Skip to main content

FIGO NA VIHATARISHI 8 USIVYOFAHAMU VYA FIGO










1. NYAMA NYEKUNDU

Protini ni muhimu kwa afya zetu, lakini kama figo zako zina hitilafu, ama ulishawahi kupata vipimo na kujua kuwa figo zako haziwezi kuhimili vyakula vyenye protini nyingi sanasana ile protini itokananyo na nyama nyekundu basi unahitaji kupunguza matumizi makubwa ya nyama nyekundu na badala yake ukatumia vyakula vingine vyenye protini kama samaki, mayai, maharage, na karanga.

2.CHUMVI

Kwa  baadhi ya watu matumizi makubwa ya chunvi yanaweza kuongeza chembechembe za protini kwenye mkojo, hii inaashiria kwamba figo yako haiko vizuri kiafya na pia inaweza kuashiria kufanyika kwa mawe kwenye figo (kidney stones) ambayo yanaweza kuleta dalili kama maumivu makali pembeni mwa tumbo, na maumivu wakati wa kukojoa.

3. UVUTAJI WA SIGARA

Uvutaji wa sigara siyo tu unaongeza presha ya damu na kusababisha  kisukari ambayo ni magonjwa yanayoongoza kusababisha matatizo ya figo lakini pia uvutaji wa sigara hupunguza mzunguko wa damu kwenye figo nahivyo kuletekeza matatizo ya figo.

4. UNYWAJI WA POMBE

Matumizi makubwa ya pombe ni hatari kwa afya yako, wanaume wanaotumia zaidi ya chupa 14 kwa week na wanawake wanaotumia zaidia ya chupa 7 kwa week wapo katika hatari kubwa mara mbili ya kuugua magonjwa ya figo.

5. MATUMIZI YA SODA

Matumizi ya soda mbili kwa siku yanakuweka katika hatari kubwa ya kupata magonjwa ya figo.

6. UPUNGUFU WA MAJI

Figo zako zinahitaji maji safi kwa wingi ili kufanya kazi vizuri. Kutopata maji kwa wingi husababisha matatizo ya figo, unywaji wa maji vizuri husaidia kusafisha sumu na kupunguza hatari ya kuzeesha figo.

7. VIDONGE VYA KUPUNGUZA MAUMIVU

Matumizi ya mara kwa mara ya vidonge vya kupunguza maumivu mfano aspirini, ibuprofen huleta madhara kwenye figo zako. Ongea na tabibu wako kama kuna kuna njia ingine unaweza kutumia kupunguza maumivu  badala ya kumeza vidonge.

8. MADAWA YA KULEVYA

Matumizi ya cocaine, herion na madawa mengine ya kulevya huleta madhara na kupunguza utendaji kazi wa figo yako. Baadhi ya dawa hizi huongeza presha ya damu na kupelekea kutofanya kazi vizuri kwa figo.
Kama una maoni ama ushauri ama unahitaji tiba basi usisite

Kubofya hapa kuchati na Daktari kwa Whatsapp 


 utapata tiba na virutubisho kwa gharama ya sh 90,000/=   Kumbuka kushare pia na marafiki na ndugu

Usiache kufuatilia makala yetu inayofuata: Jinsi ya kujikinga na mawe kwenye figo pasipo kumeza vidonge. 

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUGUNDUA NA KUTHIBITI VIDONDA VYA TUMBO( PEPTIC ULCER)

MAELEZO YA UTANGULIZI KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO Tunashukuru kwa kuendelea kufatilia makala zetu, kwa maoni na ushauri ama uhitaji wa kufika ofisini basi endelea kutuandikia kwa namba  0714206306 .  Kupata ufahamu mpana juu ya vidonda vya tumbo ni vema kuelewa kwanza mfumo unaohusika na tumbo ambao ni umen'genyaji wa chakula. Sehemu kuu zinazohusika katika umen'genyaji huo ni kinywa,umio ambayo ni misuli wenye urefu wa sentimeta 23 ambao huunganisha koromeo na tumbo'esophagus',mfuko wa nyongo na sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo'duodenum',utumbo mdogo,kongosho,utumbo mpana na sehemu ya mwish oni ya utumbo'rectum'. Mfumo wa mmen'genyo wa chakula hasa kuta za umio,tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na tindikali inayotumika kumen'genya chakula inaposhambulia kuta hizo, hii ndiyo vidonda vya tumbo'Peptic Ulcers',vidonda vya mfumo wa umen'genyaji chakula vikiwa kwenye tumbo ni 'Gastric Ulcer'vikiwa kati...

Kisonono ni nini ?, je kuna Tiba ya kisonono ?

Nini maana ya kisonono, je naweza kupata tiba sahihi ya kisonono?  Soma makala jii upate kujifunza na kupata ueewa juu ya tatizo la kisonono ambalo limeathiri watu wengi sana kwa sasa hasa vijana wa kiume. Kisonono au kwa lugha ya kitaalamu Gonorrhea ni moja ya ugonjwa wa ngono ambao huambukizwa baada ya mtu mmoja mwenye ugonjwa kukutana kimwili mtu mwingine mzima. Kisonono mara nyingi husababisha maumivu makali na dalili zingine mbaya kwenye via vya uzazi na sehemu zingine kama, sehemu ya haja kubwa, macho na pia maumivu ya viungo. Ugonjwa huu wa kisonono huweza kuwapata watu wa jinsia zote wanawake kwa wanaume huku tafiti zikionesha kwamba wanaume ndio wanaoongoza kuambukizwa kuliko wanawake. Nnini husababisha kinonono au Gonorrhea?? Ugonjwa huu wakuambukizwa kwa njia ya ngono husababishwa na bacteria wanaoitwa Neisseria gonorrhoeae. Na hivo pale watu wanapokutana kingono bacteria hawa huweza kusambaa kwenda kwa mtu mwingine kutokana na msuguano wa viungo laini vya uza...

UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE

 FAHAMU TATIZO LA UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE (OVARIAN CYST ) Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovary) hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana kama ovarian cyst. Uvimbe huu unaweza kumtokea mwanamke wa umri wowote ingawa mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito. MAYAI YA MWANAMKE  Kwa kawaida mwanamke anakuwa na mayai mawili katika mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto. Mayai haya hupatikana pembezoni mwa mfuko wa uzazi (uterus). Mayai haya huanza kuzalisha mayai ya uzazi yanayojulikana kama ovum  ambapo mayai hayo ya uzazi hukuwa ndani ya mayai ya mwanamke (ovary) kwa kuchochewa na baadhi ya homoni.  Katikati ya mwezi, siku ya kumi na nne, saa 24-36 baada ya kiwango cha kichocheo aina ya Luteinizing Hormone kuwa juu, mayai ya uzazi hutolewa k...