1. NYAMA NYEKUNDU
Protini ni muhimu kwa afya zetu,
lakini kama figo zako zina hitilafu, ama ulishawahi kupata vipimo na kujua kuwa
figo zako haziwezi kuhimili vyakula vyenye protini nyingi sanasana ile protini
itokananyo na nyama nyekundu basi unahitaji kupunguza matumizi makubwa ya nyama
nyekundu na badala yake ukatumia vyakula vingine vyenye protini kama samaki,
mayai, maharage, na karanga.
2.CHUMVI
Kwa baadhi ya watu matumizi makubwa ya chunvi
yanaweza kuongeza chembechembe za protini kwenye mkojo, hii inaashiria kwamba
figo yako haiko vizuri kiafya na pia inaweza kuashiria kufanyika kwa mawe
kwenye figo (kidney stones) ambayo yanaweza kuleta dalili kama maumivu makali
pembeni mwa tumbo, na maumivu wakati wa kukojoa.
3. UVUTAJI WA SIGARA
Uvutaji wa sigara siyo tu unaongeza
presha ya damu na kusababisha kisukari
ambayo ni magonjwa yanayoongoza kusababisha matatizo ya figo lakini pia uvutaji
wa sigara hupunguza mzunguko wa damu kwenye figo nahivyo kuletekeza matatizo ya
figo.
4. UNYWAJI WA POMBE
Matumizi makubwa ya pombe ni
hatari kwa afya yako, wanaume wanaotumia zaidi ya chupa 14 kwa week na wanawake
wanaotumia zaidia ya chupa 7 kwa week wapo katika hatari kubwa mara mbili ya
kuugua magonjwa ya figo.
5. MATUMIZI YA SODA
Matumizi ya soda mbili kwa siku
yanakuweka katika hatari kubwa ya kupata magonjwa ya figo.
6. UPUNGUFU WA MAJI
Figo zako zinahitaji maji safi
kwa wingi ili kufanya kazi vizuri. Kutopata maji kwa wingi husababisha matatizo
ya figo, unywaji wa maji vizuri husaidia kusafisha sumu na kupunguza hatari ya
kuzeesha figo.
7. VIDONGE VYA KUPUNGUZA MAUMIVU
Matumizi ya mara kwa mara ya
vidonge vya kupunguza maumivu mfano aspirini, ibuprofen huleta madhara kwenye
figo zako. Ongea na tabibu wako kama kuna kuna njia ingine unaweza kutumia
kupunguza maumivu badala ya kumeza
vidonge.
8. MADAWA YA KULEVYA
Matumizi ya cocaine, herion na
madawa mengine ya kulevya huleta madhara na kupunguza utendaji kazi wa figo
yako. Baadhi ya dawa hizi huongeza presha ya damu na kupelekea kutofanya kazi vizuri
kwa figo.
Kama una maoni ama ushauri ama
unahitaji tiba basi usisite
utapata tiba na virutubisho kwa gharama ya sh 90,000/= Kumbuka kushare pia na marafiki na ndugu
Kubofya hapa kuchati na Daktari kwa Whatsapp
utapata tiba na virutubisho kwa gharama ya sh 90,000/= Kumbuka kushare pia na marafiki na ndugu
Comments
Post a Comment
TUANDIKIE UJUMBE MFUPI, JUU YA TATIZO LAKO, JINSIA, UMRI, NA MAHALI UNAKOPATIKANA