Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2016

UNACHOTAKIWA KUFAHAMU KUUSU SHINIKIZO LA DAMU.(Bp)

Je una shaka kuusu shinikizo lako la damu? Je upo kwenye usalama ama hatari??, kama unamaswali mengi juu ya presha ya damu basi hauko peke ako, watu wengi wanaishi bila kufahamu shinikizo lao la damu, nashauri kama unahitaji kuwa na afya nzuri basi hakikisha unafahamu kiwango cha presha yako ya damu. KWANN NI MUHIMU KUFAHAMU Presha ya damu iliyo ya kawaida ni kipimo kizuri cha afya ya moyo. Kiwango cha damu kinachosukumwa na pia uwezo mzuri wa mishipa ya damu kutanuka na kusinyaa.hivo presha ya damu inaweza kuongezeka endapo kuna kiwango kikubwa cha damu ama mishipa haiwezi kutanuka vizuri, hali hii ni ya kawaida kwani hutokea sana pale mtu anapofanya mazoezi, tatizo linakuja endapo hali hii ikawa ni ya mwendelezo.. Hapo moyo unahitaji kufanya kazi kubwa sana ili kufanya damu iendelee kutembea mwili.   Kikawaida Namba mbili hutumika kupima presha ya damu, systolic na diastolic. Kama systolic ni 120-139 mmHg na diastolic ni 80-89mmHg basi upo kwenyq hatari ya kupata shinik

ZIJUE FAIDA YA KUTUMIA TANGAWIZI, HUTIBU MAGONJWA

MAELEZO YA UTANGULIZI Tangawizi Ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa Tangawizi. Mmea huu unafanana sana na Binzari ikiwa bado haijamenywa maganda yake. Na kwa hapa Tanzania Tangawizi hulimwa sana mikoa ya nyanda za juu Kusini na baadhi ya mikoa kama Kilimanjaro, baadhi ya maeneo ya mkoa wa Manyara, Morogoro, na kwingineko nchini. Pia kama bidhaa inapatikana nchi nzima kwa bei nafuu kabisa na kila mtu mwenye uwezo wowote wa kiuchumi anaweza kununua aidha kwa kipande kimoja, fungu au kwa kilo pia. Tangawizi inatumikaje ?: Mmea huu unaweza kuonekana kama mmea wa kawaida na watu kuutumia tu kama mazoea lakini Kiungo hiki kinaweza kutumiwa kama Dawa. Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kikiwa kimekaushwa na kutengenezwa unga. Nini Faida ya Tangawizi? Tangawizi ni mmea kati ya mimea mingi yenye maajabu, Mmea huu unaweza kutumika kama dawa na kutibu magonjwa mengi tu zaidi ya 72 yaliyo ndani ya miili yetu na kutuacha tukiwa wazima na kutekeleza majukumu

MASUNDOSUNDO /VIGWARU /GENITAL WARTS

Genital warts ni nini? Ni vinyama Laini vidogovidogo vinavyoota kwenye ngozi au utando Laini unaozunguka maeneo ya sehemu za siri, vinyama hivyo vinaweza kutokea kwenye uume, uke, mrija wa mkojo (urethra), maeneo yanayozunguka haja kubwa na sehemu mbalimbali za mwili, ~Ugonjwa huu unaenezwa kwa njia ya kujamiiana (SEXUAL TRANSMITTED INFECTION) STI) CHANZO CHA TATIZO HILI ~Ugonjwa wa Masundosundo husababishwa na virus waitwao HUMAN PAPILLOMA VIRUS ( HPV) hata hivyo Kuna Aina tofauti za virus wa HPV hivyo sio wote wanaosababisha tatizo hili kwani Kuna ambao wanaosababisha Masundosundo katika sehemu tofauti kama vile mkono, mgongoni, mguuni nk pia HPV huweza kasababisha saratani ya shingo ya kizazi(CARCINOMA OF THE CERVIX) kwa wanawake, na pia huweza kusababisha saratani ya sehemu ya haja kubwa (ANAL CANCER) kwa jinsia zote mbili ~Ugonjwa huu wa Masundosundo umejitokeza kwa kiasi kikubwa baada ya kuwepo kwa janga la UKIMWI hivyo watu wenye wapenzi wengi, wanaofanya mapenzi kwa nji

UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA

WATU wengi wanasumbuliwa na tatizo hili ambalo huwafanya kuwa na uoga na aibu wa kuelezea na kushindwa hata kwenda hospital kupata tiba JE, UNAJUA BAWASIRI/HEMORRHOIDS NI NINI? Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na Inje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe. ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles. Tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30 mpaka 50 AINA ZA BAWASIRI Kuna Aina kuu mbili za bawasiri (A) BAWASIRI YA NDANI Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili Aina