Skip to main content

NINI MCHANGO WA VINYWAJI VYENYE SUKARI NYINGI NA VYAKULA VYA VIWANDANI KATIKA UPUNGUFU WA NGUVU ZAKIUME

Ndugu karibu sana katika makala zangu ambazo huzungumzia chanzo cha tatizo, namna ya kuepuka na kutibu kabisa hilo tatizo bila kukaa kuhangaikia kutibu dalili ya ugonjwa. Ni dhahili kuwa maisha yetu ya kifahari tumekuwa tunakula vyakula vyakutosha lakini vyakula hivi si vyakujenga mwili bali vinakuja na magonjwa mengi ndani yake.
Siwezi kuilaumu jamii kwa kuendelea kula vyakula hivi bila kuwa na kiasi bali ni mfumo wa afya kwa ujumla ambayo inaweka juhudi kubwa kubaini magonjwa na kutibu dalili na siyo kuweka jitihada kubwa katika kutoa elimu ya namna ya kujikinga na magonjwa na kushughurika na chanzo au mzizi wa ugonjwa.
Hivyo ni jukumu letu kuhakikisha jamii inaepukana na magonjwa haya kwani tukifanya hivyo utamaduni huu wa kutuletea vyakula vinavyo dhoofisha miili yetu na hatimaye wanaleta misaada ya matibabu inayo lenga kubaini magonjwa na sio kutoa elimu ya kuzuia na kupambana na vyanzo hasa vya tatizo.
Baada ya kusema hivyo basi ningependa kwa siku ya leo nizungumzie kidogo madhara ya vyakula vyenye sukari nyingi na nguvu za kiume ambazo hadi sasa wanaume ambao hawawezi kutungisha mimba idadi inaongezeka. Kumekuwa na usemi kuwa upungufu wa nguvu za kiume unahusishwa sana na kuzeeka kwa mtu. Ni dhahiri kuwa kuzeeka kwako sio chanzo cha wewe kupata upungufu wa nguvu za kiume na hutakiwi kuhusisha bali ni tabia yako inayo ambatana na ulaji wa vyakula na unywaji wa vinywaji vyenye sukari nyingi,unywaji pombe,uvutaji sigara, utumiaji wa madawa ya hospitali bila ushauri maalumu na pia utumiaji madawa ya hospitali pale unapotibu ugonjwa flani kwa mfano dawa za kifafa, dawa za usingizi na dawa za dege dege,utumiaji wa madawa ya kulevya na kujichua kila siku. Hivyo maisha yetu ya kila siku ndio chanzo cha ukosefu wa nguvu za kiume
NINI MCHANGO WA VINYWAJI VYENYE SUKARI NYINGI NA VYAKULA VYA VIWANDANI KATIKA UPUNGUFU WA NGUVU ZAKIUME
Tumekuwa tukiishi mazingira ya kula vyakula vya sukari kila siku kwa mfano, ukiamka asubuhi unakula mikate, tafiti zinasema kuwa mkate una aina ya wanga iitwayo amylopectin  ambayo endapo ikimeng”enywa ni chanzo cha sukari nyingi sana kwenye damu. Pia unatakiwa kufahamu kuwa slice mbili za mikate ni sawa kama umeramba vijiko viwili vya sukari ya mezani yani sukari nyeupe. Hivyo mikate ni moja ya vyakula vyakuepuka sana kama unahitaji kuwa na afya njema na mwenye nguvu za kiume tele.
Pia imekuwa ni kawaida unaamka asubuhi na soda kwani hii ni ishara kuwa tayari kiini mahususi kwenye soda ambacho huitwa ASPARTAME kimesha kuaathiri na umekuwa addicted na vyakula vya sukari. Aspartame ni kiambata mahususi kwenye vinywaji vya koka na hivyo kimewekwa humo ili kukufanya uwe na hamu ya kunywa soda mara kwa mara au kula vyakula vitamu vitamu. Kiini hiki huenda kwenye ubongo na kujishika kwenye vipokea taarifa yani receptors na kutoa taarifa ambazo zina angamiza mwili wako.
Sukari inapozidi mwilini inasababisha uchovyaji wa insulin kwa wingi ambayo hupunguza kiasi cha testosterone ndani ya ndamu na hatimaye kupunguza nguvu na shauku ya tendo la ndoa. Kulingana na utafiti uliofanywa kwa kutumia kipimo cha sukari kiitwacho ORAL GLUCOSE TORELANCE TEST AU OGT kinaonesha kuwa wanaume wenye sukari nyingi kwenye mzunguko wa damu walionesha kiwango kidogo cha kichocheo cha nguvu za kiume kiitwacho testosterone ambacho hushughurika na sifa za kiume,kutengeneza mbegu za kiume na kuimarisha misuli bila kusahau nguvu za kiume.
