Moja ya vyakula ambavyo tumekuwa tukitumia kwa wingi sana
hasa kwa watanzania wenye kipato cha kati na chini kabisa ni vyakula vya aina
kuu tatu, WANGA,PROTINI NA MAFUTA (FATS). Na kwa kiwango kidogo sana tunatumia
vitamin na madini katika miili yetu. Na moja ya masomo ya chakula
tunayofundishwa ni kula MLO KAMILI. Na ndio watu wengi tumekuwa tukitumia elimu
hio hadi hapa tulipo fika. Lakini basi napenda kusema tu kwamba mlo kamili ni
kwa ajili ya mtu mzima ambaye hana ugonjwa wowote na ni kwa yule tu ambaye
hataki kula kiafya.
Napenda kusema haya
kwa sababu tumekuwa tukila vyakula vya namna ile ile lakini tumekuwa tukiugua
sana magonjwa mbalimbali yatokanayo na lishe mbovu. Na hadi sasa ugonjwa wa
kisukari hapa duniani unaua sana Zaidi ya ugonjwa wa HIV sasa ni swala la
kujiuliza tunakosea wapi mbali katika
lishe?
Leo nataka nikueleze kidogo kuhusu sayansi ya chakula aina
ya wanga. Maana kila mtu ninayemwelekeza njia sahihi ya kupunguza uzito anakwambia
nitaishije bila chakula cha wanga? Mwili wako hutumia vyakula vikuu aina tatu
ambavyo ni wanga,protini na fats. Na unatakiwa ujue kuwa gramu moja ya wanga
hutengeneza nishati ya mwili kalori 4, ambapo protini nayo hutengeneza kalori 4
na Fats hutenegenza kalori 9. Unaona ni Zaidi ya mara mbili ya nishati
zinazotengenezwa na chakula cha wanga. Hii ina maana kuwa ninaposema kuwa
tunaweza kupunguza wanga na ukaishi ukiwa na nguvu nyingi Zaidi hata ya ulivyo
kuwa katika lishe ya wanga nyingi.
KWA NINI NAKUSHAURI UPUNGUZE WANGA NA SUKARI KIAFYA?
Unapokuwa umepunguza wanga na sukari au kuacha kabisa ulaji wa vyakula
vyenye wanga nyingi, mfano mikate,ugali,wali,tambi nk na hakikisha kitendo
hicho kiendane na kuongeza kiwango cha mafuta na vyakula vya protini mwilini
mwako katika lishe yako. Hii itaufanya mwili wako kuanza kutumia mafuta kama
nishati ya mwili ya kwanza kujitengenezea nishati. Na viungo vya binadamu kama
Ini na figo vinapokuwa vinatumia mafuta kuzalisha nishati ya mwili hutenegeneza
viini vya nishati viitwavyo KETONE BODIES, ambavyo hivi ndivyo hutumiwa na seli
za mwili kujitengenezea nishati kwa wingi.
Hivyo basi unapokuwa unajizuia kutumia vyakula vya wanga
mwili wako utatumia karibia siku 5 hadi wiki kuanza kutumia mafuta kama
nisharti ya mwili na hicho kitendo tunaita KETO ADAPTATION. Ningependa kusema
kwamba KETO ADAPTATION ni ile hali mwili wako kujenga mazoea ya kutumia mafuta
kama chanzo cha nishati ya mwili na hapo ndipo utaanza kuona mabadiriko katika
mwili wako makubwa sana.
Utakuwa unajisikia mwenye nguvu na unatashangaaa dalili
mbalimbali zilizokuwa zinakusumbua zinapotea hii ni kwa sababu ya uwezo mkubwa
wa ketone bodies katika mwili wako dhidi ya glucose.
Sote tunajua kwamba ulaji wa vyakula vya wanga kwa wingi na
vyakula vyenye sukari nyingi vinaongeza kiwango cha sukari kwenye damu Zaidi ya
kiwango ambacho mwili wako unaweza kuhimili.
