Skip to main content

Posts

Showing posts from November, 2016

VYAKULA 6 BORA NA MUHIMU KWENYE MLO WAKO

Lishe ni moja ya nguzo kubwa kwenye afya ya mtu, na ndio maana unatakiwa uanze kutazama kwa jicho la karibu, kama ulikuwa unajali zaidi kazi huku ukibugia vyakula vibovu naviita junk foods, bila kutambua madhara makubwa ya kiafya yanayoletekezwa na vyakula huku ukijikuta unatumia pesa zote ulizotolea jasho kuhudhuria matibabu, basi anza kugeuka ssasa, uweze kutumia pesa kidogo kununua chakula bora na uepushe magonjwa mengi kama kisukari, saratani na magonjwa ya moyo. Unachokula si tu kinafanya mwili unawiri na kuongeza nguvu pia kinaongeza ufanisi wa mwili katika kufanya shughuli zake kama usagaji wa chakula na usafirishaji wa chakula na takamwili.   Kama ulaji wako ni mbovu unaotegemea vyakula vilivyosindikwa na fast foods, ambavyo si tu vinakosa baadhi ya virutubisho muhimu bali pia vinakuja na sumu nyingi zikiwemo vionjo viongeza utamu (artificial sweeters) zitakazorudisha nyuma afya ya mwili wako. Kinyume kabisa na vyakula asili ambavyo vitakupa vitamin za kutosha, madini, kuk...

FAIDA ZA KABEJI KIAFYA

Napenda kuwashukuru wote ambao mmekuwa mkishiriki katika masomo yangu, sasa kupitia ukurasa wangu wa facebook utajifunza mboga za majani zina umuhimu gani mwilini mwako. Hakikisha unaungana nami facebook kwenye ukurasa wa Mkumbo healthcare products ili uendelee kupata elimu hii adimu ambayo imekuwa na shuhuda nyingi sana na inaweza kuokoa gharama zako nyingi sana katika kuokoa afya yako.Unaweza kualika na marafiki zako waweze kulike page hii ili wajifunze zaidi. KABEJI Kabeji ni miongoni mwa mboga za majani zenye uwezo mkubwa sana kukufanya uwe mwenye afya milele na milele. Mmea huu unajulikana kitaalamu kama Brassica oleracea na unaweza kupatikana katika rangi mbalimbali, Kijani,nyekundu au damu yam zee nk. Ili uweze kujipatia viini vyote vya mboga hii tunashauri ule kama kachumbali na hata kama ukiamua kupika kidogo hakikisha unapika inakuwa karibia na mbichi hii itasaidia kutoangamiza viini lishe ndani ya mboga hii yenye faida kubwa mwilini mwako. FAIDA YA KABEJI KIAFYA 1....