Kwanini Tezi Dume inavimba, Je Kuna Tiba ya Tezi Dume?
Ili kujibu maswali haya na mengine mengi tuanze kwanza kwa kufahamu nini maana ya tezi dume.
Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra).Tezi hii ina sifa zifuatazo.
· Ina umbo
kama yai (oval shape)
· Ina
ukubwa wenye vipimo hivi, upana 4cm na unene 3cm ingawaje hivi vipimo vinatofautiana kwa kila mwanaume.
· Tezi hii
hua yenye ukubwa wa kawaida lakini huongezeka ukubwa kadri ya umri
unavoongezeka.
· Tezi
hii hutengeneza majimaji yenye rutuba ya mbegu za kiume(shahawa) yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati
wa kilele cha tendo la ngono. Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo
hufanya shahawa (semen). Aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume
nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya fallopian tayari
kwa utungisho na yai la kike. Vilevile husaidia kupunguza hali ya kitindikali
(acidic condition) iliyopo katika uke,
ambayo kama isiporekebishwa, huweza kuua mbegu nyingi za kiume na kufanya
utungisho kuwa wa shida.
KUVIMBA TEZI DUME (BPH)
Kwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la
kawaida pia kwa tezi dume kuongezeka ukubwa na kuvimba. Hali hii kitabibu
huitwa Benign Prostate Hyperplasia au wengine hupenda kutumia maneno Benign
Prostate Hypertrophy kwa kifupi BPH. Hivyo
tezi inaweza ikawa kubwa sana lakini haina dalili hii ni kutokana na sehemu
gani ya tezi iliyovimba au kuongezeka. Tezi inapoonesha dalili jua tatizo hilo
ni sugu na liko ktk hali mbaya. Kwenye
makala hii tutautumia sana ufupisho huu wa BPH ili kurahisisha kuelewa.
Ukuaji wa tezi dume hupitia hatua kuu mbili.
Hatua ya kwanza hutokea kipindi cha balehe wakati tezi dume linapoongezeka
ukubwa na kuwa mara mbili ya lilivyokuwa hapo awali. Baada ya hapo ukuaji
husimama kwa muda mpaka kijana anapofikisha miaka 25 hadi 30 ndipo hatua ya
pili ya ukuaji huanza tena. Ukuaji huendelea kwa viwango na kasi tofauti kati
ya mtu na mtu na hatimaye kusababisha BPH katika umri wa utu uzima.
Wakati tezi dume linapokua na kutanuka, utando
wa tishu unaozulizunguka hutanuka pia. Hata hivyo ingawa tezi dume huendelea
kukua, hufikia wakati utando wake huacha kutanuka na kufanya tezi dume kubana
mrija wa kutolea mkojo kutoka kwenye kibofu. Hali hii husababisha kibofu cha
mkojo kuwa na ngozi ngumu. Hali hii hufanya kibofu cha mkojo kuhisi kutaka
kutoa mkojo nje hata kama kiasi cha mkojo ndani yake ni kidogo sana. Hufikia
wakati, kibofu huwa dhaifu na kupoteza uwezo wake wa kuhisi kutoa mkojo na
hivyo kufanya mtu anapokojoa kushindwa kutoa mkojo wote na badala yake hubakiza
kiasi fulani cha mkojo kwenye kibofu.
kuvimba kwa tezi dume husababishwa na nini?
Chanzo halisi cha BPH au vihatarishi vyake
(risk factors) havijulikani kwa uhakika. Kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa
kuwa BPH hutokea kwa wanaume watu wazima na wazee tu. Aidha imewahi kuonekana
huko nyuma kuwa PBH haitokei kwa wanaume ambao wamewahi kufanyiwa operesheni ya
kuondoa korodani au wale ambao walizaliwa bila korodani. Hali imepelekea baadhi
ya watafiti kuamini kuwa BPH ina uhusiano mkubwa na umri wa mtu pamoja na uwepo
wa korodani.
Dhana (theories) kadhaa zinazojaribu kuelezea chanzo cha BPH. Dhana hizo ni pamoja na
Uhusiano kati ya BPH na homoni ya estrogen:
Wanaume huzalisha testosterone, homoni ya muhimu sana katika mwili wa mwanaume.
Hali kadhalika huzalisha pia estrogen ambayo ni homoni ya kike kwa kiwango
kidogo sana. Kadiri jinsi mtu anavyozeeka, ndivyo uzalishaji wa testosterone
unavyokuwa mdogo na kufanya kiwango chake katika damu kupungua kulinganisha na
kiwango cha estrogen ambacho huongezeka kwa kiasi fulani. Pamoja na kazi
nyingine, estrogen pia huchochea ukuaji wa chembe hai za mwili. Tafiti
zilizofanywa kwa wanyama zimeonesha kuwa BPH hutokea kwa sababu kiwango kikubwa
cha estrogen katika damu huchochea ukuaji wa seli za tezi dume na hivyo kufanya
tezi dume kuvimba.
