Kati ya watu
watatu basi mmojawapo tayari ana ugonjwa wa kisukari ama atapata ugonjwa huu
hivi karibuni: je wewe ni mmojawapo, na hufahamu hili???
Tafiti
iliyofanyika mwaka 2015, inasema gharama zinazotumika kwenye kutibu ugonjwa wa
kisukari kwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara zinafikia dola bilioni 19.5,
hapo utaona jinsi gani tatizo linavoongezeka miaka hadi miaka na kuharibu afya
za wapendwa wetu. Sasa leo tutafahamu kisukari ni nini, aina za kisukari, nini
chanzo cha kisukari, aina ya vyakula unachotakiwa kula ili kujikinga na tatizo
hili na mwisho kama tayari umeugua na unateseka na ugonjwa wa kisukari ufanye
nini. Fuatana nami katika Makala hii ukisoma taratibu upate maarifa kwa kina.
What is
diabetes?? Kisukari ni nini??
Kisukari ni
ugonjwa wa kiutendaji (metabolic disorder) unaopelekea kupanda kwa kiwango cha
sukari kwenye damu na mwili kushindwa kustahimili tena ngezeko la sukari.
AINA ZA KISUKARI
Kuna aina kuu 2
za kisukari, aina ya kwanza ambayo kisukari cha utotoni na aina ya pili ya
kisukari ambacho ni kisukari cha ukubwani.
1.
KISUKARI CHA UTOTONI
Aina
hii ya kisukari huanza pale mtoto anapozaliwa hadi kufkia umri wa miaka 18 au
20, husababishwa na mpambano kati ya kinga ya mwili dhidi ya seli za beta
ambazo hutengeneza homoni ya insulin (homoni inayorekebisha kiwango cha sukari
kwenye damu), sasa mpambano huu hupelekea kupungua kwa uzalishaji wa insulini ama kukosekana kabisa kwa insulin kwene kongosho, na kwasababu miiili yetu imeubwa
kutumia insulini wagonjwa hawa huhitaji kudungwa sindano za insulin kila siku
ili kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu.
DALILI
ZA KISUKARI CHA UTOTONI( TYPE 1 DIABETES)
1.
Wagonjwa wenye aina hii ya kisukari huwa
wamekonda na kudhoofu sana afya zao
2. Seli za kutengeneza kichocheo cha insulin
zinakuwa zimeangamizwa kwa kiasi kikubwa kutokana na mpambano na kinga ya
mwili.
3. Kiwango cha insulin kwenye damu huwa kipo chini
sana kutokana na uwezo mdogo wa kongosho kutengeneza insulin.
KISUKARI CHA UKUBWANI (type 2
diabetes)
Aina hii ya kisukari nafahamika sana
na imekuwa janga la dunia nzima likiathiri mamia ya watu kila siku. Kinyume na
kisukari cha utotoni, aina hii ya kisukari husababishwa na kiasi kikubwa cha
insulin kwenye damu. Hivo ukiwa na kisukari cha ukubwani ni kwamba insulin io
nyingi kwenye damu na mwili hauwezi kuitumia vizuri hali hii kitalamu ni
INSULINI RESISTENSE, ama kongosho yako inatengeneza insulini nyingi lakini
imezidiwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu. Kupanda kupita kiasi kwa
kiwango cha insulin kwenye damu huweza kuletekeza ama kupelekea matatizo
mengine ya kiafya kama
- Stroke na matatizo mengine ya utendaji wa ubongo kama Alzheimer
- Kupanda kwa shinikizo la damu
- Magonjwa ya viuongo kama arthritis
- kupungua uwezo wa kuona na hatimaye Upofu
- Kitambi na uzito mkubwa
- Kufeli kwa figo
- Kurundikama kwa Mafuta mabaya kwenye viungo muhimu kama ini
- Saratani
- Upungufu wa nguvu za kiume
- matatizo ya uzazi kwa wanawake kama ugumba na uvimbe na
- matatzo ya upumuaji na alegi
Hivo magonjwa haya huambatana na
tatizo la kisukari na kadri ugonjwa unavokomaa na kufkia hatua mbaya ndivyo
magonjwa haya ambatanishi yanavojitokeza Zaidi, najua unaweza kuwa ni muhanga
wa ugonjwa huu na umeteseka kwa miaka mingi umetumia madawa mengo bila
mafanikio, napenda kukupa tumaini kuwa suluhisho lipo, ni kurekebisha lishe
yako tu na kutumia virutubisho muhimu. Ebu futa kwanza elimu za nyuma ulizopewa
na hazijakusaidia kisha pokea ushauri mpya ambao umeleta matunda kwa wagonjwa
wengie tunaowahudumia kila kukicha.
