Skip to main content

VYAKULA 6 BORA NA MUHIMU KWENYE MLO WAKO

Lishe ni moja ya nguzo kubwa kwenye afya ya mtu, na ndio maana unatakiwa uanze kutazama kwa jicho la karibu, kama ulikuwa unajali zaidi kazi huku ukibugia vyakula vibovu naviita junk foods, bila kutambua madhara makubwa ya kiafya yanayoletekezwa na vyakula huku ukijikuta unatumia pesa zote ulizotolea jasho kuhudhuria matibabu, basi anza kugeuka ssasa, uweze kutumia pesa kidogo kununua chakula bora na uepushe magonjwa mengi kama kisukari, saratani na magonjwa ya moyo. Unachokula si tu kinafanya mwili unawiri na kuongeza nguvu pia kinaongeza ufanisi wa mwili katika kufanya shughuli zake kama usagaji wa chakula na usafirishaji wa chakula na takamwili.  Kama ulaji wako ni mbovu unaotegemea vyakula vilivyosindikwa na fast foods, ambavyo si tu vinakosa baadhi ya virutubisho muhimu bali pia vinakuja na sumu nyingi zikiwemo vionjo viongeza utamu (artificial sweeters) zitakazorudisha nyuma afya ya mwili wako. Kinyume kabisa na vyakula asili ambavyo vitakupa vitamin za kutosha, madini, kukufanya ujiskie una nguvu mda wote kwa kukulinda dhidi ya magonjwa na hivo kufanya maisha yako kuwa ya furaha siku zote.
1. NYANYA
Nyanya ni zao ambalo linapatikana kila sehemu ndani ya nchi yetu. Kabla ya kutumia nyanya yako hakikisha imelimwa katika udongo salama ambao haujachafuliwa sana  na mbolea za kisasa, pia nyaya yako inatakiwa iwe na asilimia ndogo ama hakuna ya dawa za vijiua vidudu, na pia iwe ni nyanya ambayo haijabadilishwa genetiki zake ( nitakwambia madhara ya mkono wa mtu ikiwemo ubadilishaji wa genetiki za mimea hapo mbele.
Nini kinaifanya nyanya kuwa chakula bora.
Nyanya zina kemikali zinazoitwa flavonoids (anticarcinogenic) ambazo hupambana na visababisha saratani. Moja ya kemikali hiyo inaitwa lycopene ambayo hulipa tunda kama nyanya, tikiti ile rangi yake nyekundu. Lycopene ina nguvu kubwa katika kupambana na kuzuia saratani, hasa saratani ya tezi dume ( prostate cancer). Nyanya pia huchangia aslimia 38 ya vitamin C , 30% ya vitamin A na 18% ya vitamin K kwa matumizi ya kila siku. Kumbuka ili upoate lycopene ya kutosha kwenye nyanya unahitaji kuzikaanga kidogo kwenye mafuta kisha ukala pamoja na mchanganyiko wako wa vyakula vingine ulivyoandaa.
2. BROCCOLI
Ni moja ya chakula kinachopatikana kwa wingi pia kwenye masoko ya vyakula. Historia inasema kuwa Broccoli ni mboga ambayo ilitumiwa sana za waroma hapo zamani.matumizi yake makubwa yalianza karne ya 16, wafaransa na waingereza walianza kutumia mboga hii mnamo miaka ya 1700 na hulo marekani mboga hii ilianza kutumiwa na kuuzwa kibiashara mwaka 1920. Mboga unaweza kuandaa kwa namna nyingi ikiwemo, kurosti, kula ikiwa mbichi, ni vizuri zaidi kutokana na kwamba upikaji unaharibu baadhi ya virutubisho.
Nini kinafanya broccoli kuwa chakula bora ambacho hutakiwi kukikosa.
Broccoli ina kiasi cha vitamin C mara mbili zaidi ya chungwa, madini mengi ya calcium kama maziwa na pia sifa ya kupigana na magonjwa kama saratani, kupambana na virusi, kutokana na wingi wa madini ya selenium. Kikombe kimoja cha mtori wa broccoli kitakupa mahitaji yako ya siku nzima ya Vitamin C na Vitamini K na pia ni chanzo kizuri cha Vitamin A na Potasium. Baadhi yua faida zingine zinazofahamika za broccoli ni hizi
1. kupambana na saratani ama cancer
2. kupambana na mashambulizi ya magonjwa
3. kusaidia usagaji wa chakula na kuondoa sumu mwilini
4.Ulinzi dhidi ya ,magonjwa mbalimbali hatari kama magonjwa ya moyo
5.afya nzuri ya mifupa na meno