Uhusiano kati ya BPH na Dihydrotestosterone
(DHT): DHT ni kiasili kinachozalishwa kutokana na testosterone kwenye tezi
dume, ambacho husaidia kuthibiti ukuaji wa tezi dume. Ingawa wanyama wengi
hupoteza uwezo wa kuzalisha DHT wanapofikia umri wa uzee, baadhi ya tafiti
zimeonesha kuwa, kwa binadamu, hata kama kiwango cha testosterone kitapungua
sana katika
damu, wanaume watu wazima bado wana uwezo wa
kuzalisha kiasili hiki cha DHT katika tezi dume zao. Uzalishaji huu wa DHT
huchochea kwa kiasi kikubwa ukuaji wa seli za tezi dume na kusababisha BPH.
Wanasayansi wamegundua kuwa wanaume watu wazima wenye.
Kiwango kidogo cha DHT hawapati BPH. Uhusiano kati ya BPH na maelekezo ya seli.
Dhana
nyingine inasema kwamba baadhi ya seli kutoka katika sehemu fulani ya matezi
yanayohusika na ukuaji mwilini hupewa maelekezo wakati mtu anapokuwa bado
mdogo. Seli hizi hutunza maelekezo hayo na baada ya miaka kadhaa maelekezo haya
huanzwa kutekelezwa na seli za matezi mengine. Mojawapo ya melekezo hayo ni
kuchochea ukuaji wa tezi dume na kusababisha BPH.
Dalili za kuvimba kwa tezi dume
1. Kukojoa mara kwa mara
2. Kubakiza mkojo kwenye kibofu
3. Kukujoa sana usiku
4. Maumivu wakati wa kukojoa
6. UTI ya mara kwa mara
7. Mawe kwenye kibofu kutokana na mrundikano wa mkojo.
8. Figo kujaa maji. Hii sababu mkojo huo unarudi nyuma
kuelekea figo (hydronephrosis)
9. Kupoteza fahamu(uremia)
Madhara ya kuvimba kwa tezi dume.
BPH kama ilivyo saratani ya tezi dume, inaweza
kumletea mgonjwa madhara (complications) kadhaa. Madhara hayo ni pamoja na
·
Mkojo kushindwa kutoka (retention of urine)
·
Mgandamizo kwenye kibofu cha mkojo
·
Vijiwe kwenye kibofu cha mkojo
·
Uambukizi katika njia ya mkojo (UTI)
·
Madhara katika figo au kibofu
·
Kushindwa kutoa shahawa kwenye uume
(retrograde ejaculation)
·
Nimonia (Pneumonia)
·
Damu kuganda
Baada ya mgonjwa kujihisi dalili zilizotajwa
hapo juu, daktari atamfanyia uchunguzi wa mwili kabla ya kumfanyia vipimo
zaidi. Vipimo vyaweza kutofautiana kati ya mgonjwa namgonjwa, lakini baadhi ya
vipimo ni pamoja na
1.KUCHUNGUZA TEZI DUME KUPITIA NJIA YA HAJA KUBWA AU
DIGITAL RECTAL EXAMINATION (DRE):
Hiki ni kipimo cha kwanza
kabisa ambacho mgonjwa hufanyiwa na daktari wake. Ni kipimo kinachoweza kumpa
daktari picha ya tatizo na kufahamu kuhusu ukubwa na hali ya tezi dume. Daktari
akiwa amevaa glovu huingiza kidole chake cha shahada katika njia ya haja kubwa
au puru (rectum) ya mgonjwa kasha kuzungusha zungusha ili kufahamu kama tezi
limevimba ama la na pia hali yake kama ni gumu
kuliko kawaida ama lina utando na nyama laini.
2.KIPIMO
CHA DAMU CHA PROSTATE-SPECIFIC ANTIGEN (PSA):
PSA husaidia
kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH. PSA ni aina ya protein
inayozalishwa na seli za tezi dume na kiwango chake huongezeka iwapo kuna
saratani ya tezi dume.
3.UTRASOUND YA PURU (RECTAL ULTRASOUND):
Kipimo
hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa saratani ya tezi dume badala ya
BPH. Utrasound ya puru pamoja na kuonesha taswira ya tezi dume ilivyo, pia
humuwezesha daktari kuchukua kinyama (biopsy) kwenye tezi dume kwa ajili ya
uchunguzi zaidi ili kutofautisha kati ya saratani na BPH.
