Je una shaka kuusu shinikizo lako la damu? Je upo kwenye
usalama ama hatari??, kama unamaswali mengi juu ya presha ya damu basi hauko
peke ako, watu wengi wanaishi bila kufahamu shinikizo lao la damu, nashauri
kama unahitaji kuwa na afya nzuri basi hakikisha unafahamu kiwango cha presha
yako ya damu.
KWANN NI MUHIMU KUFAHAMU
Presha ya damu iliyo ya kawaida ni kipimo kizuri cha afya ya
moyo.
Kiwango cha damu kinachosukumwa na pia uwezo mzuri wa mishipa
ya damu kutanuka na kusinyaa.hivo presha ya damu inaweza kuongezeka endapo kuna
kiwango kikubwa cha damu ama mishipa haiwezi kutanuka vizuri, hali hii ni ya
kawaida kwani hutokea sana pale mtu anapofanya mazoezi, tatizo linakuja endapo
hali hii ikawa ni ya mwendelezo.. Hapo moyo unahitaji kufanya kazi kubwa sana
ili kufanya damu iendelee kutembea mwili.
Kikawaida Namba mbili hutumika kupima presha ya damu, systolic
na diastolic.
Kama systolic ni 120-139 mmHg na diastolic ni 80-89mmHg basi
upo kwenyq hatari ya kupata
shinikizo kubwa la damu.
KAMA SHINIKIZO LAKO NI KUBWA BASI FAHAMU KUWA KUNA NJIA
NYINGI ZA KUPUNGUZA UKIWA NYUMBANI KWAKO
1.
SHUUGULISHA MWILI NA FANYA MAZOEZI ZAIDI YA
KUTEMBEA
Mazoezi ni moja ya silaha kubwa katika
kurekebisha shinikizo lako la damu na level ya homini ya insulin. Panga kutembea
hatua kuanzia 7000 mpaka 10000 kwa siku.
2.
Epuka msongo wa mawazo
3.
Usitumie vyakula na vinywaji vilivyosindikwa;
vyakula vingi vilivyosindikwa vina sukari nyingi, chunvi na mafuta mabaya vyote
hivi vinaathiri shinikizo lako la damu kwa kiasi kikubwa
4.
Hakikisha unapata vkiwango kizuri cha vitamin D,
kwa kupata mwanga mwingi wa jua.
5.
Lishe yenye matunda na mboga mboga pia husaidia
kusawazisha shinikizo lako la damu.
Comments
Post a Comment
TUANDIKIE UJUMBE MFUPI, JUU YA TATIZO LAKO, JINSIA, UMRI, NA MAHALI UNAKOPATIKANA