3. TANGO
Ni moja ya tunda na  mboga inayozalishwa kwa wingi zaidi duniani. Chanzo chake ni katika ukanda wa bahari ya mediterania. Kuweza kutumia tango unaweza kukata kata na ukachanganya kwenye kachumbari yako, ama unaweza kutengeneza jiuisi kwa kutumia blender yako ukiwa nyumbani.
Ni nini kinafanya Tango kuwa ni moja ya chakula bora
Hapo zamani za mababu zetu Tango lilitumika kama njia ama dawa ya asili kwa ajili ya kutibu maumivu ya kichwa, juisi ya tango husaidia kusafisha ngozi, na kuondoa uchovu kwenye macho. Maajabu haya ya tango yaliwafanya wanasayansi kuanza kutafiti juu ya tunda hili, zikiwemo mbegu zake, Asilimia 90 ya Tango ni maji ambapo zifuatazo ni virutubisho vinavyopatikana:-
1.Vitamini K kwa ajili ya kuzuia maambukizi
2. Vitamin C kwa ajili ya kupambana na maambukizi
3. Vitamini B% ambayo huzalisha nguvu kwenye mwili
4. Madini ya manganese kwa ajili ya kuimarisha mifupa
5.madini ya potassium na magnesium kwa ajili ya afya ya Moyo
Tafiti za hivi karibuni zinasema kuwa tunda la Tango kemikali inayoitwa lignans ambayo hupatikana pia kwenye kabeji na vitunguu ambayo kazi ya lignans ni kupunguza hatari ya kuugua magonjwa ya moyo, pia muungano wa lignin na bacteria wazuri walioko kwenye mfumo wa usagaji chakula husaidia kupunguza hatari ya kuugua badhi ya saratani kama saratani ya matiti, kizazi, na saratani ya tezi dume
   4. PARACHICHI
Ni nini kinafanya Parachichi kuwa ni moja ya chakula bora
Parachichi ukilinganisha na matunda mengine ni tunda ambalo lina virutubisho vingi zaidi na hutakiwi kulikosa kwenye mlo wako kila siku, tunda moja la parachichi lina virytubisho vifuatavyo:-
1. Vitamini K ambayo inaweza kuchangia 36% ya mahitaji yako
2. 30% ya mahitaji yako ya siku ya vitamin B
Muhimu zaidi ni kwamba parachichi ni moja ya matunda machache ambayo yana kiasi kikubwa cha mafuta mazuri (god fats) ambayo na hivyo itakusaidia kuweka mafuta yako ya mwili  kwenye msawazo na hivyo kupunguza hatari ya kuugua magonjwa ya Moyo na uzito mkubwa.

5. NAZI
Mafuta ya nazi ambayo hutengenezwa kutoka kwenye nazi iliyokomaa hutumika zaidi katika nchi za wenzetu kama India, Sri lanka, Thailand na Ufilipino ambako mmea huu hulimwa kwa wingi zaidi, hapa nchini pia mmea huu hulimwa sana mikoa ya pwani kama Tanga, Pwani, Dar es salaam na Mtwara.
Mafuta ya kula ya nazi yanaweza kutumika katika mapishi ya vyakula, kuchanganywa kwenye saladi ayko, ama unaweza kutumia kutengenezea juisi.
Ni nini kinafanya Nazi kuwa ni moja ya chakula bora,
Kwa wale ambao wanapunguza uzito basi badala ya kutumia wanga na sukari, anza kutumia Nazi kama chanzo cha mafuta mazuri (medium chain fats) ambazo huweza kuvunjwa vunjwa kirahisi  ndani ya mwili  na hivo kuweza kubadilishwa na ini kuwa nguvu moja kwa moja pasipo kuhifadhiwa kama mafuta kama ilivyo ukila wanga na sukari. Nazi ina uwezo mkubwa wa kupambana na bacteria, virusi na protozoa. Matumizi ya nazi pia yatakusaidia
1. Kuimarisha afya ya moyo
2. kusapoti ufanyaji kazi wa tezi ya thairodi
3. kuimarisha utendaji kazi wa ubongo
4. kuimarisha kinga ya mwili
5. Nazi ni chanzo kizuri cha petrol ya mwili ili kutoa nguvu
6. Kusaidia muimarisha utendaji kazi wa mwili katika kukuwezesha kupunguza uzito.




