Skip to main content

UGONJWA WA PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE AU MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI)na jinsi ya kupata tiba sahihi

Maelezo ya awali ya ugonjwa wa PID

Habari za siku ndugu zangu ni matumaini yangu mnaendea vizuri. Kutokana na kundi kubwa la wanawake wamekuwa wakiteseka na tatizo hili, bila kupata msaada wa tiba huku wakibaki na madhara makubwa kama ugumba, , basi leo hii napenda nianze na ugonjwa wa PID(PELVIC INFLAMMATORY DISEASE AU MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI )
UGONJWA WA PID NI NINI??
~ni ugonjwa wa maambukizi unaotokea katika via vya uzazi wa mwanamke ambapo huhusisha maambukizi katika shingo ya kizazi (CERVICITIS),nyama katika mfuko wa uzazi (ENDOMETRITIS) na mirija ya uzazi (SALPINGITIS)

VYANZO NA VIHATARISHI VYA KUPATA UGONJWA WA PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE)

Vimelea aina ya NEISSERIA GONORHOEAE pamoja na CHLAMYDIA TRACHOMATIS ndio chanzo cha maambukizi ya ugonjwa wa PID ingawaje kuna aina kadhaa za vimelea vinahusishwa kusababisha ugonjwa wa PID hivyo nilivyotaja ndio vinaongoza Kwa umaarufu kusababisha ugonjwa wa PID
~pamoja na vimelea hao kuwa chanzo kikuu cha ugonjwa wa PID zipo njia kadhaa hatarishi kusababisha maambukizi haya Nazo ni ÷

  • kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi(IUCD) kama njia mojawapo ya uzazi wa mpango
  • Kufanya ngono isiyo salama
  • Maambukizi ya njia za uzazi mara baada ya kujifungua au mimba kuharibika
  • Kuambukizwa kupitia damu yenye vimelea wa PID
  • Kupata maambukizi wakati wa kutoa mimba kwa njia isiyo salama


DALILI/VIASHIRIA VYA UGONJWA WA PID
Kuna dalili mbalimbali zinazoweza kuashiria ugonjwa huu wa PID miongoni mwa dalili hizo ni

  • Mwanamke kupata maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu
  • Kupata maumivu wakati wa kukojoa
  • Kupata homa na kuhisi kichefuchefu
  • Kupata maumivu ya mgongo na kutapika
  • Kutokwa na hedhi bila mpangilio
  • kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
  • Kutokwa na uchafu(utoko)mweupe ukeni unaotoa harufu mbaya


NAMNA YA KUJIEPUSHA NA UGONJWA WA PID
Pamoja na kuwepo kwa dawa za kutibu tatizo hili ni vyema ukajiepusha na  vihatarishi vya kupata tatizo hili kwa kuzingatia yafuatayo
  • Epuka kufanya ngono isiyo salama.
  • Jiwekee tabia ya kufanya vipimo mara kwa mara hasa kizazi
  • Usifanye mapenzi mara baada ya kujifungua au mimba kutoka mpaka utakapohakikisha shingo ya uzazi imefunga vema
  • Kuwahi kuonana na daktari unapoona dalili za ugonjwa
  • Kuwa msafi na kula lishe bora
  • Note:Uonapo dalili za ugonjwa huu wahi kupata matibabu kwani ugonjwa huu ni mkubwa huweza kusababisha ugumba  ikiwa hautapata tiba vizuri


MATIBABU
Ugonjwa huu unatibika vizuri kwenye tiba asili hivo kama tayari unaumwa na umezunguka mahospitali bila msaada  basi tunaweza kukusaidia,

Tupigie kwa namba 0762336530 au 
Bofya hapa Kuchati na Daktari kwa Whatsapp

Dawa zinagarimu sh 50,000 tu.
Ofisi zetu zipo Magomeni Mwembechai.
 Kama upo mkoani usipate shaka maana utatumiwa dawa baada ya kufanya malipo.
USISAHAU KUSHARE NA RAFIKI

    Usiache kufuatilia makala yetu inayofuata:  Nini kinapelekea mwanamke kukosa Hmu ya tendo la ndoa?