NINI KINASABABISHA UGONJWA WA
KISUKARI CHA UKUBWANI.
Kwanza kabisa ni vyema kufahamu
kwamba ugonjwa wa kisukari syo ugonjwa wa kuwa na sukari nyingi hapa, kisukari
ni ugonjwa wa homoni, homoni ya insulin, kumbuka kwamba mwili unahitaji kiwango
kidogo tu cha glucose kukibadilisha kuwa nishati ili kuendesha shuguli zake,
kiwango kingine kinachozidi huwa hakipotei bali huhifadhiwa katika seli za
mwili kwenye mfumo wa mafuta, hivo kazi ya insulin ni kusukuma sukari iliyozidi
kwenda kwenye seli ili ibadilishwe kuwa mafuta. Sasa inapotokea mwili hausikii
uwepo wa insulin kwenye damu yaani insulin inamwagwa lakini kiwango cha sukari
kwenye damu kipo pale pale hao ndipo hatari ya kuugua kisukari huanza.
Sasa ni wakati wa kutambua kwamba
aina ya chakula unachokula kinachangia kwa kiasi kikubwa kupata magonjwa haya
kama kisukari na uzito mkubwa,vyakula kama wanga na sukari hupandisha insulin
kwenye damu kwa kasi sana huku vyakula vya protini na mafuta vikithibitika
kupandisha insulin kwa kiasi kidogo sana. Kula wanga na sukari nyingi na
kufanya mazoezi sana haikusaidii kuepuka magonjwa haya ya kisukari na uzito
mkubwa badala yake kula vyakula vya mafuta kama parachichi, samaki, nyama,
mayai , nazi na mboga za majani kwa wingi muhimu.
KWANINI KUWA MWEMBAMBA SIYO KIASHIRIA
CHA AFYA NJEMA
Tafiti zinasema watu wembamba wapo
katika hatari Zaidi ya kufa endapo wakiugua kupita kiasi tofauti na watu
wanene, na mara nyingi watu wembanba hupatikana na mrundikano wa mafuta mabaya
{trigleycrides} kwenye viungo kama moyo,
ini na figo ambayo huhatarisha ufanyaji kazi wa viungo husika, Kwa bahati mbaya
ni vigumu sana kugundua hatua za mwanzo za ugonjwa wa kisukari , hii ni hutokana
na kwamba upimaji unaotumika mara nyingi ni ule wa kuangalia kiwango cha sukari
kwenye damu ambacho mara zote kinakuwa sawa mpaka pale mgonjwa anapofikia hatua
mbaya ya kuanzishiwa dozi ya kudungwa insulin.
JE KISUKARI NI UGONJWA WA KURITHI??
Nafahamu kundi kubwa la watu na
wataalamu wa afya wanaimani kubwa kwamba kisukari huambukizwa kutoka kizazi
kimoja hadi kingine, yawezekana mpenzi msomaji wa Makala hii baada ya
kushihudia wazazi wako wote wawili wakiugua ugonjwa huu sasa una mashaka kwamba
nawe utaugua kisukari, la hasha kama ukirekebisha tu lishe yako basi
nakuhakikishia hutaugua ugonjwa wa kisukari,
nadhari hii ya kurithi haina
mashiko kabisa hasa ukizingatia kwamba mpangilio wa gene hubadilika kwa 0.2%
kila baada ya miaka elfu 20, sasa iweje kuwepo na kuongezeka kwa magonjwa haya
ya kisukari ukilinganisha na enzi za mababu zetu, jibu ni kwamba mazingira na
lishe tunazokula ndizo zinabadili namna hizi gene zinavofanya kazi. Namna
tunavyokula, kiasi gani miili yetu inashugulishwa, namna tunacontrol msongo wa
mawazo, na jinsi mazingira yanayotuzunguka ikiwemo sumu na kemikali zilizopo
haya yote yanachangia kwa kiasi kikubwa kukua na kuongezeka kwa janga la
kisukari.
Unapokuwa umepunguza wanga na sukari au kuacha kabisa ulaji
wa vyakula vyenye wanga nyingi, mfano mikate,ugali,wali,tambi nk na hakikisha
kitendo hicho kiendane na kuongeza kiwango cha mafuta na vyakula vya protini
mwilini mwako katika lishe yako. Hii itaufanya mwili wako kuanza kutumia mafuta
kama nishati ya mwili ya kwanza kujitengenezea nishati. Na viungo vya binadamu
kama Ini na figo vinapokuwa vinatumia mafuta kuzalisha nishati ya mwili
hutenegeneza viini vya nishati viitwavyo KETONE BODIES, ambavyo hivi ndivyo
hutumiwa na seli za mwili kujitengenezea nishati kwa wingi.