Comments

Popular posts from this blog

KUTOKWA NA UCHAFU UKENI, CHANZO NA TIBA YAKE

Uke wa mwanamke hufanya kazi ya kutoa njia kati ya sehemu ya nje ya mwili na viungo vya uzazi vya ndani vya mwanamke. Hali ya kawaida ya majimaji yaliyomo katika uke wa mwanamke huwa ni ya tindikali ili kuzuia maambukizi ya vijidudu wa kuleta maradhi. Hali hii ya utindikali huletwa na bacteria waishio katika uke wa mwanamke. Bacteria hawa ni wa kawaida na hawana madhara kwa mwili. Uke ulio katika hali nzuri hutoa majimaji haya ili kujisafisha. Majimaji haya yanayotengenezwa katika uke na kwenye eno la cervix hufanya kazi ya kuondoa seli zilizokufa na bacteria waharibifu nje ya mwili na huu ndio uchafu wa kawaida ambao mwanamke hutoa ukeni. Kutoa uchafu huu sehemu za siri ni njia ya kuusafisha uke na kuzuia maambukizi ya magonjwa. Kitu cho chote ambacho kitaharibu uwiano wa utengeneaji wa majimaji haya ndani ya uke kinaweza kujenga mazingira ya maambukizi katika uke. Uchafu Wa Sehemu Za Siri  Wa Kawaida Wanawake wote hutoa uchafu sehemu za siri. Kiwango cha uchafu unaotoka, ra

JINSI YA KUONGEZA UFANISI WA VICHOCHEO VYA KIUME (TESTOSTERONE) NA KUKINGA DHIDI YA MATATIZO YATOKANAYO NA KUKUA KWA TEZI DUME KWA KUTUMIA VYAKULA HIVI VI 5

Maelezo ya utangulizi. Kichocheo cha testosterone, japo huusishwa zaidi na upande wa mwananume ni muhimu kwa afya ya pande zote mbili yaani mwanamke na mwanamme pia.kadiri umri unavoenda mbele basi kiwango cha uzalishaji wa kichocheo cha testerone kupungua, kupungua kwa kichocheo hiki kunaambatana na ukuaji wa tezi dume (prostate gland),kupotea kwa nywele na pia saratani mfano saratani ya tezi dume. .KAZI KUBWA YA KICHOCHEO HIKI NI KUONGEZA MSUKUMO NA HAMU YA TENDO LA NDOA , KUIMARISHA MISULI NA MIFUPA MWILINI. NINI KINAHITAJIKA ILI KUZALISHA KICHOCHEO CHA TESTOSTERONE? Ili kuhakikisha uzalishaji wa kichocheo cha kiume unafanyika, mwili unahitaji virutubisho au viini lishe mbalimbali, baadhi ya viini lishe hivyo ni madini ya ZINC na vitamin D3,  vitamini D inaweza kuzalishwa na mwili pale ngozi yako inapokutana na mwanga wa jua, hapa nazungumzia mwanga wa asubuhi wakati jua ndo linachomoza na pia lile jua la jion karibia na kuzama, hivyo utakubaliana na mimi kuwa wengi wet

MADHARA YA PUNYETO NA TIBA YAKE

MAELEZO  YA AWALI KUHUSU TATIZO LA UPIGAJI PUNYETO Watu wengi sana wanataka kufahamu jinsi gani wafanye ili kuachana na kitendo cha upigaji punyeto. Punyeto ni tendo la mtu la kuamsha hisia za mapenzi au msisimko ambao unampelekea mtu huyu kufikia kilele cha kujimalizia tamaa zake! Bila kufanya tendo halisi, hutumia fikra zake katika picha za zinazoitwa za ngono au picha zozote zinazoweza kulifanikisha tendo hilo, movie n.k. Kilele cha yote anafikia mahali anajimalzia tamaa zake mwenyewe!. Nimekuwa nikiona baadhi ya watu wanaosema wameelimika wakipingana wao kwa wao katika suala zima la kupiga punyeto! Wako wanaotetea kutokana na elimu yao na wanasema kwa ujasiri mkubwa kwamba "kupiga punyeto ni sehemu ya maisha ya mwanadamu" Ina maana katika maisha ya mwanadamu upigaji punyeto inaelezwa ni kama tendo la lazima mpaka inafikia mahali wanasema ni sehemu ya maisha (Maisha) ya mwanadamu. Nimekuwa nikipata kesi nyingi sana juu ya madhara yatokanayo na punyeto. Aslimia 60