Comments

Popular posts from this blog

KUTOKWA NA UCHAFU UKENI, CHANZO NA TIBA YAKE

Uke wa mwanamke hufanya kazi ya kutoa njia kati ya sehemu ya nje ya mwili na viungo vya uzazi vya ndani vya mwanamke. Hali ya kawaida ya majimaji yaliyomo katika uke wa mwanamke huwa ni ya tindikali ili kuzuia maambukizi ya vijidudu wa kuleta maradhi. Hali hii ya utindikali huletwa na bacteria waishio katika uke wa mwanamke. Bacteria hawa ni wa kawaida na hawana madhara kwa mwili. Uke ulio katika hali nzuri hutoa majimaji haya ili kujisafisha. Majimaji haya yanayotengenezwa katika uke na kwenye eno la cervix hufanya kazi ya kuondoa seli zilizokufa na bacteria waharibifu nje ya mwili na huu ndio uchafu wa kawaida ambao mwanamke hutoa ukeni. Kutoa uchafu huu sehemu za siri ni njia ya kuusafisha uke na kuzuia maambukizi ya magonjwa. Kitu cho chote ambacho kitaharibu uwiano wa utengeneaji wa majimaji haya ndani ya uke kinaweza kujenga mazingira ya maambukizi katika uke. Uchafu Wa Sehemu Za Siri  Wa Kawaida Wanawake wote hutoa uchafu sehemu za siri. Kiwango cha uchafu unaotoka, ra

JINSI YA KUONGEZA UFANISI WA VICHOCHEO VYA KIUME (TESTOSTERONE) NA KUKINGA DHIDI YA MATATIZO YATOKANAYO NA KUKUA KWA TEZI DUME KWA KUTUMIA VYAKULA HIVI VI 5

Maelezo ya utangulizi. Kichocheo cha testosterone, japo huusishwa zaidi na upande wa mwananume ni muhimu kwa afya ya pande zote mbili yaani mwanamke na mwanamme pia.kadiri umri unavoenda mbele basi kiwango cha uzalishaji wa kichocheo cha testerone kupungua, kupungua kwa kichocheo hiki kunaambatana na ukuaji wa tezi dume (prostate gland),kupotea kwa nywele na pia saratani mfano saratani ya tezi dume. .KAZI KUBWA YA KICHOCHEO HIKI NI KUONGEZA MSUKUMO NA HAMU YA TENDO LA NDOA , KUIMARISHA MISULI NA MIFUPA MWILINI. NINI KINAHITAJIKA ILI KUZALISHA KICHOCHEO CHA TESTOSTERONE? Ili kuhakikisha uzalishaji wa kichocheo cha kiume unafanyika, mwili unahitaji virutubisho au viini lishe mbalimbali, baadhi ya viini lishe hivyo ni madini ya ZINC na vitamin D3,  vitamini D inaweza kuzalishwa na mwili pale ngozi yako inapokutana na mwanga wa jua, hapa nazungumzia mwanga wa asubuhi wakati jua ndo linachomoza na pia lile jua la jion karibia na kuzama, hivyo utakubaliana na mimi kuwa wengi wet

MADHARA YA PUNYETO NA TIBA YAKE

MAELEZO  YA AWALI KUHUSU TATIZO LA UPIGAJI PUNYETO Watu wengi sana wanataka kufahamu jinsi gani wafanye ili kuachana na kitendo cha upigaji punyeto. Punyeto ni tendo la mtu la kuamsha hisia za mapenzi au msisimko ambao unampelekea mtu huyu kufikia kilele cha kujimalizia tamaa zake! Bila kufanya tendo halisi, hutumia fikra zake katika picha za zinazoitwa za ngono au picha zozote zinazoweza kulifanikisha tendo hilo, movie n.k. Kilele cha yote anafikia mahali anajimalzia tamaa zake mwenyewe!. Nimekuwa nikiona baadhi ya watu wanaosema wameelimika wakipingana wao kwa wao katika suala zima la kupiga punyeto! Wako wanaotetea kutokana na elimu yao na wanasema kwa ujasiri mkubwa kwamba "kupiga punyeto ni sehemu ya maisha ya mwanadamu" Ina maana katika maisha ya mwanadamu upigaji punyeto inaelezwa ni kama tendo la lazima mpaka inafikia mahali wanasema ni sehemu ya maisha (Maisha) ya mwanadamu. Nimekuwa nikipata kesi nyingi sana juu ya madhara yatokanayo na punyeto. Aslimia 60