Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2017

MIKAKATI 7 YA KIAFYA UNAYOTAKIWA KUTEKELEZA 2017

Heri ya mwaka mpya 2017. Je umeshaweka mipango yako ya mwaka huu?? Watu wengi wameshafanya hivo lakini pia asilimia kubwa wanawahi kukata tamaa na kupunguza juhudi kuelekea kutimiza malengo yao  ifikapo mwezi wa 2 ama wa 3. Nashauri mwaka huu jikite katika kulinda fya yako kwa kubadili mtindo mbovu wa maisha na baadhi ya tabia hatarishi. Kubadili mtindo wa maisha ni suala endelevu na siyo kitu cha kutimiza siku moja au week chache . MIKAKATI 7 YA KIAFYA UNAYOTAKIWA KUTEKELEZA 2017 1.        ACHA KUNYWA SODA NA VINJWAJI VILIVOSINDIKWA Hii ni kwa sababu soda ina uhusiano na matatizo kama uzito mkubwa, magonjwa ya moyo, magonjwa ini,  na pia matatizo yamifupa, kama bado unatumia soda mara kwa mara basi badilisha kwa kutumia maji, kahawa na juisi ambayo umetengeneza mwenyewe nyumbani. 2.        KULA PARACHICHI KILA SIKU Parachichi ni tunda linalopatikana kirahisi na ni chanzo cha  mafuta mazuri ambayo ...