Skip to main content

JE UNATAFUTA TIBA YA MAUMIVU YA VIUNGO NA MGONGO?? SOMA MAKALA HII

Maumivu ya joint ni tatizo linalosumbua watu wengi kwa sasa kutokana na mabadiliko ya mitindo ya Maisha. Umri mkubwa ni moja ya sababu inayopelekea kutokea kwa tatizo, ambapo tishu za mwili zinakuwa kavu na kupoteza uwezo wa kuvutika. Watu wengi wanfikiri kwamba kufanya mazoezi ni hatari kwa afya ya joints lakini ukweli ni kwamba ili kuepuka magonjwa ya joints mazoezi ni lazima katika akuongeza ufanisi wa viungo pia. 
Nina uhakika kuwa umewaona akina mama wenye umri mkubwa na miili mikubwa wanavyopata shida kutembea huku wakiinama toka upande mmoja hadi mwingine kila wakipiga hatua au shida wanayopata pale inapowabidi kupanda ngazi au kukuchuchumaa. Maneno kama “ugonjwa wa kuumwa joints, nina tatizo la joints, maumivu ya joints” na maumivu ya mifupa umeyasikia mara nyingi. Tatizo hasa hapa ni nini? Ungana nami katika mada hii uujue ugonjwa huu wa arthritis.


 UGONJWA WA ARTHRITIS NI NINI?

