“KUNYWA MAJI MENGI” ni msisitizo
ambao umekuwa ukipewa mara nyingi labda na mama nyumbani, ama na Daktari wako
au rafiki wako wa karibu, lakini ambacho hukuambiwa ni kwanini maji ni muhimu
kwa afya yako na pia kiasi cha maji unachotakiwa kunywa na ubora wa maji vyote
ni muhimu kufahamu. Najua swali la watu wengi ni kwamba Je ni kiasi gani cha
maji unachotakiwa kunywa kila siku?? . Maji ni muhimu sana kwa afy zetu ni
dhahiri kwamba unaweza kuishi bila chakula kwa siku nyingi lakini bila maji
utaishi mud mfupi sana. Miili yetu kiujumla imetengenezwa kwa maji ambayo
1. Ni muhimu katika kurahisisha umeng’enyaji
wa chakula, uvyonzwaji wa virutubisho na pia utoaji wa takamwili.
2. Kusaidia usafirishaji wa vitu
mbalimbali kwenye mwili.
3. Kurekebisha joto la mwili
4. Kulainisha joint ili kupunguza
msuguano wa mifupa na
5. Kusafisha ngozi ya mwili
KIASI GANI CHA MAJI NATAKIWA KUNYWA??
Japo kila siku unapoteza maji kwa
njia ya mkojo na jasho, maji yanayopotea yanatakiwa kufidiwa. Cha kufurahisha
ni kwamba mwili umeumbwa na njia inayokwambia ni muda gani ufidie hayo maji
yaliyopotea, njia hii huitwa “KIU”. Inawezekana ushauri mwingi ulopata
ukikwambia kunywa lita 2 ama 3 ama 4 za maji kila siku japo ni vizuri lakini
siyo ushauri sahihi. UKWELI ni kwamba hakuna kiwango kimoja ambacho kinaweza
kutumika na watu wote, chukulia mfano Mcheza mpira ambaye kila siku asubuhi na
jioni anapiga mazoezi kipindi cha kiangazi,na mzee wa miaka 50 ambaye hafanyi
mazoezi, na mama mwenye kilo 100 wakati wa kipindi cha baridi, ni dhahiri
kwamba watu hawa watatu watakuwa na ujazo tofauti kabisa katika kunywa maji.
Hivo nashauri kwamba usikilize mwili
wako unasemaje katika kuamua kiwango cha maji yanayotakiwa, pale unapopata kiu
basi kunywa maji kukata kiu na usinywe soda. Njia nyingine ya kugundua uhitaji
wa maji kwenye mwili ni kuangalia rangi ya mkojo, mkojo ukiwa na rangi ya Njano
ilokolea basi inaonyesha kwamba una uhitaji mkubwa wa kunywa maji, ;lakini kama
ni njano nyepesi basi upo sawa. NB kama unameza vidonge vya vitamin B2 basi
hutaweza kufanya jaribio hili maana vidonge hivi huweza kubadilisha mkojo na
kuwa njano nyepesi isiyokolea. Inashauriwa pia kunywa maji kidogo kidogo na
siyo kubugia glas nyingi kwa mara moja, kutokana na ukubwa wa mwili miili yetu
ina uwezo wa kutumia maji kidogo kidogo, hivo ukinywa maji mengi kwa mara moja
yatatumika kidogo na mengine yatatolewa nje kama uchafu.
FANYA KIU KUWA NI MWONGOZO WAKO WA
KUNYWA MAJI
Mwili unapokuwa umepoteza maji
asilimia 2 mpaka 3 basi hutoa alam ambayo ni kwa njia ya kiu kukwambia kwamba
unatakiwa kunywa maji. Kam una afya njema basi hakikisha unakunywa maji kila
unapopata kiu na hiyo ndo itakuwa mwongozo wako wa kiasi gani cha maji uweze
kunywa. Ni dhahiri kwamba kama unaishi kwenye maeneo ya joto mfano maeneo ya
pwani au unafanya sana mazoezi au shughuli nzito utahitaji kunywa maji mara
nyingi zaidi.
MAJI NA SIYO SODA NDO IWE KIKATA KIU YAKO, Maji safi na salama
ni kinywaji kizuri kukata kiu yako na kuujenga mwili, kama umeshakuwa mnywaji
wa kupindukia wa soda basi ni vizuri ukafanya mabadiliko.
Comments
Post a Comment
TUANDIKIE UJUMBE MFUPI, JUU YA TATIZO LAKO, JINSIA, UMRI, NA MAHALI UNAKOPATIKANA