Ni dhahili kuwa ongezeko kubwa la wanaume ambao wana matatizo ya nguvu za kiume inasababishwa na ulaji na unywaji wa vyakula vyenye sukari nyingi. Hivyo basi ni dhahiri kuwa kama una tatizo hilo linaweza kukupelekea kukosa mtoto kwani hata manii ya kiume kutengenezwa kwake itakuwa ni kwa shida sana. Epuka hivi vyakula na jua namna gani unaweza rudisha afya yako mwanzo kwa kutumia vyakula na virutubisho mahususi vinavyo ondoa tatizo la nguvu za kiume.
Pia vyakula vya sukari nyingi hupunguza kwa hali ya juu vichocheo vya kujenga mwili yani GROWTH HORMONE ambayo hutolewa na tezi ya pituitary wakati wa usingizi mzito. Kichocheo hiki cha kujenga mwili yani GROWTH HORMONE kinafanya kazi kubwa ya kutumia mafuta yaliyohifadhiwa kwa matumizi ya ziada, pia growth hormone huimarisha misuli ya mwili na kuimarisha nguvu za kiume. Hivyo kupungua kwa kichocheo hiki husababisha mrundikano wa mafuta mabaya na kutengeneza nyama zembe yani BELLY FAT, kuongezeka uzito,kupata kizuizi cha insulin na hatimaye kisukari aina ya pili.
Vyakula vya sukari nyingi hukufanya muda wote ujihisi umechoka na huna nguvu ya kufanya kazi yoyote na wengine hufikiria kuwa wanasumbuliwa na ugonjwa wa malaria. Hii ni kwa sababu sukari nyingi kupita kiasi inasababisha utoaji wa insulin kuongezeka ili kupunguza sukari hiyo na matokeo yake kusababisha njaa na shauku ya kula mara kwa mara. Pia sukari nyingi huzuia utengenezwaji wa kichocheo kiitwacho OREXIN ambacho husafirisha taarifa na kuongoza kitendo cha ulaji na kukufanya uwe na nguvu ya kuwa macho na kufanya kazi zako. Sasa orexin inapopungua inasababisha muda wote kukaa umechoka na unasinzia ovyo ovyo. Ni dhahiri kuwa unaweza kuwa unasoma hii makala ni miongoni mwa waathiriwa wa sukari nyingi kwani uzito umekuzidi,kitambi,unasinzia ovyo ovyo na muda wote umechoka. Usihofu na usikate tama chakula cha matunda na mboga mboga ndio suluhisho lako kama wewe huwezi kutumia hivi basi jitahidi kutafuta virutubisho vyenye kurudisha afya yako upya bila usumbufu kabisa.
Pia sukari nyingi kwenye damu husababisha msongo wa mawazo sana na hatimaye kusababisha utolewaji wa vichocheo vya CORTISOL ambayo husababisha ulaji ovyo wa vyakula wa bila mpangilio. Mtu kama huyu utakuta unakula pale pale baada ya muda mfupi tena njaa. Hivyo tujifunze namna gani sasa unaweza kuirudisha afya yako bila tena kuendelea kuongeza sumu mbali mbali mwilini. 
Napenda nikupongeze msomaji wangu ni jukumu lako kujua nini cha kufanya kama wewe bado hujafikia kuathiriwa na tatizo hili. Hivyo basi nina imani utailinda afya yako na kuipenda. Chakula cha mimea na matunda kinakuweka mbali na dawa hizi kwani tusipende kula vyakula vyenye nembo ya kuisha muda wake. Kwa Yule tayari ameshakumbwa na tatizo hili kwa sababu ya matumizi ya sukari nyingi napenda kukuambia kuwa CHAKULA PEKEE NI TIBA KABISA NA KUJIEPUSHA NA DAWA ZA KILA SIKU UNAZO NUNUA AMBAZO HAZITIBU TATIZO. Kama huwezi kupangilia chakula chako vizuri na namna ya kurudisha tatizo lako unaweza tumia viutubisho vinavyo ondoa tatizo na kurudia kuwa kijana. Wasiliana nasi ili upate maelekezo ya kufika ofisini
 Tuandikie msg au whatsapp namba 0678626254 (whatsapp tu) na  0762336530 sms+call au tembelea page yetu ya facebook; mkumbohealthcareproducts.

