONGEZA MSUKUMO NA HAMU YA TENDO LA NDOA , KUIMARISHA MISULI NA MIFUPA MWILINI. NINI KINAHITAJIKA ILI KUZALISHA KICHOCHEO CHA TESTOSTERONE? Ili kuhakikisha uzalishaji wa kichocheo cha kiume unafanyika, mwili unahitaji virutubisho au viini lishe mbalimbali, baadhi ya viini lishe hivyo ni madini ya ZINC na vitamin D3,  vitamini D inaweza kuzalishwa na mwili pale ngozi yako inapokutana na mwanga wa jua, hapa nazungumzia mwanga wa asubuhi wakati jua ndo linachomoza na pia lile jua la jion karibia na kuzama, hivyo utakubaliana na mimi kuwa wengi wet

MADHARA YA PUNYETO NA TIBA YAKE

MAELEZO  YA AWALI KUHUSU TATIZO LA UPIGAJI PUNYETO Watu wengi sana wanataka kufahamu jinsi gani wafanye ili kuachana na kitendo cha upigaji punyeto. Punyeto ni tendo la mtu la kuamsha hisia za mapenzi au msisimko ambao unampelekea mtu huyu kufikia kilele cha kujimalizia tamaa zake! Bila kufanya tendo halisi, hutumia fikra zake katika picha za zinazoitwa za ngono au picha zozote zinazoweza kulifanikisha tendo hilo, movie n.k. Kilele cha yote anafikia mahali anajimalzia tamaa zake mwenyewe!. Nimekuwa nikiona baadhi ya watu wanaosema wameelimika wakipingana wao kwa wao katika suala zima la kupiga punyeto! Wako wanaotetea kutokana na elimu yao na wanasema kwa ujasiri mkubwa kwamba "kupiga punyeto ni sehemu ya maisha ya mwanadamu" Ina maana katika maisha ya mwanadamu upigaji punyeto inaelezwa ni kama tendo la lazima mpaka inafikia mahali wanasema ni sehemu ya maisha (Maisha) ya mwanadamu. Nimekuwa nikipata kesi nyingi sana juu ya madhara yatokanayo na punyeto. Aslimia 60