Haya ni maumivu ambayo huyapata kifuani na kukunyima amani
kutokana na misuli ya moyo kukosa kiasi cha damu yenye oxygen. Kwa kawaida huu
sio ugonjwa bali ni dalili ya magonjwa ya coronary heart diseases.
DALILI ZA MTU MWENYE ANGINA PECTORIS
Dalili ya kwanza ya mtu mwenye tatizo la moyo{coronary heart
disease} ni angina pectori. Maumivu ya kifua kuanzia katikati kuelekea mkono wa
kushoto, maumivu ya shingo na hatimaye kwenye taya bila kusahau mgongo, dalili
nyingine ni kichefuchefu, kutapika,moyo kwenda mbio sana
kuvuja jasho kwa wingi baada ya mwendo kasi wa moyo.
AINA ZA ANGINA PECTORIS
Stable angina pectoris: aina hii ndio ujitokeza mara nyingi
zaidi ya zingine. Hali huwa mbaya tu unapokuwa unafanya kazi au mazoezi au kitu
chochote kinachoweza sababisha moyo kufanya kazi kwa nguvu. Hali hutulia au
kurudi katika hali ya kawaida unapopumzika. haina maana kwamba kuna shambulio
la moyo bali ni taarifa kuwa wakati wowote hali inaweza kuwa mbaya.
Unstable angina: hali hii haina mpangilio na hujitokeza
wakati wowote. Haiwezi kutulizwa na kupumzika kama ilivyokuwa kwa stable
angina, Na hata dawa haiwezi kutuliza hali hii. Aina hii ni hatari sana kwani
hali hii inapojitokeza huduma ya haraka inahitajika. kwani huwa ni ashirio la
shambulio la moyo ambalo linaweza kutokea wakati wowote.
Variant angina: Aina hii hutokea mara chache sana na haswa
asubuhi, ukiwa umepumzika na usiku wa manane. Tatizo hili haliwezi kutatuliwa
na pumzika au kutumia dawa.
Microvascular angina: aina hii ni hatari sana maumivu makali
sana na ya muda mrefu. Kwa hali hii huwa ni vigumu sana kutulizwa na dawa.
Kumbuka kuwa sio kila maumivu unayoyasikia kifuani ni angina
bali unaweza kuwa na matatizo mengine kama vile
Pulmonary ambolism{kuzba kwa artery za mapafu}
Maambukizi kwenye mapafu.
Aortic dissection{kuchanika kwa mishipa mikubwa}
Hypertrophic cardiomyopathy{kuathirika kwa misuli ya moyo}
Pericarditis{kuvimba nyama iuzungukayo moyo kwa ndani}
Panic attack
Angina ni ishara tosha kuwa damu inaenda kiasi kidogo sana.
Na mtiririko wake kwenye misuli ya moyo haukidhi mahitaji. Shambulio la angna huongezewa
na mazoezi au hali inaosababisha moyo kufanya kazi zaidi na hata misongo pia huchangia.
Coronary heart disease inawezapelekea shambulio la moyo. Kutokana na damu
kuzuiwa eidha kwa mishipa kupungua kipenyo au kuganda kwa damu. Shambulio la
damu ambalo husababishwa na kufa kwa misuli ya moyo myocardium muscles kutokana
na hawe ya oxygen na viinilishe kufika kiasi kidogo sana. Ifahamike kuwa moja
ya tatu ya watu wenye shambulio la moyo hufariki dunia kutokana na kupuuzia
dalili za awali.
CHANZO
Chanzo kikuu cha matatizo haya ni mrundikano mkubwa wa
mafuta ya cholesterol kwenye damu na mishipa ya moyo. Hali hii utokana na
matumizi makubwa ya vyakula vyenye mafuta{saturated fat}nyama, maziwa na mayai
ni chanzo kikuu bila kusahau dawa za mpango wa uzazi. Hali ya kurithi pia
imekuwa chanzo, uvutaji wa sigara, shinikizo la damu, uzito mkubwa na watu
wasiofanya mazoezi au kazi za kukaa kwa muda mrefu. Mwanzoni ilifahamika kuwa
ugonjwa huu ulikuwa unawashambulia wanaume zaidi lakin tafti za hivi karbuni
idadi iko sawa japokuwa wanawake uchelewa kuupata mpaka hormone ya estrogen
itakapopungua kuzalishwa.
USHAURI
Kama unapata dalili zisizo za kawaida basi muone dactari
mapema kwa ushauri na tiba.
Imetolewa na Mkumbo health.
Kama tayari unasumbuliwa na tatizo na umejaribu tiba bila
manufaa, hakikisha unafika ofsini kwetu hapa Dar es salaam , Magomeni Mwembechai upate huduma ya tiba
ya mimea kwa gharama ya sh 120,000/= laki 1 na elfu ishirini tu
Tupigie namba 0762336530.
kama upo mkoani basi ondoa shaka maana utatumiwa dawa baada ya kufanya malipo.
kama upo mkoani basi ondoa shaka maana utatumiwa dawa baada ya kufanya malipo.
Comments
Post a Comment
TUANDIKIE UJUMBE MFUPI, JUU YA TATIZO LAKO, JINSIA, UMRI, NA MAHALI UNAKOPATIKANA