Unaweza kushare Makala hii ili tuzidi kufundishana na kulinda afya zetu

Comments

Popular posts from this blog

KUTOKWA NA UCHAFU UKENI, CHANZO NA TIBA YAKE

Uke wa mwanamke hufanya kazi ya kutoa njia kati ya sehemu ya nje ya mwili na viungo vya uzazi vya ndani vya mwanamke. Hali ya kawaida ya majimaji yaliyomo katika uke wa mwanamke huwa ni ya tindikali ili kuzuia maambukizi ya vijidudu wa kuleta maradhi. Hali hii ya utindikali huletwa na bacteria waishio katika uke wa mwanamke. Bacteria hawa ni wa kawaida na hawana madhara kwa mwili. Uke ulio katika hali nzuri hutoa majimaji haya ili kujisafisha. Majimaji haya yanayotengenezwa katika uke na kwenye eno la cervix hufanya kazi ya kuondoa seli zilizokufa na bacteria waharibifu nje ya mwili na huu ndio uchafu wa kawaida ambao mwanamke hutoa ukeni. Kutoa uchafu huu sehemu za siri ni njia ya kuusafisha uke na kuzuia maambukizi ya magonjwa. Kitu cho chote ambacho kitaharibu uwiano wa utengeneaji wa majimaji haya ndani ya uke kinaweza kujenga mazingira ya maambukizi katika uke. Uchafu Wa Sehemu Za Siri  Wa Kawaida Wanawake wote hutoa uchafu sehemu za siri. Kiwango cha uchafu unaotoka, ra

JINSI YA KUONGEZA UFANISI WA VICHOCHEO VYA KIUME (TESTOSTERONE) NA KUKINGA DHIDI YA MATATIZO YATOKANAYO NA KUKUA KWA TEZI DUME KWA KUTUMIA VYAKULA HIVI VI 5

Maelezo ya utangulizi. Kichocheo cha testosterone, japo huusishwa zaidi na upande wa mwananume ni muhimu kwa afya ya pande zote mbili yaani mwanamke na mwanamme pia.kadiri umri unavoenda mbele basi kiwango cha uzalishaji wa kichocheo cha testerone kupungua, kupungua kwa kichocheo hiki kunaambatana na ukuaji wa tezi dume (prostate gland),kupotea kwa nywele na pia saratani mfano saratani ya tezi dume. .KAZI KUBWA YA KICHOCHEO HIKI NI KUONGEZA MSUKUMO NA HAMU YA TENDO LA NDOA , KUIMARISHA MISULI NA MIFUPA MWILINI. NINI KINAHITAJIKA ILI KUZALISHA KICHOCHEO CHA TESTOSTERONE? Ili kuhakikisha uzalishaji wa kichocheo cha kiume unafanyika, mwili unahitaji virutubisho au viini lishe mbalimbali, baadhi ya viini lishe hivyo ni madini ya ZINC na vitamin D3,  vitamini D inaweza kuzalishwa na mwili pale ngozi yako inapokutana na mwanga wa jua, hapa nazungumzia mwanga wa asubuhi wakati jua ndo linachomoza na pia lile jua la jion karibia na kuzama, hivyo utakubaliana na mimi kuwa wengi wet

MADHARA YA PUNYETO NA TIBA YAKE

MAELEZO  YA AWALI KUHUSU TATIZO LA UPIGAJI PUNYETO Watu wengi sana wanataka kufahamu jinsi gani wafanye ili kuachana na kitendo cha upigaji punyeto. Punyeto ni tendo la mtu la kuamsha hisia za mapenzi au msisimko ambao unampelekea mtu huyu kufikia kilele cha kujimalizia tamaa zake! Bila kufanya tendo halisi, hutumia fikra zake katika picha za zinazoitwa za ngono au picha zozote zinazoweza kulifanikisha tendo hilo, movie n.k. Kilele cha yote anafikia mahali anajimalzia tamaa zake mwenyewe!. Nimekuwa nikiona baadhi ya watu wanaosema wameelimika wakipingana wao kwa wao katika suala zima la kupiga punyeto! Wako wanaotetea kutokana na elimu yao na wanasema kwa ujasiri mkubwa kwamba "kupiga punyeto ni sehemu ya maisha ya mwanadamu" Ina maana katika maisha ya mwanadamu upigaji punyeto inaelezwa ni kama tendo la lazima mpaka inafikia mahali wanasema ni sehemu ya maisha (Maisha) ya mwanadamu. Nimekuwa nikipata kesi nyingi sana juu ya madhara yatokanayo na punyeto. Aslimia 60