4.KIWANGO CHA UTOKAJI WA MKOJO (URINE FLOW STUDY): Ni kipimo
kinachotumika kufahamu kasi ya utokaji wa mkojo. Mkojo unaotoka kwa kasi na
kiwango kidogo huashiria kuwepo kwa BPH.
5. KIPIMO CHA KUCHUNGUZA KIBOFU CHA MKOJO (CYSTOSCOPY): Kipimo
hiki husaidia kuweza kufahamu ukubwa wa tezi, sehemu tezi lilipobana njia ya
mkojo na kiwango cha kubana huko. Aidha huwezesha pia kutambua hali ya kibofu
cha mkojo ikoje.
MATIBABU
YA TEZI DUME
Matibabu ya BPH yameganyika katika sehemu
mbili, yale yanayofanywa kwa kutumia dawa na yale yanayofanywa kwa kutumia
upasuaji mdogo. Aidha matibabu hufanywa kwa watu wenye BPH kubwa zaidi na
dalili zinazowaletea usumbufu na kuathiri maisha yao, wakati wale wenye dalili
ndogo ndogo hawalazimiki sana kuhitaji matibabu.
MATIBABU
KWA NJIA YA DAWA
Dawa hizi hutumika kwa lengo la kulifanya tezi
dume kusinyaa na kupungua ukubwa wake.
MATIBABU KWA NJIA YA UPASUAJI)
·
Upasuaji mdogo husaidia kuondoa dalili za BPH
na hufanyika pale ambapo matibabu kwa njia ya dawa yameshindwa kuonesha
mafanikio yeyote. Njia hizo niTiba ya kutumia mawimbi ya joto (Transurethral
microwave procedures, TUMT): Tiba hii hutumia kifaa kinachotoa mawimbi ya joto
(microwave) yanayochoma na kuharibu tishu zilizovimba za tezi dume.
·
Matibabu huchukua chini ya saa moja na
yanaweza kufanyika bila mgonjwa kuhitaji kulazwa.Tiba ya kutumia sindano maalum
(Transurethral needle ablation, TUNA): Njia hii hutumia visindano vidogo
ambavyo huunganiswa kwenye chombo chenye kutoa nishati ya joto kuunguza tishu zilizovimba
za tezi dume.
·
Tiba ya kutumia joto la maji (Water-induced
thermotherapy): Tiba hii hutumia maji ya moto yaliyochemshwa kwa kifaa maalum
kuunguza na kupunguza tishu zilizovimba za tezi dume.
Madaktari wengi hushauri kuondolewa kabisa kwa
tezi dume iwapo itathibitika kuwa mgonjwa ana BPH. Zipo njia nyingi za upasuaji
wa BPH, nazo ni pamoja na upasuaji kwa kupitia kwenye mrija wa mkojo
(Transurethral surgery, TURP), upasuaji mkubwa wa wazi (Open surgery), upasuaji
wa kutumia nishati kuondoa tishu za tezi dume Laser surgery), na upasuaji wa
kutumia joto la fibreoptic probe kuchoma tishu za tezi dume (Interstitial laser
coagulation).
MADHARA
YA TIBA HIZI
1. Kukosa uwezo wa kufikia kishindo yani hutoi shahawa(RETROGRADE EJACULATION)
wazee wengi hulalamika sana baada ya hizi operation hivyo ushauri nasaha lazima
utolewe ili mgonjwa ajue nini madhara yake kabla ya operation.
2. Kuziba kwa njia ya mkojo kutoka na kuumia kwa njia hizo wakati wa kitendo
hicho. Panapokua panapona hilo kovu linaziba njia ya mkojo.
3. Operation kubwa ya kuondoa tezi hio hufanyika kwa kufungua kibofu cha mkojo
na kutoa hio tezi. Madhara ni mengi sana kuhusu njia hii.
4. Shida ya kuthibiti mkojo
usitoke ovyo (Incontinence): Ni kawaida kwa mgonjwa kushindwa kuthibiti kutoka
kwa mkojo katika siku za mwanzo baada ya operesheni. Hata hivyo hali hii
hujirekebisha baada ya siku kadhaa kupita.Kutokwa na damu: Katika siku za wali
mara baada ya TURP, kidonda kwenye tezi dume kinaweza kuvuja damu ambayo
itaonekana katika mkojo.
5. Wanaume kuwa wagumba yaani wasioweza kupata watoto. Kwa
kawaida, wakati wa tendo la ngono, mbegu za kiume kutoka kwenye korodani
huingia kwenye urethra
karibu na kijitundu cha kibofu cha mkojo.
