Lishe
ni moja ya nguzo kubwa kwenye afya ya mtu, na ndio maana unatakiwa uanze
kutazama kwa jicho la karibu, kama ulikuwa unajali zaidi kazi huku ukibugia
vyakula vibovu naviita junk foods, bila kutambua madhara makubwa ya kiafya
yanayoletekezwa na vyakula huku ukijikuta unatumia pesa zote ulizotolea jasho
kuhudhuria matibabu, basi anza kugeuka ssasa, uweze kutumia pesa kidogo kununua
chakula bora na uepushe magonjwa mengi kama kisukari, saratani na magonjwa ya
moyo. Unachokula si tu kinafanya mwili unawiri na kuongeza nguvu pia kinaongeza
ufanisi wa mwili katika kufanya shughuli zake kama usagaji wa chakula na
usafirishaji wa chakula na takamwili.
Kama ulaji wako ni mbovu unaotegemea vyakula vilivyosindikwa na fast
foods, ambavyo si tu vinakosa baadhi ya virutubisho muhimu bali pia vinakuja na
sumu nyingi zikiwemo vionjo viongeza utamu (artificial sweeters)
zitakazorudisha nyuma afya ya mwili wako. Kinyume kabisa na vyakula asili
ambavyo vitakupa vitamin za kutosha, madini, kukufanya ujiskie una nguvu mda
wote kwa kukulinda dhidi ya magonjwa na hivo kufanya maisha yako kuwa ya furaha
siku zote.
1.
NYANYA
Nyanya
ni zao ambalo linapatikana kila sehemu ndani ya nchi yetu. Kabla ya kutumia
nyanya yako hakikisha imelimwa katika udongo salama ambao haujachafuliwa
sana na mbolea za kisasa, pia nyaya yako
inatakiwa iwe na asilimia ndogo ama hakuna ya dawa za vijiua vidudu, na pia iwe
ni nyanya ambayo haijabadilishwa genetiki zake ( nitakwambia madhara ya mkono
wa mtu ikiwemo ubadilishaji wa genetiki za mimea hapo mbele.
Nini
kinaifanya nyanya kuwa chakula bora.
Nyanya
zina kemikali zinazoitwa flavonoids (anticarcinogenic) ambazo hupambana na
visababisha saratani. Moja ya kemikali hiyo inaitwa lycopene ambayo hulipa
tunda kama nyanya, tikiti ile rangi yake nyekundu. Lycopene ina nguvu kubwa
katika kupambana na kuzuia saratani, hasa saratani ya tezi dume ( prostate
cancer). Nyanya pia huchangia aslimia 38 ya vitamin C , 30% ya vitamin A na 18%
ya vitamin K kwa matumizi ya kila siku. Kumbuka ili upoate lycopene ya kutosha
kwenye nyanya unahitaji kuzikaanga kidogo kwenye mafuta kisha ukala pamoja na
mchanganyiko wako wa vyakula vingine ulivyoandaa.
2.
BROCCOLI
Ni
moja ya chakula kinachopatikana kwa wingi pia kwenye masoko ya vyakula.
Historia inasema kuwa Broccoli ni mboga ambayo ilitumiwa sana za waroma hapo
zamani.matumizi yake makubwa yalianza karne ya 16, wafaransa na waingereza
walianza kutumia mboga hii mnamo miaka ya 1700 na hulo marekani mboga hii
ilianza kutumiwa na kuuzwa kibiashara mwaka 1920. Mboga unaweza kuandaa kwa
namna nyingi ikiwemo, kurosti, kula ikiwa mbichi, ni vizuri zaidi kutokana na
kwamba upikaji unaharibu baadhi ya virutubisho.
Nini
kinafanya broccoli kuwa chakula bora ambacho hutakiwi kukikosa.
Broccoli
ina kiasi cha vitamin C mara mbili zaidi ya chungwa, madini mengi ya calcium
kama maziwa na pia sifa ya kupigana na magonjwa kama saratani, kupambana na
virusi, kutokana na wingi wa madini ya selenium. Kikombe kimoja cha mtori wa
broccoli kitakupa mahitaji yako ya siku nzima ya Vitamin C na Vitamini K na pia
ni chanzo kizuri cha Vitamin A na Potasium. Baadhi yua faida zingine
zinazofahamika za broccoli ni hizi
1.
kupambana na saratani ama cancer
2.
kupambana na mashambulizi ya magonjwa
3.
kusaidia usagaji wa chakula na kuondoa sumu mwilini
4.Ulinzi
dhidi ya ,magonjwa mbalimbali hatari kama magonjwa ya moyo
5.afya
nzuri ya mifupa na meno
3.