 Arthritis ni ugonjwa unaotokana na namna yo yote ya hitilafu katika maungio ya mifupa ya binadamu ambao husababisha maumivu na pengine kuvimba katika sehemu moja au zaidi ya maungio hayo. Neno arthritis halilengi ugonjwa mmoja bali jamii ya magonjwa ambayo kwa ujumla yapo zaidi ya 100. Tabia kuu ya magonjwa haya ni maumivu kwenye maungio ya mifupa (joints) ambayo ni endelevu na ambayo hutokea eneo hilo moja.
 CHANZO CHA ARTHRITIS NI NINI?
 Kusudi kuelewa chanzo cha ugonjwa huu, hebu kwanza tutazame muundo wa joint au sehemu mifupa miwili inapokutana. Fikiria goti ambapo mifupa miwili mmoja wa paja na mwingine wa mguu vinapokutana:
 Ligaments: Ndicho kitu kinachoshikilia mifupa hii miwili pamoja. Hii ni kama utepe wa plastiki au mpira unaonyumbuka uliozunguka eneo hilo kwa nje, ukikunja goti inanyumbuka na ukinyoosha mguu inarudi.
Cartilage: Huu ni utando unafunika eneo ambalo mifupa hugusana ili kuzuia mifupa hii isisuguane moja kwa moja. Utando huu ambao kwa kiswahili tunauita gegedu huyawezesha maungio hayo kufanya kazi kiulaini pasipo kusababisha maumivu.
Capsule: Hiki ni kitu kinachofunika maungio haya kikizunguka pande zote. Ndani ya mfuko huu wa capsule kuna synovial fluid ambayo huzalishwa na synovial membrane. Synovial fluid ni ute wa kulainisha sehemu hiyo ya maungio na synovial membrane ni utando ulio kwenye kuta za ndani za capsule.
 Ugonjwa wa arthritis unasababishwa na hitilafu yoyote katika sehemu hizo za maungio ya mifupa. Inaweza kuwa cartilage inalika, upungufu wa synovial fluid, maambukizi ya vijidudu katika moja ya maeneo hayo au mchanganyiko wa matatizo.
 AINA ZA UGONJWA WA JOINTS-ARTHRITIS
Kama nilivyoeleza hapo juu, kuna aina zaidi ya 100 za ugonjwa huu wa joints au arthritis. Katika mada yetu ya leo tutatazama aina kama nne hivi za ugonjwa huu, tukielezea chanzo cha kila aina.
OSTEOARTHRITIS: Hii ni aina ya arthritis inayosumbua watu wengi zaidi kuliko aina nyingine zote. Ugonjwa huu huwapata zaidi watu wenye umri mkubwa. Osteoarthritis hutokea pale cartilage inapopoteza uwezo wake wa kubonyea na kuwa ngumu hivyo kuharibika haraka. Cartilage ni kiungo cha kuhimili migandamizo ya ghafla (shock absorber). Cartilage hii inapopoteza ubora wake, tendons na ligaments huvutika na kusababisha maumivu. Hali ya uharibifu huu wa cartilage ikiendelea, mwishowe mifupa huanza kusuguana moja kwa moja na ndipo mgonjwa atakapoanza kupata maumivu makali sana.
Athari za ugonjwa huanza taratibu na kuongezeka na muda. Kutaanza kutokea maumivu kwenye joint baada ya kufanya shuguli fulani au baada ya mapumziko ya muda mrefu. Joints zitakaza, hasa mapema asubuhi unapotaka kuanza shughuli zako za kawaida. Siku zinavyosogea ndivyo utakavyoona ni vigumu zaidi kukitumia kiungo chako. Mara nyingine utaona uvimbe kwenye joint. Osteoarthritis hushambulia zaidi nyonga, mikono, magoti na uti wa mgongo.
RHEUMATOID ARTHRITIS: Ugonjwa huu hutokea pale mfumo wa kinga ya mwili kwa bahati mbaya kuanza kushambulia viungo vya mwili ikiwa ni pamoja na synovial membrane (synovium) na kusababisha uvimbe na maumivu. Hali hii isipodhibitiwa, huweza kusababisha ulemavu.  Ugonjwa huu unaweza pia kushambulia macho, ngozi, mapafu, midomo, damu na mishipa ya damu. Huu ni ugonjwa ambao zaidi ni wa wanawake na huwatokea zaidi wawapo kati ya umri wa miaka 40 hadi 60. Mgonjwa atasikia maumivu na kuona uvimbe kwenye joints za pande zote za mwili, yaani kama ni magoti, yote mawili la kulia na la kushoto, yote yatashambuliwa. Viungo vinavyoshambuliwa zaidi ni vidole, viwiko vya mikono na miguu.
Athari zake huonekana zaidi asubuhi unapoamka na maumivu yanaweza kudumu kwa muda wa hadi nusu saa. Muathirika wa ugonjwa huu hujisikia mchovu muda wote, hukosa hamu ya kula na hupungua uzito.
INFECTIOUS ARTHRITIS (SEPTIC ARTHRITIC): Aina hii ya arthritis inatokana na maambukizi ya bacteria kwenye synovial fluid. Maambukizi haya yanaweza kuwa pia ni ya fungus au virusi. Wadudu kutoka sehemu nyingine ya mwili iliyo karibu na maungio ya mifupa huweza kusambaa kupitia mfumo wa damu hadi kwenye joint na kuleta maambukizi. Mara nyingi mtu mwenye aina nyingine ya arthritis ndiye anayepata maambukizi ya namna hii. Mgonjwa ataanza kwanza kupata homa, maumivu na uvimbe kwenye joint. Maeneo ambayo hushambuliwa zaidi na aina hii ya arthritis ni goti, mabega, kiwiko cha mkono, kiganja (wrist) na vidole na mara nyingi ni eneo moja tu ndilo litakaloshambuliwa.
JUVENILE RHEUMATOID ARTHRITIS (JRA): Juvenile rheumatoid arthritis (JRA) ni ugonjwa ambao huwapata zaidi vijana walio na umri ulio chini ya miaka 16 na unakuja kwa namna nyingi. Kuna aina kuu tatu za ugonjwa huu:
1. Pauciarticular JRA, huu ndiyo unaoonekana zaidi na hauna madhara makubwa ukilinganisha na aina nyingine. Mtoto atasikia maumivu kwenye joints zinazofikia nne.
2. Polyarticular JRA, huu hushambulia joints nyingi zaidi, zaidi ya nne na maumivu yake ni makali zaidi. Kadri siku zinavyoongezeka, ndivyo maumivu yatakavyozidi.
3. Systemic JRA, huu huonekana kwa nadra ambapo maumivu hujitokeza kwenye maeneo mengi na madhara yake kuwa makubwa zaidi.
Mtoto ataanza kusikia homa za vipindi ambapo huzidi zaidi nyakati za jioni. Hali hii inaweza kumtokea mtoto kwa muda mfupi au kwa wengine kwa muda mrefu sana . Mtoto atapata mauvimu kwenye maungio ya mifupa (joints), uvimbe kwenye maungio hayo na kukakamaa kwa viungo. Mtoto huyu atakosa hamu ya kula hivyo kumfanya akonde. Ugonjwa ukizidi, mtoto anaweza kudumaa (kushindwa kukua), ukuaji wa mifupa yake kuathirika  na kupata matatizo ya macho 


MAFUTA ASILI YA EUCALYPTUS NA FRANKINCENCE

Kazi na faida ya mafuta haya

  •             Kuondoa maumivu makali ya viungo yanayotokana na arthrits
  •             Kuzuia kutokea kwa magonjwa ya viungo
  •    Mafuta haya yanawafaa zaidi wenye matatizo ya viungo na mgongo, wagonjwa wenye matatizo ya gout, na wenye matatizo ya kumomonyoka kwa kifupa (osteoporosis).
   

