Skip to main content

Posts

Showing posts from August, 2016

FIGO NA VIHATARISHI 8 USIVYOFAHAMU VYA FIGO

1. NYAMA NYEKUNDU Protini ni muhimu kwa afya zetu, lakini kama figo zako zina hitilafu, ama ulishawahi kupata vipimo na kujua kuwa figo zako haziwezi kuhimili vyakula vyenye protini nyingi sanasana ile protini itokananyo na nyama nyekundu basi unahitaji kupunguza matumizi makubwa ya nyama nyekundu na badala yake ukatumia vyakula vingine vyenye protini kama samaki, mayai, maharage, na karanga. 2.CHUMVI Kwa  baadhi ya watu matumizi makubwa ya chunvi yanaweza kuongeza chembechembe za protini kwenye mkojo, hii inaashiria kwamba figo yako haiko vizuri kiafya na pia inaweza kuashiria kufanyika kwa mawe kwenye figo (kidney stones) ambayo yanaweza kuleta dalili kama maumivu makali pembeni mwa tumbo, na maumivu wakati wa kukojoa. 3. UVUTAJI WA SIGARA Uvutaji wa sigara siyo tu unaongeza presha ya damu na kusababisha  kisukari ambayo ni magonjwa yanayoongoza kusababisha matatizo ya figo lakini pia uvutaji wa sigara hupunguza mzunguko wa damu kwenye figo nahivyo kuletekeza mat