Maumivu ya joint ni tatizo linalosumbua watu
wengi kwa sasa kutokana na mabadiliko ya mitindo ya Maisha. Umri mkubwa ni moja
ya sababu inayopelekea kutokea kwa tatizo, ambapo tishu za mwili zinakuwa kavu
na kupoteza uwezo wa kuvutika. Watu wengi wanfikiri kwamba kufanya mazoezi ni
hatari kwa afya ya joints lakini ukweli ni kwamba ili kuepuka magonjwa ya
joints mazoezi ni lazima katika akuongeza ufanisi wa viungo pia.
Nina uhakika kuwa umewaona akina mama wenye
umri mkubwa na miili mikubwa wanavyopata shida kutembea huku wakiinama
toka upande mmoja hadi mwingine kila wakipiga hatua au shida wanayopata
pale inapowabidi kupanda ngazi au kukuchuchumaa. Maneno kama “ugonjwa wa kuumwa
joints, nina tatizo la joints, maumivu ya joints” na maumivu ya mifupa
umeyasikia mara nyingi. Tatizo hasa hapa ni nini? Ungana nami katika mada
hii uujue ugonjwa huu wa arthritis.
UGONJWA WA ARTHRITIS NI NINI?
Arthritis ni ugonjwa unaotokana na namna
yo yote ya hitilafu katika maungio ya mifupa ya binadamu ambao husababisha
maumivu na pengine kuvimba katika sehemu moja au zaidi ya maungio hayo. Neno
arthritis halilengi ugonjwa mmoja bali jamii ya magonjwa ambayo kwa ujumla
yapo zaidi ya 100. Tabia kuu ya magonjwa haya ni maumivu kwenye maungio ya
mifupa (joints) ambayo ni endelevu na ambayo hutokea eneo hilo moja.
CHANZO CHA ARTHRITIS NI NINI?
Kusudi kuelewa chanzo cha ugonjwa huu,
hebu kwanza tutazame muundo wa joint au sehemu mifupa miwili inapokutana.
Fikiria goti ambapo mifupa miwili mmoja wa paja na mwingine wa mguu
vinapokutana:
Ligaments: Ndicho
kitu kinachoshikilia mifupa hii miwili pamoja. Hii ni kama utepe wa plastiki au
mpira unaonyumbuka uliozunguka eneo hilo kwa nje, ukikunja goti
inanyumbuka na ukinyoosha mguu inarudi.
Cartilage: Huu ni utando
unafunika eneo ambalo mifupa hugusana ili kuzuia mifupa hii isisuguane moja
kwa moja. Utando huu ambao kwa kiswahili tunauita gegedu huyawezesha
maungio hayo kufanya kazi kiulaini pasipo kusababisha maumivu.
Capsule: Hiki ni kitu
kinachofunika maungio haya kikizunguka pande zote. Ndani ya mfuko huu wa capsule kuna
synovial fluid ambayo huzalishwa na synovial membrane. Synovial fluid ni ute wa
kulainisha sehemu hiyo ya maungio na synovial membrane ni utando ulio
kwenye kuta za ndani za capsule.
Ugonjwa wa arthritis unasababishwa na
hitilafu yoyote katika sehemu hizo za maungio ya mifupa. Inaweza kuwa
cartilage inalika, upungufu wa synovial fluid, maambukizi ya vijidudu katika
moja ya maeneo hayo au mchanganyiko wa matatizo.
AINA ZA UGONJWA WA JOINTS-ARTHRITIS
Kama nilivyoeleza hapo juu, kuna aina zaidi ya
100 za ugonjwa huu wa joints au arthritis. Katika mada yetu ya leo
tutatazama aina kama nne hivi za ugonjwa huu, tukielezea chanzo cha kila aina.
OSTEOARTHRITIS: Hii ni aina ya
arthritis inayosumbua watu wengi zaidi kuliko aina nyingine zote. Ugonjwa huu huwapata
zaidi watu wenye umri mkubwa. Osteoarthritis hutokea pale cartilage inapopoteza
uwezo wake wa kubonyea na kuwa ngumu hivyo kuharibika haraka. Cartilage ni
kiungo cha kuhimili migandamizo ya ghafla (shock absorber). Cartilage hii
inapopoteza ubora wake, tendons na ligaments huvutika na
kusababisha maumivu. Hali ya uharibifu huu wa cartilage ikiendelea,
mwishowe mifupa huanza kusuguana moja kwa moja na ndipo mgonjwa
atakapoanza kupata maumivu makali sana.
Athari za ugonjwa huanza taratibu na kuongezeka
na muda. Kutaanza kutokea maumivu kwenye joint baada ya kufanya shuguli
fulani au baada ya mapumziko ya muda mrefu. Joints zitakaza, hasa mapema
asubuhi unapotaka kuanza shughuli zako za kawaida. Siku zinavyosogea
ndivyo utakavyoona ni vigumu zaidi kukitumia kiungo chako. Mara nyingine
utaona uvimbe kwenye joint. Osteoarthritis hushambulia zaidi nyonga,
mikono, magoti na uti wa mgongo.
