Uke wa
mwanamke hufanya kazi ya kutoa njia kati ya sehemu ya nje ya mwili na viungo
vya uzazi vya ndani vya mwanamke. Hali ya kawaida ya majimaji yaliyomo
katika uke wa mwanamke huwa ni ya tindikali ili kuzuia maambukizi ya
vijidudu wa kuleta maradhi. Hali hii ya utindikali huletwa na bacteria waishio
katika uke wa mwanamke.
Bacteria hawa ni wa kawaida na hawana madhara kwa
mwili. Uke ulio katika hali nzuri hutoa majimaji haya ili kujisafisha.
Majimaji haya yanayotengenezwa katika uke na kwenye eno la cervix hufanya kazi
ya kuondoa seli zilizokufa na bacteria waharibifu nje ya mwili na huu ndio
uchafu wa kawaida ambao mwanamke hutoa ukeni.
Kutoa uchafu huu sehemu za
siri ni njia ya kuusafisha uke na kuzuia maambukizi ya magonjwa. Kitu cho
chote ambacho kitaharibu uwiano wa utengeneaji wa majimaji haya ndani ya
uke kinaweza kujenga mazingira ya maambukizi katika uke.
- Uchafu Wa Sehemu Za Siri Wa Kawaida
Wanawake wote
hutoa uchafu sehemu za siri. Kiwango cha uchafu unaotoka, rangi yake na harufu
yake vitabalikabadilika kutoka kipindi kimoja hadi kingine kulingana na
muda mwanamke aliopo katika mzunguko wake wa mwezi. Uchafu huu utabadilika
vilevile kama ananyonyesha, atakuwa na hisia za kufanya mapenzi, atakuwa
na mabadiliko ya lishe, anatumia madawa hasa ya mpango wa uzazi au atakuwa na
ujauzito.
Kwa kawaida uchafu huu huwa usio na rangi, wenye rangi yenye
weupe wa mawingu au njanonjano pale unapokaukia kwenye nguo. Unaweza kuwa
na vijipande vidogovidogo na mara nyingine ukawa wa kunatanata.
2. Uchafu Wa Ukeni Usio Wa Kawaida
Madiliko ya
uwingi wa uchafu unaotoka au katika rangi ya uchafu unaotoka ni dalili ya
maambukizi ya magonjwa katika uke. Maambukizi katika uke ni tatizo la kawaida
kwa wanawake na wanawake wengi wameshapata tatizo la maambukizi angalau
mara moja katika maisha yao. Ukiona yafuatayo, ujue unaweza kuwa na tatizo
la maambukizi ya vijijidudu vya maradhi katika uke wako:
- Kutokwa na uchafu ukeni kunakoambatana na kuwashwa au vijipele
- Kutokwa na uchafu ukeni ambako ni endelevu na kwa kiwango kinachozidi kila siku
- Kusikia maumivu wakati wa kutoa haja ndogo Kutokwa na uchafu mweupe, mzito kama jibini
- Uchafu wa kijivu/mweupe au njano/kijani unaotoa harufu mbaya
Aina Za Uchafu Wa Ukeni Usio Wa Kawaida
Kitu chochote kitakachoharibu uwiano wa bakteria wa kawaida waishio katika uke kinaweza
kuleta mabadiliko katika rangi, harufu au muundo wa uchafu utakaotoka
katika uke. Hapa chini naonyesha aina ya uchafu unaotoka, maana yake au
chazo chake na dalili ambazo zitatokea kwenye mwili wa mwanamke husika:
- Uchafu Wenye Damu Au Wa Rangi Ya Kahawia.
Hii ni dalili
ya mzungumko wa mwezi wa mwanamke uliovurugika na mara chache ni dalili ya
kansa ya Cervix au aina nyingine ya kansa iitwayo endometrial cancer.
Mwanamke mwenye tatizo hili atatoa damu nyingi ukeni na kuumwa nyonga.
- Uchafu Wenye Rangi Ya Mawingu Au Njano
Hii ni dalili
ya ugonjwa wa kisonono (Gonorrhea). Mwanamke atatokwa na damu katikati ya siku
zake, atatokwa na mkojo bila kukusudia na kupata maumivu ya nyonga.
- Uchafu Wa Njano Au Kijani Wenye Harufu Mbaya
Endapo uchafu
utatoka kama mapovu, wenye rangi ya kijani au njano ukiambatana na harufu mbaya
, hii ni dalili ya Trichomoniasis, maambukizi (parasitic) yanayotokana na
ngono zembe. Dalili nyigine ni maumivu na kuwashwa wakati wa kutoa haja
ndogo.
- Uchafu Mweupe Mzito Kama Jibini
Hii ni dalili
ya maambukizi ya aina ya fungus (Yeast infection) na dalili nyingine
atakazozisikia mwanamke huyu ni kuvimba na maumivu kwenye sehemu za nje za
siri (vulva), kuwashwa na maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa.