Mfano, Kiwango cha kawaida cha sukari kinachohitajika
mwilini mwako ni kijiko kimoja cha chai, hiki ni kiwango ambacho hakiwezi
kukuletea matatizo. Basi kama binadamu anaishi kwa sukari inayokadiriwa kuwepo
kwenye damu kama kijiko kimoja tu cha chai. Unywaji wa soda moja unaweza
kuongeza Zaidi ya vijiko 10 hivyo basi mwili wako unakuwa unashindwa kuhimili
sukari iliyozidi. Na ulaji wa Baga inakadiliwa kuwa baga moja ya kati inaweza
kutoa sukari Zaidi ya vijiko 16 kwenye damu. Swali la kujiuliza mwili unapeleka
wapi sukari iliyozidi wakati miili yetu inahitaji sukari kiwango kidogo sana
kama kijiko kimoja tu kuishi?
Mwili hutengeneza maji kutoka kwenye seli za kongosho ziitwazo beta seli,maji haya ni
homon iitwayo INSULIN
Kazi kubwa ya insulin ni kutunza glucose hii katika damu kwa
matumizi ya baadae, na inatunza katika kiasi maalumu katika mfumo wa Glycogen
na kiasi kikubwa katika mafuta. Na hivyo basi mafuta haya huhifadhiwa katika
sehemu mbalimbali kama tumboni,shingoni,mikononi,kifuani,kiunoni nk. Na mafuta
haya huhifadhiwa katika mfumo wa TRYGLYCERIDES ambayo haya ni miongoni vya
mafuta mabaya mwilini mwako. Sasa mtu anayekwambia wanga nyingi katika chakula
chako ni salama anakudanganya kwa kiasi kikubwa kwani tunaona jinsi gani ulaji
wa kiwango kingi cha vyakula vya wanga na sukari vinavyo sababisha sukari
kupanda kupita kiasi na insulinkuanza kuhifadhi katika mafuta.
Kila siku nasema, tumekaririshwa adui mkuu ni fats, na
kujisahau ulaji mbovu wa vyakula vya wanga na hatimaye tumeishia kulea vitambi
na magonjwa sugu hii yote ni kutokuwa na ufuatiliaji wa lishe nzuri na salama
kwako.
NINI MADHARA MENGINE YA SUKARI KUWA KATIKA KIWANGO KIKUBWA
KUZIDI MAHITAJI YA KAWAIDA YA MWILI?
Napenda kuwarudisha nyuma kidogo katika somo la bailojia.
Tulijifunza kuwa miili yetu umejengwa kwa kiini kidogo sana kiitwacho SELI
ambapo shughuli zote za mwili zinafanyika humo. Na nilipo fika mbali Zaidi
katika bailojia nilijifunza kuwa ndani ya seli kuna viungo vidogo vidogo
navifananisha na ( Apartments kwenye
nyumba kubwa) moja wapo ni MITOCHONDRIA, hiki ni kiungo kidogo sana katika seli
ambacho kinahusika na kuzalisha nishati ya mwili tu.
Mfano, una nyumba yako kubwa sana na hio nyumba ukaitenga
kuwa ya biashara na kila chumba ukakiwekea majukumu yake na mitambo yake. Hivyo
basi kile chumba kimoja ukakiwekea mitambo ya kufua umeme na ndicho kitafanya
shughuli zote zifanyike katika kiwanda chako ndani ya hio nyumba ya kibiashara.
Hicho chumba cha kufua umeme nakifananisha na MITOCHONDRIA ndani ya seli ya
binadamu ambayo hushughurika na kutenegeneza nishati ya mwili ndani ya seli.