RHEUMATOID ARTHRITIS: Ugonjwa huu
hutokea pale mfumo wa kinga ya mwili kwa bahati mbaya kuanza kushambulia viungo
vya mwili ikiwa ni pamoja na synovial membrane (synovium) na kusababisha
uvimbe na maumivu. Hali hii isipodhibitiwa, huweza kusababisha ulemavu.
Ugonjwa huu unaweza pia kushambulia macho, ngozi, mapafu, midomo, damu na
mishipa ya damu. Huu ni ugonjwa ambao zaidi ni wa wanawake na huwatokea
zaidi wawapo kati ya umri wa miaka 40 hadi 60. Mgonjwa atasikia maumivu na
kuona uvimbe kwenye joints za pande zote za mwili, yaani kama ni magoti, yote
mawili la kulia na la kushoto, yote yatashambuliwa. Viungo vinavyoshambuliwa
zaidi ni vidole, viwiko vya mikono na miguu.
Athari zake huonekana zaidi asubuhi unapoamka
na maumivu yanaweza kudumu kwa muda wa hadi nusu saa. Muathirika wa
ugonjwa huu hujisikia mchovu muda wote, hukosa hamu ya kula na hupungua uzito.
INFECTIOUS ARTHRITIS (SEPTIC
ARTHRITIC): Aina hii ya arthritis inatokana na maambukizi ya bacteria
kwenye synovial fluid. Maambukizi haya yanaweza kuwa pia ni ya fungus au
virusi. Wadudu kutoka sehemu nyingine ya mwili iliyo karibu na maungio ya
mifupa huweza kusambaa kupitia mfumo wa damu hadi kwenye joint na kuleta
maambukizi. Mara nyingi mtu mwenye aina nyingine ya arthritis ndiye anayepata
maambukizi ya namna hii. Mgonjwa ataanza kwanza kupata homa, maumivu na
uvimbe kwenye joint. Maeneo ambayo hushambuliwa zaidi na aina hii ya
arthritis ni goti, mabega, kiwiko cha mkono, kiganja (wrist) na vidole
na mara nyingi ni eneo moja tu ndilo litakaloshambuliwa.
JUVENILE RHEUMATOID ARTHRITIS
(JRA): Juvenile
rheumatoid arthritis (JRA) ni ugonjwa ambao huwapata zaidi vijana walio na
umri ulio chini ya miaka 16 na unakuja kwa namna nyingi. Kuna aina kuu tatu za
ugonjwa huu:
1. Pauciarticular JRA, huu ndiyo unaoonekana zaidi na
hauna madhara makubwa ukilinganisha na aina nyingine. Mtoto atasikia
maumivu kwenye joints zinazofikia nne.
2. Polyarticular JRA, huu hushambulia joints nyingi
zaidi, zaidi ya nne na maumivu yake ni makali zaidi. Kadri siku
zinavyoongezeka, ndivyo maumivu yatakavyozidi.
3. Systemic JRA, huu huonekana kwa nadra ambapo
maumivu hujitokeza kwenye maeneo mengi na madhara yake kuwa makubwa zaidi.
Mtoto ataanza kusikia homa za vipindi ambapo
huzidi zaidi nyakati za jioni. Hali hii inaweza kumtokea mtoto kwa muda mfupi
au kwa wengine kwa muda mrefu sana . Mtoto atapata mauvimu kwenye maungio ya
mifupa (joints), uvimbe kwenye maungio hayo na kukakamaa kwa viungo. Mtoto
huyu atakosa hamu ya kula hivyo kumfanya akonde. Ugonjwa ukizidi, mtoto
anaweza kudumaa (kushindwa kukua), ukuaji wa mifupa yake kuathirika na
kupata matatizo ya macho
- Kuondoa maumivu makali ya viungo yanayotokana na arthrits
- Kuzuia kutokea kwa magonjwa ya viungo
- Mafuta haya yanawafaa zaidi wenye matatizo ya viungo na mgongo, wagonjwa wenye matatizo ya gout, na wenye matatizo ya kumomonyoka kwa kifupa (osteoporosis).
VIRUTUBISHO
VYOTE HIVI VINAPATIKANA OFSINI KWETU HAPA DAR MAENEO YA MWEMBECHAI, hivo huhitaji
kuagiza nje ya nchi, Tayari tumefanya utafiti kuhusu ubora wake unaweza kufika
kwa kuwasiliana nasi moja kwa moja kupitia .
Comments
Post a Comment
TUANDIKIE UJUMBE MFUPI, JUU YA TATIZO LAKO, JINSIA, UMRI, NA MAHALI UNAKOPATIKANA