Wakati wa tendo la ngono, misuli maalum hufunga kijitundu hicho ili kuzuia
mbegu zisiingie kwenye kibofu badala yake zielekee kwenye urethra ya katika
uume. Hata hivyo, upasuajiwa BPH huondoa misuli hiyo na kufanya mbegu kuingia
kwenye kibofu cha mkojo badala ya kuendelea
kwenye urethra ya uume. Shahawa hizo hatimaye hutolewa nje ya kibofu pamoja na
mkojo.Kufika kilele UTAFITI
UNASEMA NINI KUHUSU KUKUA KWA TEZI NA MATIBABU YAKE.
1. LYCOPENE.
-Hivi ni virutunisho vinavyotokana na nyanya. Lycopene ina uwezo wa kupenya
kwenye tezi dume na kuondoa tatizo lolote na kuzuia kabisa kukua kwa tezi dume.
Pia ina uwezo mkubwa wa kuzuia kansa ya tezi dume. Hivyo tunashauri kila mtu
mwenye umri wa miaka 30 atumie virutubisho hivi ili kujilinda na tezi kukua.
Utumiapo lycopene iliyotengenezwa kwa kiwango kingi(concentrated) kuna
uwezekano mkubwa wa kutopata kabisa tezi hii dume hata kama kwenye ukoo wenu
wote walipata tezi hii. Kama utahitaji hii bidhaa bora kabisa imetengezwa
katika mfumo wa vidonge ni asili haina madhara kwani haina chemical imetokana
na NYANYA. Tumia lycopine at least kopo mbili kwa mwaka lenye virutubisho 60
kwa mwezi mmoja ili kujiepusha kabisa na tezi tume na kansa ya tezi dume.
~Zinc ni kiondoa sumu kikubwa sana yani POWERFUL ANT OXIDANT hivyo utafiti
unaonesha utumiapo virutubisho hivi saratani ya tezi dume na kuvimba kwa tezi utaviepuka kwa asilimia 80 zaidi.
3. PROSTACARE
Dawa hii ni ya kiasili
imetengenezwa kwa kutumia viambata vifuatavyo
Extractum of Radix Rehmanniae, Rhizoma Anemarrhenae,
Cortex Phellodendri Chinsis, Herba Ecliptae, Fructus Ligustri Lucidi, Harba
Plantaginis, Radix Paeoniae Rubra Ambavyop kwa pamoja husaidia
·
Kuboresha mzunguko wa damu ndani ya tezi dume
·
Kuzuia kuzaliana kwa wadudu wabaya ndani ya
tezi dume
·
Kuondoa dalili za matatizo ya tezi dume
Inafaa kwa mwanamme mwenye tatizo lolote la
tezi dume na inawafaa Wanaume wenye umri unaozidi miaka 40 kwaajili ya
kujikinga na tezi dume
Jaribu prostate care package kutoka kwetu kwa Sh 250,000/=
J
Tutakupatia virutubisho tulivyoeleza hapo juu ili uweze kutibu tatizo lako la tezi dume na kuilinda
familia yako kwa kurudisha tendo la unyumba. Bila kusahau kingine kina ongeza
nguvu,shauku ya kufanya na kurudia tendo la ndoa.
SULUHISHO LAKO LIPO DHIDI YA TEZI DUME, USIKUBALI UVIMBE KUFKIA HATUA MBAYA NA KUTENGENEZA SARATANI. CHUKUA HATUA , LINDA AFYA YAKO KABLA HUJAUGUA .
VIRUTUBISHO
NA DAWA ZOTE HIZI ZA ASILI ZINAPATIKANA OFSINI KWETU HAPA DAR, MWEMBECHAI , KAMA UPO MKOANI
BASI USIHOFU MAANA UTATUMIWA DAWA BAADA YA KUFANYA MALIPO.
Bofya hapa Kuchati na Daktari kwenye Whatsapp
ANGALIZO
kumbuka afya yako siyo dhamana ya mtu, afya yako ina thamani kubwa kuliko pesa unayotoa hivo usiangalie gharama za dawa na kuamua kwenda mitaani kununua dawa za bei nafuu halafu ukaendelea kuwa muhanga na kuteseka na matatizo yako. tunakuhakikishia kwamba lazima utapona ukitumia dawa hizi pasipo na mashaka kabisa.
Comments
Post a Comment
TUANDIKIE UJUMBE MFUPI, JUU YA TATIZO LAKO, JINSIA, UMRI, NA MAHALI UNAKOPATIKANA