Pia nikikumbuka watu wote tulijifunza kwamba mwili wetu
hujitenegenezea nishati ya mwili au nguvu kupitia kuifanyia kazi sukari iliyo
ndani ya damu baada ya kuingia ndani ya seli. Hivyo basi insulin ni kama
ufunguo ambao unafungua milango ili sukari iweze kuingia ndani ya seli hadi
kwenye mitochondria. Baada ya kufika huko, mwili huanza kuzalisha nishati na
kuitoa katika mfumo wa ATP kupitia kitendo cha AEROBIC RESPIRATION. Kitendo
hiki hufanyika ndani ya seli ndani ya mitondria kwa kuwepo na hewa ya oxygen.
Hewa hii lazima iwepo ili mwili uweze kuzalisha nishati ya kutosha uweze
kufanya kazi mbalimbali.
Mwili wako unapokuwa unatumia hewa ya oxygen kuna uwezekano
mkubwa wa kupatikana kwa athari iitwayo OXDATIVE STRESS. Hii ndio inayofanya
chuma ipate kutu, hii ndio inayofanya mafuta ukiyaweka kwenye jua kwa muda
mrefu yanaharibika. Basi mwili wako unakuwa unatengeneza vihatarishi viitwavyo
REACTIVE OXYGEN SPECIES kwa kifupi huitwa FREE RADICALS. Hizi free radicals ni
sumu ambazo hupatikana wakati mwili unajitenegenezea nishati yake kwa kutumia
oxygen na hizi zinapokuwa kiwango kikubwa huweza kuharibu kabisa seli na kuziua
na pia zinaweza kupelekea kupata magonjwa sugu kama kansa nk. Hivyo tafiti
zinaonesha kwamba vyakula vya wanga na sukari vina matokeo makubwa ya
kutenegeneza FREE RADICALS nyingi kupita kiasi. Miili yetu ina kiwango flani
cha viondoa sumu ambavyo vinaipunguza
sumu ya free radicals kuepusha kusababisha magonjwa kwa kuziua seli.
Lakini panapokuwa na kiwango kikubwa cha uzalishaji wa free radicals mwili
unashindwa kuhimili na hatimaye free radicals zinaanza kuleta madhara mwilini
mwako. Kadri mitochondria zinavyo dhoofika ndivyo magonjwa nyemelezi ya lishe
yanavyotukabili kila kukicha.
MADHARA YA FREE RADICALS
1. Hudhoofisha seli zako na kusababisha mwili kutofanya kazi
ipasavyo
2. Huua kabisa seli za mwili
3. Huweza kubadili seli za mwili wako na kuwa kansa
Pili kunapokuwa na sukari nyingi katika damu, sukari nyingi
katika damu huwa ipo katika mfumo wa kimiminika mfano wa dawa za maji za watoto (syrup) au juisi ya embe
inayokumwagikia mkononi chukulia mfano huo. Sukari iliyozidi huungana na protin
katika tishu za mwili na kutenegeneza kitu kiitwacho GLYCATION. Muungano huo
ufanya protini zisiweze kufanya kazi na hatimaye kuishia hatua ya mwisho
iitwayo ADVANCED GLYCATED END PRODUCTS (AGEs) ambacho ni kiini kinacho ambatana
na magonjwa mengi, magonjwa ya kusau,magonjwa ya kisukari,magonjwa ya
kutetemeka uzeeni,baridi yabisi,upungufu wa nguvu za kiume,maumivu ya
misuli,uchovu wa muda mrefu,macho kutoona vizuri nk. Advanced Glycated end
products pia ndio chanzo kikubwa kinacho ua nguvu za macho kwa wagonjwa wa
kisukari,figo,miguu kufa ngazi nk
FAIDA YA MWILI KUTUMIA FATS KUZALISHA NISHATI YA MWILI
1. Mwili unakuwa una nguvu za kutosha unapokuwa unatumia
fats au ketone bodies kuzalisha nguvu
2. Mwili unapokuwa unatumia mafuta kuzalisha nishati
hupunguza kiwango cha cha FREE RADICALS MWILINI
3. Vyakula vya Protini,mafuta vinaonesha kutopandisha
kiwango cha insulin (Kihifadhi mafuta) kwa kiwango kikubwa kama ilivyo vyakula
vya wanga
4. Utajitibu magonjwa mengi sana kwani utazuia utenegenzwaji
wa FREE RADICALS na Advanced Glycated End Products ambavyo ni vyanzo vya
magonjwa mengi ambapo chanzo chake ni ulaji wa vyakula vya wanga kwa wingi
kupita kiasi.