- Uchafu Mweupe, Wa Njano Au Wa Kijivu Wenye Harufu Ya Samaki
Uchafu wa
aina hii ni dalili za maabukizi ya Bacterial Vaginosis. Mwanamke mwenye tatizo
hili atasikia miwasho au maumivu, kuvimba kwa uke au sehemu ya nje ya uke
(vulva).
Aina Ya
Maambukizi Ya Ukeni
Kuifanya mada
yetu iwe na maana na msaada zaidi, tutazungumzia kwa undani zaidi aina tatu za
maambukizi ya ukeni ambazo zinawasumbua wanawake wengi zaidi, ambapo
tutatazama dalili zake na kuelezea tiba ambazo zinawea kutolewa kuondoa
matatizo hayo. Hapa tutazungumzia Bacterial Vaginosis, Trichomoniasis na
Monilia (Yeast) Infection.
Bacterial
Vaginosis: Chanzo halisi cha ugonjwa huu hakifahamiki. Kinachotokea ni
kuongezeka kwa ghafla kwa idadi ya bacteria hawa na kubadilisha uwiano
wake kwenye mazingira ya uke. Wanawake wenye wapenzi wengi au wanaofanya
mapenzi kupitia midomo wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata maambukizi ya
Bacterial Vaginosis.
Dalili za
Bacterial Vaginosis:
– Kuongezeka
kwa uchafu unaotoka ukeni
– Kutokwa na
uchafu wa kijivu/mweupe, mwepesi au wa majimaji
– Harufu kama
ya samaki ikiambatana na uchafu
– Harufu
inayozidi au uchafu unaozidi mara baada ya kufanya tendo la ndoa.
Tiba kwa
tatizo la bacterial vaginosis zipo za aina mbili. Tiba ya aina ya kwanza ni
kutumia metronidazole (Flagyl) na tiba ya pili ni kutumia antibiotic
ya vidonge au ya cream.
Trichomoniasis: Maambukizi
haya hutokana na aina ya protozoa wa seli moja. Trichomoniasis
maranyingi huambukizwa kwa kufanya ngono. Protozoa huyu huweza kukaa
kwenye mazingira ya unyevunyevu kwa muda wa saa 24 bila kufa hivyo kufanya
taulo na nguo nyingine za kuogea kuwa chanzo kingine kikuu cha maambukizi.
Dalili Za Trichomoniasis
– Kutokwa na
uchafu wa rangi ya njano/kijani ulio kama mapovu
– Harufu
mbaya inayoambatana na kutokwa na uchafu
– Kuongezeka
kwa uwingi wa uchafu wa ukeni
– Maumivu ya
ukeni au sehemu za nje ya uke (vulva)
– Kujisaidia
haja ndogo mara nyingi zaidi
– Kuwashwa
sehemu za siri
Tiba ya
Trichomoniasis ni kunywa vidonge vya antibiotic, metronidazole.
Monilia
(Yeast) Infection: Kwa kawaida kuna kiwango kidogo cha yeast (Candida
albicans) katika uke. Tunasema kuna maambukizi ya yeast pale kiwango chao
kinapozidi hali ambayo inatokana na kubadilika kwa hali ya ukeni (change
in the pH balance of the vagina). Maambukizi ya yeast hayatokani na tendo la
ngono. Kuna mambo ambayo yanaweza kusababisha kuongezeka kwa yeast katika
uke, nayo ni; msongo wa mawazo, matumizi ya dawa za kuziua mimba,kisukari, ujauzito na matumizi ya antibotics.
Dalili Za
Monilia (Yeast) Infection
– Mwongezeko
wa uchafu unaotoka ukeni
– Uchafu
mweupe unaotoka katika vifungu vidogo kama vya jibini
– Kuwashwa na
mauvivu ya ukeni au sehemu za nje (vulva)
Tiba ya
Monilia (Yeast) Infection inalenga kuzuia mwongezeko wa yeast katika uke na
kuwarudisha kwenye kiwango kinachofaa na si kuwaondoa. Tiba ni kutumia
vidonge vya antifungal na cream za kupaka ukeni. Kuna dawa nyingi za
kuweza kuondoa tatizo hili.
USHAURI.
unapoona dalili hatari kama tulivoelelezea hapo juu basi fika haraka hospitali kupata vipimo na ushauri wa dactari. kama tatizo limekuwa sugu na umetumia dawa nyingi bila msaada basi usikate tamaa, unaweza kufika ofsini kwetu Mwembechai ukapata huduma ya dawa kupitimia vodonge vya mimea na ushauri ili kutibu tatizo lako.
tuandikie mda wowote.
Hakikisha tu umefanya vipimo na kujua chanzo cha tatizo lako.
Comments
Post a Comment
TUANDIKIE UJUMBE MFUPI, JUU YA TATIZO LAKO, JINSIA, UMRI, NA MAHALI UNAKOPATIKANA