Hivyo basi unapokuwa unajizuia kutumia vyakula vya wanga
mwili wako utatumia karibia siku 5 hadi wiki kuanza kutumia mafuta kama
nisharti ya mwili na hicho kitendo tunaita KETO ADAPTATION. Ningependa kusema
kwamba KETO ADAPTATION ni ile hali mwili wako kujenga mazoea ya kutumia mafuta
kama chanzo cha nishati ya mwili na hapo ndipo utaanza kuona mabadiriko katika
mwili wako makubwa sana.
Utakuwa unajisikia mwenye nguvu na unatashangaaa dalili
mbalimbali zilizokuwa zinakusumbua zinapotea hii ni kwa sababu ya uwezo mkubwa
wa ketone bodies katika mwili wako dhidi ya glucose.
Sote tunajua kwamba ulaji wa vyakula vya wanga kwa wingi na
vyakula vyenye sukari nyingi vinaongeza kiwango cha sukari kwenye damu Zaidi ya
kiwango ambacho mwili wako unaweza kuhimili.
Mfano, Kiwango cha kawaida cha sukari kinachohitajika
mwilini mwako ni kijiko kimoja cha chai, hiki ni kiwango ambacho hakiwezi
kukuletea matatizo. Basi kama binadamu anaishi kwa sukari inayokadiriwa kuwepo
kwenye damu kama kijiko kimoja tu cha chai. Unywaji wa soda moja unaweza
kuongeza Zaidi ya vijiko 10 hivyo basi mwili wako unakuwa unashindwa kuhimili
sukari iliyozidi. Na ulaji wa Baga inakadiliwa kuwa baga moja ya kati inaweza
kutoa sukari Zaidi ya vijiko 16 kwenye damu. Swali la kujiuliza mwili unapeleka
wapi sukari iliyozidi wakati miili yetu inahitaji sukari kiwango kidogo sana
kama kijiko kimoja tu kuishi?
Mwili hutengeneza maji kutoka kwenye seli za kongosho
ziitwazo beta seli,maji haya ni homon iitwayo INSULIN
Kama nilivoandika hapo juu kazi kubwa ya insulin ni kutunza
glucose hii katika damu kwa matumizi ya baadae, na inatunza katika kiasi
maalumu katika mfumo wa Glycogen na kiasi kikubwa katika mafuta. Na hivyo basi
mafuta haya huhifadhiwa katika sehemu mbalimbali kama
tumboni,shingoni,mikononi,kifuani,kiunoni nk. Na mafuta haya huhifadhiwa katika
mfumo wa TRYGLYCERIDES ambayo haya ni miongoni vya mafuta mabaya mwilini mwako.
Sasa mtu anayekwambia wanga nyingi katika chakula chako ni salama anakudanganya
kwa kiasi kikubwa kwani tunaona jinsi gani ulaji wa kiwango kingi cha vyakula
vya wanga na sukari vinavyo sababisha sukari kupanda kupita kiasi na
insulinkuanza kuhifadhi katika mafuta.
HATUA ZINGINE MUHIMU ZA KUZINGATIA ILI KUREKEBISHA KIWANGO
CHA SUKARI KWENYE DAMU, na kuepuka magonjwa kama kisukari, kitambi, presha kubwa ya damu, mvurugiko wa homoni, na upungufu wa nguvu za kiume.
1.
Ongeza kiwango cha vyakula
vya nyuzinyuzi au kambakamba (fibers) kwenye mlo wako kila siku. Vyakula hivi
husaidia kupunguza kasi ya usagaji wa chakula kwenye mwili kwa kunyonya maji
kwenye utumbo na hivo kusaidia kupunguza umwagaji wa insulin kila mara kwenye
damu, maana muda mwingi utajihisi umeshiba na hutahitaji kula kilamara, rejea maelezo
ya juu kuhusu madhara ya umwagaji wa insulin nyingi kwenye damu, faida nyingine
za vyakula vya kambakamba ni kupunguza hatari ya kupata kansa ya utumbo mpana
na tumbo kujaa gesi. Chanzo kizuri cha vyakula hivi ni mboga za majani, na siyo
ugali wa dona wala nafaka isiyokobolewa kama ulivoelekezwa.
2.
Punguza wanga na
sukari maana ni vyakula vinavyopandisha, kiwango cha insulin kwa kiasi kikubwa
kwenye damu, kumbuka wanga inapoingia kwenye mwili hubadilishwa kuwa sukari na
kisha uchakataji wake kuendelea kama sukari.
3.