FIKRA POTOFU ZITAKAZO KUPOTOSHA KATIKA SAFARI YAKO KIAFYA
Najua kuna watu wanashangaa kwa nini nasema kuwa ili uweze
kushusha uzito na kitambi lazima tupigane vita na wingi wa vyakula vya wanga
katika mlo wako na sio mafuta kama wengi tulivyokaririshwa. Adui yetu mkuu ni
sukari na huyo kila siku tumpinge na rafiki yetu katika kupunguza uzito ni
vyakula vya mafuta,protini,mboga za majani na baadhi ya matunda hasa yenye
nyuzi nyingi.
1. Wataalamu wengine watakuambia Ubongo hautumii chanzo cha
nishati yoyote isipokuwa wanga? Sasa wewe unaye acha wanga utaishi vipi? Hii ni
kauli inatufanya tuzidi kulea vitambi kila siku.
Ni kweli ubongo,seli za retina za jicho na seli za figo
hutegemea sukari itokanayo na wanga kuzalisha nishati ya kufanyia kazi. Lakini
napenda kusema kuwa usigubikwe na uelewa mdogo wa sayansi ya kupungua uzito wa
mtaalamu wako. Napenda kukuambia kuwa, ili mwili wako ubadirilke uwe machine
inayo unguza mafuta tunashauri kiwango cha wanga kiwe chini ya gramu 50 tu.
Yani namaanisha kuwa hicho kiwango utakipata katika vyakula vyenye kiwango
kidgo cha wanga kama mboga za majani,protini na baadhi ya matunda nitakayo
kuruhusu utumie na sio upotoshaji kwamba ule kaugali kadogo kumaanisha kuwa
unatumia wanga kidogo! Wanga utaipata kwenye aina zingine za vyakula.
Hivyo
basi ubongo wako utaishi hai kwa kutumia wanga ambao utaipata kwenye mboga za
majani,protini na baadh ya matunda ambapo si Zaidi za gramu 50 utapata. Kiasi
kingine mwili huzalisha glucose kwa njia kuu mbili kwenye Ini la binadamu,
Gluconeogenesis na Glycogenolysis hivyo mwili wako utapata nishati za kutosha
kwa zile seli zinazotegemea glucose kufanya kazi. Na hio ndiyo sayansi ya
kupungua uzito, kwamba mwili ukisha maliza kutumia chakula cha protini ,mafuta
ulicho kula, basi mwili utaanza kutumia mafuta yaliyohifadhiwa kama nyama
uzembe na hapo ndipo mwili wako utabadirika kuwa mashine inayo unguza mafuta.
Na sio kuhifadhi mafuta tena maana hakuna sukari inayozidi kwenye damu, sukari
yote inayopatikana inatumka kuendesha shughuri za mwili.
2. Wataalamu watakwambia Ketone bodies ambazo ni vyanzo vya
nishati ambavyo huzalishwa pale mwili unapotumia mafuta kama chanzo cha nishati
ni sumu kwenye neva za fahamu na hatari sana.
Hii nimekuwa nikisikia wataalamu baadhi wanajaribu kuoanisha
jinsi gani elimu ya ketones bodies kwa watu wenye kisukari aina ya kwanza
inavyo wapata. Ukweli ni kwamba ketone bodies ndio chanzo cha pekee
kinachokufanya hata leo hii upo hai. Kama ingekuwa sumu ungekuwa basi hatupo na
wewe hapa duniani kwa sababu unapokuwa hujala angalau masaa 8 mpaka 16 mwili
wako huanza kuzalisha niashati mbadala kutokana na ketones kwa sababu sukari
imeisha mwilini.