TANGO
Ni
moja ya tunda na mboga inayozalishwa kwa
wingi zaidi duniani. Chanzo chake ni katika ukanda wa bahari ya mediterania.
Kuweza kutumia tango unaweza kukata kata na ukachanganya kwenye kachumbari
yako, ama unaweza kutengeneza jiuisi kwa kutumia blender yako ukiwa nyumbani.
Ni nini kinafanya Tango kuwa ni
moja ya chakula bora
Hapo
zamani za mababu zetu Tango lilitumika kama njia ama dawa ya asili kwa ajili ya
kutibu maumivu ya kichwa, juisi ya tango husaidia kusafisha ngozi, na kuondoa
uchovu kwenye macho. Maajabu haya ya tango yaliwafanya wanasayansi kuanza
kutafiti juu ya tunda hili, zikiwemo mbegu zake, Asilimia 90 ya Tango ni maji
ambapo zifuatazo ni virutubisho vinavyopatikana:-
1.Vitamini
K kwa ajili ya kuzuia maambukizi
2.
Vitamin C kwa ajili ya kupambana na maambukizi
3.
Vitamini B% ambayo huzalisha nguvu kwenye mwili
4.
Madini ya manganese kwa ajili ya kuimarisha mifupa
5.madini
ya potassium na magnesium kwa ajili ya afya ya Moyo
Tafiti
za hivi karibuni zinasema kuwa tunda la Tango kemikali inayoitwa lignans ambayo
hupatikana pia kwenye kabeji na vitunguu ambayo kazi ya lignans ni kupunguza
hatari ya kuugua magonjwa ya moyo, pia muungano wa lignin na bacteria wazuri
walioko kwenye mfumo wa usagaji chakula husaidia kupunguza hatari ya kuugua
badhi ya saratani kama saratani ya matiti, kizazi, na saratani ya tezi dume
4. PARACHICHI
Ni nini kinafanya Parachichi kuwa
ni moja ya chakula bora
Parachichi
ukilinganisha na matunda mengine ni tunda ambalo lina virutubisho vingi zaidi
na hutakiwi kulikosa kwenye mlo wako kila siku, tunda moja la parachichi lina
virytubisho vifuatavyo:-
1.
Vitamini K ambayo inaweza kuchangia 36% ya mahitaji yako
2.
30% ya mahitaji yako ya siku ya vitamin B
Muhimu
zaidi ni kwamba parachichi ni moja ya matunda machache ambayo yana kiasi
kikubwa cha mafuta mazuri (god fats) ambayo na hivyo itakusaidia kuweka mafuta
yako ya mwili kwenye msawazo na hivyo
kupunguza hatari ya kuugua magonjwa ya Moyo na uzito mkubwa.
5. NAZI
Mafuta
ya nazi ambayo hutengenezwa kutoka kwenye nazi iliyokomaa hutumika zaidi katika
nchi za wenzetu kama India, Sri lanka, Thailand na Ufilipino ambako mmea huu
hulimwa kwa wingi zaidi, hapa nchini pia mmea huu hulimwa sana mikoa ya pwani
kama Tanga, Pwani, Dar es salaam na Mtwara.
Mafuta
ya kula ya nazi yanaweza kutumika katika mapishi ya vyakula, kuchanganywa
kwenye saladi ayko, ama unaweza kutumia kutengenezea juisi.
Ni nini kinafanya Nazi kuwa ni moja
ya chakula bora,
Kwa
wale ambao wanapunguza uzito basi badala ya kutumia wanga na sukari, anza
kutumia Nazi kama chanzo cha mafuta mazuri (medium chain fats) ambazo huweza
kuvunjwa vunjwa kirahisi ndani ya
mwili na hivo kuweza kubadilishwa na ini
kuwa nguvu moja kwa moja pasipo kuhifadhiwa kama mafuta kama ilivyo ukila wanga
na sukari. Nazi ina uwezo mkubwa wa kupambana na bacteria, virusi na protozoa.
Matumizi ya nazi pia yatakusaidia
1.
Kuimarisha afya ya moyo
2.
kusapoti ufanyaji kazi wa tezi ya thairodi
3.
kuimarisha utendaji kazi wa ubongo
4.
kuimarisha kinga ya mwili
5.
Nazi ni chanzo kizuri cha petrol ya mwili ili kutoa nguvu
6.
Kusaidia muimarisha utendaji kazi wa mwili katika kukuwezesha kupunguza uzito.
Comments
Post a Comment
TUANDIKIE UJUMBE MFUPI, JUU YA TATIZO LAKO, JINSIA, UMRI, NA MAHALI UNAKOPATIKANA