Heri ya mwaka mpya 2017. Je umeshaweka mipango yako ya mwaka
huu?? Watu wengi wameshafanya hivo lakini pia asilimia kubwa wanawahi kukata
tamaa na kupunguza juhudi kuelekea kutimiza malengo yao ifikapo mwezi wa 2 ama wa 3. Nashauri mwaka
huu jikite katika kulinda fya yako kwa kubadili mtindo mbovu wa maisha na
baadhi ya tabia hatarishi. Kubadili mtindo wa maisha ni suala endelevu na siyo
kitu cha kutimiza siku moja au week chache .
MIKAKATI 7 YA KIAFYA UNAYOTAKIWA KUTEKELEZA 2017
1.
ACHA KUNYWA SODA NA VINJWAJI VILIVOSINDIKWA
Hii ni kwa sababu soda ina uhusiano na
matatizo kama uzito mkubwa, magonjwa ya moyo, magonjwa ini, na pia matatizo yamifupa, kama bado unatumia
soda mara kwa mara basi badilisha kwa kutumia maji, kahawa na juisi ambayo
umetengeneza mwenyewe nyumbani.
2.
KULA PARACHICHI KILA SIKU
Parachichi ni tunda linalopatikana kirahisi
na ni chanzo cha mafuta mazuri ambayo
mwili huweza kuunguza kiurahisi ili kutoa nishati, tafiti zinasema kwamba
unapoweka parachichi kwenye saladi yako basi unaongeza uvyonzaji wa viondoa sumu ambavyo hulinda mwili dhidi
sumu. Pia tafiti zinasema kwamba parachichi husaidia kulinda ini na kuzuia
kansa ya mdomo.
3.
FANYA MAZOEZI YA KUTOSHA
Tafiti zinasema kwamba kukaa kwa mda mref
ni sabab moja pekee inayoongeza hatari ya vifo na magonjwa, hatar ya kuugua kwa
watu wasiofanya mazoezi ni sawa na hatar ya watu wanaovuta sigara. Unatakiwa
kufahamu ni kwamba miili yetu iliubwa kushugulika na siyo kukaa seem moja bila
movement. Weka lengo la kutembea walu hatua 7000 mpaka 10000 ambazo ni sawa na
kilomita 6 mpaka 9.
4.
Kula zaidi samaki na mboga za majani
Protini ni virutubisho muhimu kwenye mwili
kama sehemu ya afya na kiungo cha cell, misuli mifufa na viini vya kusaga
chakula (enyzmes), lakini angalizo ulaji mwingi wa protini ni hatari kwa afya,
hivo badala ya kula nyama zaidi basi kula samaki kwa wingi.
5.
Kufunga kula kwa masaa kadhaa
Moja ya mkakati ambao sio tu unaondoa
kitambi na uzito mkubwa bali pia kuepusha magonjwa mengine hatari kama kisukari matatizo ya moyo, ulaji wa kila
mara ni chanzo cha matatizo haya yote na pia huufanya mwili kuana kuunguza
sukari kamachanzo cha nishati badala ya mafuta kitendo ambacho hupunguza viini
vinavyounguza mafuat. Tafiti zinasema kwamba mwili hujisafisha wenyewe na
kujijenga vizuri pale tumbo likiwa tupu
bila chakula. Kufunga kula kunajumuisha kukaaa jumla ya masaa 13 mpaka 18 bila
kula kwa siku hii unaweza kutimiza tu kwa kuvusha either chakula cha mchana ama
asubuhi, na kula milo miwili tu, hivo kama utachagua kula usiku basi hakikisha
unakula masaa ma3 kabla ya kulala, unapolala mwili uhuhitaji nishati kidogo na
hivo unapokula chakula kingi basi mwili unazalisha sumu nyingi kutokana na chakula kutosagw vizuri.
6.
LALA
MASAA 8 KILAUSIKU
Kutopata usngizi wa kutosha huleta madhara
katika kinga ya mwili na pia kuongeza msongo wa mawazo na hatari ya kuugua
maradhi. Ukosefu wa usingizi hupunguza homoni ya melatonin ambayo husaidia
kukukinga dhidi ya saratani .
7.
KULA ZAIDI VYAKULA VYENYE NYUZINYUZI
Chakula chenye nyuzinyuzi kwa wingi
hupunguza hatari ya vifo vya mapema kutoka kwenye ugonjwa wowte, kwa sababu
husaidia kupunguza hatari ya baadhi ya magonjwa kama kisukari, magonjwa ya
moyo, na saratani. Zingatia chanzo
kikubwa cha nyuzinyuzi kitoke kwenye mboga mboga, jamii za karanga na mbegu, na
siyo nafaka
Comments
Post a Comment
TUANDIKIE UJUMBE MFUPI, JUU YA TATIZO LAKO, JINSIA, UMRI, NA MAHALI UNAKOPATIKANA