Kula kwa wingi vyakula vya fats au mafuta, hivo mbadala wako
wa wanga na sukari uwe vyakula vya mafuta kama na protini, kama parachichi,
nazi, samaki, nyama na maziwa kutoka kwa Wanyama walifugwa kwa kula nyasi na
siyo nafaka, mafuta ya mawese, mafuta ya mizeituni, mayai ya kienyeji, na
karanga (jamii zote za karanga mbichi).
FAIDA YA MWILI KUTUMIA FATS (VYAKULA VYA MAFUTA) KUZALISHA
NISHATI YA MWILI
1. Mwili unakuwa una nguvu za kutosha unapokuwa unatumia
fats au ketone bodies kuzalisha nguvu
2. Mwili unapokuwa unatumia mafuta kuzalisha nishati
hupunguza kiwango cha cha FREE RADICALS MWILINI
3. Vyakula vya Protini,mafuta vinaonesha kutopandisha
kiwango cha insulin (Kihifadhi mafuta) kwa kiwango kikubwa kama ilivyo vyakula
vya wanga
4. Utajitibu magonjwa mengi sana kwani utazuia
utenegenzwaji wa FREE RADICALS na Advanced Glycated End Products ambavyo ni
vyanzo vya magonjwa mengi ambapo chanzo chake ni ulaji wa vyakula vya wanga kwa
wingi kupita kiasi.
4.
Mazoezi ya viungo,
kama bado upo kwenye hatua ya kwanza ya kisukari, lakni kama umefikia hatua
mbaya basi tunashauri mazoezi yaanze baada ya mwili kutengemaa
5. Pata usingizi wa kutosha kuanzia masaa 8 mpaka 9 kila siku na Epuka msongo wa mawazo ambao hupelekea
uchovyaji kwa wingi wa homoni za glucagon na cortisol mabazo zote huchangia
katika kiwango cha sukari kwenye damu.
6. Usitumie vyakula wala vinywaji vilivyokobolewa na kusindikwa badala yake kula vyakula asili ulichoandaa jikoni
mwako.
7.
Tumia virutubisho vya
omega 3 na vitamin kutoka kwenye vyanzo vilivyothibitika unaweza kupata
virutubisho hivi ofsini kwetu pia.
8.
Mwisho kabisa
hakikisha unafatilia matokeo yako kwa kufanya vipimo kila awamu, hii
itakusaidia kfikia malengo yako ya kupunguza kiwango cha sukari haraka, hasa
ukiwa kwenye program yetu ya diabetes reverse.
Huduma hii itawalega watu wote wenye ugonjwa wa kisukari,
cha mwanzo ama cha kati,bila kujali maumivu na mateso unayopata sasa ya kisukari. huduma hii imegawanywa katika siku 60. Kila awamu
itachukua siku 20. Baadhi ya huduma muhimu utakazofaidi kupitia programme hii,
1.
Utaongea moja kwa moja
na muhudumu wetu na kupata maelekezo namna ya kuanza safari yako ya kurekebisha
tatizo la kisukari
2.
Ushauri hatua kwa
hatua jinsi ya kupangilia mlo wako na kuepuka magonjwa makubwa kama presha
kisukari, upungufu wa nguvu za kiume, na mvurugiko wa homoni kwa wanawake
3. Utapata Kirutubisho kimoja kilicho kwenye mfumo wa chai cha kukusaidia katika safari yako ya kurekebisha sukari kwa Sh 50,000/= pekee
4.
Utaweza kupata ushauri
kila siku na majibu juu ya maswali yako ya kiafya.kumbuka hata kama upo mbali na ofisi yetu ya hapa Dar maeneo ya Mwembechai, kwa wale wa mikoani na nje ya nchi huduma itakufikia kwa njia ya mtandao.
Basalam pear tea
BASALM PEAR TEA ITAKUSAIDIA
- Kukarabati Beta cells za kongosho linalohusika na utoaji wa insulin,
- Kupunguza sukari na lipids kwenye damu,
- Kuzuia ufyonzwaji wa sukari katika utumbo mdogo, na kupunguza sukari kwenye mzunguko wa damu na
- Kuepusha madhara ya kisukari kama kiu na kukauka mate
Ebu fikiria kuepuka mateso ya ugonjwa wa kisukari kama
upofu, kukatwa viungo, kushindwa kuhimili tendo la ndoa, kupungua uwezo wa
kufikiri kwa kudhoofu mwili, kwa progam fupi ya siku 60 tu. Progamu hii ikiwa imefanyiwa utafiti
na kuleta matokeo makubwa kwa wagonjwa wetu. Hakikisha unamshirikisha na mwingine habari
hizi njema
Comments
Post a Comment
TUANDIKIE UJUMBE MFUPI, JUU YA TATIZO LAKO, JINSIA, UMRI, NA MAHALI UNAKOPATIKANA