Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2017

GOUT, USHAURI NA TIBA

MAELEZO YA UTANGULIZI KUHUSU UGONJWA WA GOUT Gout ni aina ya ugonjwa wa arthrits ambao anaambatana na maumivu makali kwenye joint, kuvimba kutokana na mrundikano wa uric asidi ambayo hujikusanya na kufanya kama jiwe gumu kwenye joint. Hapo zamani gout ulijulikana kama ugonjwa wa wafalme (a disease of Kings) kutokana na unywaji wao wa pombe na vyakula vya kukidhi raha zao. Mfalme Henry wa VIII wa Uingereza ni mmoja ya wafalme waliougua ugonjwa huu. Alexander the great, Christopher columbus, Sir Isaack newton ni baadhi ya watu maarufu ambao waliugua ugonjwa wa Gout.kibaya zaidi ni kwamba namba ya watu wanaougua ugonjwa huu kwa sasa inaongeza taratibu haijalishi unatoka familia ya kitajiri ama laa. GOUT NI NINI HASA Huu ndio ugonjwa wa joints ambao huwashambulia sana na kuwapa maumivu makali wanaume. Wanawake pia huweza kuathirika na ugonjwa huu hasa baada ya kukoma hedhi. Ugonjwa huu huleta maumivu makali ya ghafla, hasa kwenye sehemu linapoanzia dole gumba la mguu. Dalili za u

Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake

Nimekuwa Napata kesi nyingi sana kutoka kwa akina mama hasa  wenye umri kuanzia miaka 25 na kuendelea wakihitaji msaada kwenye ndoa zao, maana hawafurahii tendo la ndoa kama vile inavotakiwa. Tatizo linazidi kuongezeka kwa kasi na wengi hawafahamu chanzo cha tatizo hili hivo inakuwa vigumu kulitibu. Leo tutaongelea chanzo cha tatizo na jinsi ya kuepuka na kulitibu ili uendelee kufurahia unyumba.    SABABU ZA KUPATA MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA     1.        KUVIMBA kwa kuta za uke kutokana na kushambuliwa na fangasi (candida Albicans) au bakteria. Kuta hizi huanza kuwa na vijitundu vidogo vidogo na kadiri muda unavyokwenda bila kutibiwa, vitundu hivi huongezeka ukubwa na kuwa kama vidonda na hatimaye kuta za uke kuanza kumomonyoka na hali hii huondoa kabisa hamu ya kushiriki tendo.     2.        Matatizo ya shingo ya kizazi (cervical incompetence) kutokana na maambukizi ya fangasi maeneo hayo. Kutoka kwa mbegu za kiume muda mfupi  au saa kadhaa baada ya tendo ni dalili

IJUE HOMA YA INI(HEPATITIS B)

Hepatitis B(homa ya ini/selimundu)ni mojawapo ya magonjwa yaliyo katika kundi la magonjwa ya zinaa(STD). Magonjwa mengi ya zinaa yanatibika lakini kuna baadhi ambayo hayana tiba ya uhakika kama HPV,hepatitisB na C na HIV.Mengine yameanza kuwa sugu kutokana na matumizi ya dawa za antibiotics bila mpangilio.Magonjwa hayo ni kama gono(gonorrhea),kaswende n.k. Homa hii ya Hepatitis B inapewa uzito mdogo sana licha ya kuwa ni hatari kubwa.Hata hivyo wapo wengine ambao hawaufahamu ugonjwa huu.Kwa wanaoujua wanakiri kuwa ugonjwa huu unamadhara makubwa pengine kuliko saratani na ukimwi.Wataalam wanaeleza kuwa Hepatitis B(homa ya ini) ni ugonjwa unaoambukizwa kwa urahisi wenye madhara makubwa na uwezo wa kuambukizwa kwa wepesi kuliko ukimwi. Kitaalam ugonjwa huu husababishwa na virus vya Hepatitis B(HBV)ambayo huathiri mfumo wa utoaji wa sumu mwilini.Robo tatu ya watu ulimwenguni yasemekana wameathiriwa kwa muda na homa ya ini na wengine milioni 350 wameathirika moja kwa moja.Takwimu z