Sasa kumbuka mwili wako unatumia ketone huku kiwango chako
cha insulin kipo sawa na kiwango kinacho jitosheleza, na kwa wagonjwa
wakisukari aina ya kwanza huzidiwa na ketone bodies kwa sababu huwa hawana
kabisa insulin kwenye damu yao.
Sasa je unaona utofauti hapo, ketone zinazotumika wakati una
insulin ya kutosha na ketone inapozalishwa kwa mtu ambaye hana insulin ya
kutosha.Hivyo basi nazani umeelewa jinsi gani tunavyoishi kwa kutumia kiini
hiki cha nishati baada ya mwili kukaa muda mrefu hujala badi unatafuta njia
mbadala wa kutumia mafuta kuzalisha nishati ya mwili. Sasa iweje leo hii ketone
ni sumu? Usipotoke soma upate maarifa ya sayansi ya kupungua uzito.
3. JE AINA HII YA MLO NI SAWA NA KUJINYIMA KULA
(STARVATION)?
Kujinyima kula kunafanya uzito kuongenezeka kwa kasi ya
ajabu, hii ni kwa sababu unapokuwa umekaa muda mrefu bila kupata chakula mwili
wako unatenegeneza homoni ziitwazo stress homones ambazo ni pamoja na Cortisol
hii inakufanya ulaji hovyo na kuongezeka uzito tofauti na ulivyotarajia.
Na mlo huu una utofauti sana na kujinyima maana kujinyima ni
kutokula chakula chochote ambazo sivyo ninavyofundisha mimi kila siku.
Unapokuwa huli,umefunga labda siku 5 mwili wako utaanza
kutumia protini za kwenye misuli na hatimaye mwili kuanza kudhoofika, hio ni
hali ya kutopungua kiafya. Lakini kama ukifuatilia mlo huu, mwili utaanza
kwanza kutumia lishe ambayo umekula kama mboga za majani,protini, na fats kwa
wingi na baada ya hapo mwili utaanza kuunguza mafuta. Namaanisha kuwa mwili wako
utatumia lishe uliyokula na baada ya hapo utaanza kuunguza mafuta, Je ni sawa
na mtu yaliyefunga? Hapana! Ninachokushauri jifunze sayansi ya kupungua uzito
na lishe kwa ujumla.
MAMBO YA KUZINGATIA
1. Najua umekuwa ukijitahidi kujinusuru na uzito mkubwa na
magonjwa mengi, lakini umekuwa mvivu wa kuamini lishe yako ndio chanzo cha
magonjwa yako yote uliyo nayo, ndio maana umekuwa ukitibu dalili za magonjwa
yako sugu badala ya kushughurikia tatizo kuanzia kwenye seli na jinsi gani
lishe zinavyofanyiwa kazi ndani ya seli.
2. Wengi wetu ni wavivu wa kutunza afya zao na wanaona kuwa
wanastahili kuwa katika hali hizo ambapo sio kweli, maana uzito huo hukuzaliwa
nao,kitambi hicho hukuzaliwa nacho, kwa nini leo iwe kama ni medali ya
ukubwani? Naona uchukue hatua kunusuru afya yako.
UKITAKA KUTIBU MAGONJWA MENGI TABIA, AU MAGONJWA YA LISHE
MBOVU ANGALIA CHANZO CHAKE KUANZIA KWENYE SELI JINSI GANI VIINI LISHE
VINAVYOFANYIWA KAZI.
SHARE NA MARAFIKI ZAKO MAKALA HII ILI WAPATE KUELIMIKA ZAIDI.
na ukiwa na swali ama maoni usisite kutuandikia kwa namba yetu 0762336530.
na ukiwa na swali ama maoni usisite kutuandikia kwa namba yetu 0762336530.
Comments
Post a Comment
TUANDIKIE UJUMBE MFUPI, JUU YA TATIZO LAKO, JINSIA, UMRI, NA MAHALI UNAKOPATIKANA