VIRUTUBISHO VYOTE HIVI VINAPATIKANA OFSINI KWETU HAPA DAR MAENEO YA MWEMBECHAI, hivo huhitaji kuagiza nje ya nchi, Tayari tumefanya utafiti kuhusu ubora wake unaweza kufika kwa kuwasiliana nasi moja kwa moja kupitia .

Gharama ya mafuta ni Tsh 20,000/=

Bofya hapa kuchati Na muhudumu kwenye Whatsap Kuagiza Mafuta 


Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUGUNDUA NA KUTHIBITI VIDONDA VYA TUMBO( PEPTIC ULCER)

MAELEZO YA UTANGULIZI KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO Tunashukuru kwa kuendelea kufatilia makala zetu, kwa maoni na ushauri ama uhitaji wa kufika ofisini basi endelea kutuandikia kwa namba  0714206306 .  Kupata ufahamu mpana juu ya vidonda vya tumbo ni vema kuelewa kwanza mfumo unaohusika na tumbo ambao ni umen'genyaji wa chakula. Sehemu kuu zinazohusika katika umen'genyaji huo ni kinywa,umio ambayo ni misuli wenye urefu wa sentimeta 23 ambao huunganisha koromeo na tumbo'esophagus',mfuko wa nyongo na sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo'duodenum',utumbo mdogo,kongosho,utumbo mpana na sehemu ya mwish oni ya utumbo'rectum'. Mfumo wa mmen'genyo wa chakula hasa kuta za umio,tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na tindikali inayotumika kumen'genya chakula inaposhambulia kuta hizo, hii ndiyo vidonda vya tumbo'Peptic Ulcers',vidonda vya mfumo wa umen'genyaji chakula vikiwa kwenye tumbo ni 'Gastric Ulcer'vikiwa kati...

Kisonono ni nini ?, je kuna Tiba ya kisonono ?

Nini maana ya kisonono, je naweza kupata tiba sahihi ya kisonono?  Soma makala jii upate kujifunza na kupata ueewa juu ya tatizo la kisonono ambalo limeathiri watu wengi sana kwa sasa hasa vijana wa kiume. Kisonono au kwa lugha ya kitaalamu Gonorrhea ni moja ya ugonjwa wa ngono ambao huambukizwa baada ya mtu mmoja mwenye ugonjwa kukutana kimwili mtu mwingine mzima. Kisonono mara nyingi husababisha maumivu makali na dalili zingine mbaya kwenye via vya uzazi na sehemu zingine kama, sehemu ya haja kubwa, macho na pia maumivu ya viungo. Ugonjwa huu wa kisonono huweza kuwapata watu wa jinsia zote wanawake kwa wanaume huku tafiti zikionesha kwamba wanaume ndio wanaoongoza kuambukizwa kuliko wanawake. Nnini husababisha kinonono au Gonorrhea?? Ugonjwa huu wakuambukizwa kwa njia ya ngono husababishwa na bacteria wanaoitwa Neisseria gonorrhoeae. Na hivo pale watu wanapokutana kingono bacteria hawa huweza kusambaa kwenda kwa mtu mwingine kutokana na msuguano wa viungo laini vya uza...

UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE

 FAHAMU TATIZO LA UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE (OVARIAN CYST ) Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovary) hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana kama ovarian cyst. Uvimbe huu unaweza kumtokea mwanamke wa umri wowote ingawa mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito. MAYAI YA MWANAMKE  Kwa kawaida mwanamke anakuwa na mayai mawili katika mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto. Mayai haya hupatikana pembezoni mwa mfuko wa uzazi (uterus). Mayai haya huanza kuzalisha mayai ya uzazi yanayojulikana kama ovum  ambapo mayai hayo ya uzazi hukuwa ndani ya mayai ya mwanamke (ovary) kwa kuchochewa na baadhi ya homoni.  Katikati ya mwezi, siku ya kumi na nne, saa 24-36 baada ya kiwango cha kichocheo aina ya Luteinizing Hormone kuwa juu, mayai ya uzazi hutolewa k...