Skip to main content

MIKAKATI 7 YA KIAFYA UNAYOTAKIWA KUTEKELEZA 2017

Heri ya mwaka mpya 2017. Je umeshaweka mipango yako ya mwaka huu?? Watu wengi wameshafanya hivo lakini pia asilimia kubwa wanawahi kukata tamaa na kupunguza juhudi kuelekea kutimiza malengo yao  ifikapo mwezi wa 2 ama wa 3. Nashauri mwaka huu jikite katika kulinda fya yako kwa kubadili mtindo mbovu wa maisha na baadhi ya tabia hatarishi. Kubadili mtindo wa maisha ni suala endelevu na siyo kitu cha kutimiza siku moja au week chache .
MIKAKATI 7 YA KIAFYA UNAYOTAKIWA KUTEKELEZA 2017

1.       ACHA KUNYWA SODA NA VINJWAJI VILIVOSINDIKWA
Hii ni kwa sababu soda ina uhusiano na matatizo kama uzito mkubwa, magonjwa ya moyo, magonjwa ini,  na pia matatizo yamifupa, kama bado unatumia soda mara kwa mara basi badilisha kwa kutumia maji, kahawa na juisi ambayo umetengeneza mwenyewe nyumbani.
2.       KULA PARACHICHI KILA SIKU
Parachichi ni tunda linalopatikana kirahisi na ni chanzo cha  mafuta mazuri ambayo mwili huweza kuunguza kiurahisi ili kutoa nishati, tafiti zinasema kwamba unapoweka parachichi kwenye saladi yako basi unaongeza uvyonzaji wa  viondoa sumu ambavyo hulinda mwili dhidi sumu. Pia tafiti zinasema kwamba parachichi husaidia kulinda ini na kuzuia kansa ya mdomo.
3.       FANYA MAZOEZI YA KUTOSHA
Tafiti zinasema kwamba kukaa kwa mda mref ni sabab moja pekee inayoongeza hatari ya vifo na magonjwa, hatar ya kuugua kwa watu wasiofanya mazoezi ni sawa na hatar ya watu wanaovuta sigara. Unatakiwa kufahamu ni kwamba miili yetu iliubwa kushugulika na siyo kukaa seem moja bila movement. Weka lengo la kutembea walu hatua 7000 mpaka 10000 ambazo ni sawa na kilomita 6 mpaka 9.
4.       Kula zaidi samaki na mboga za majani
Protini ni virutubisho muhimu kwenye mwili kama sehemu ya afya na kiungo cha cell, misuli mifufa na viini vya kusaga chakula (enyzmes), lakini angalizo ulaji mwingi wa protini ni hatari kwa afya, hivo badala ya kula nyama zaidi basi kula samaki kwa wingi.
5.       Kufunga kula kwa masaa kadhaa
Moja ya mkakati ambao sio tu unaondoa kitambi na uzito mkubwa bali pia kuepusha magonjwa mengine hatari  kama kisukari matatizo ya moyo, ulaji wa kila mara ni chanzo cha matatizo haya yote na pia huufanya mwili kuana kuunguza sukari kamachanzo cha nishati badala ya mafuta kitendo ambacho hupunguza viini vinavyounguza mafuat. Tafiti zinasema kwamba mwili hujisafisha wenyewe na kujijenga vizuri  pale tumbo likiwa tupu bila chakula. Kufunga kula kunajumuisha kukaaa jumla ya masaa 13 mpaka 18 bila kula kwa siku hii unaweza kutimiza tu kwa kuvusha either chakula cha mchana ama asubuhi, na kula milo miwili tu, hivo kama utachagua kula usiku basi hakikisha unakula masaa ma3 kabla ya kulala, unapolala mwili uhuhitaji nishati kidogo na hivo unapokula chakula kingi basi mwili unazalisha sumu nyingi  kutokana na chakula kutosagw vizuri.
6.       LALA  MASAA 8 KILAUSIKU
Kutopata usngizi wa kutosha huleta madhara katika kinga ya mwili na pia kuongeza msongo wa mawazo na hatari ya kuugua maradhi. Ukosefu wa usingizi hupunguza homoni ya melatonin ambayo husaidia kukukinga dhidi ya saratani .
7.       KULA ZAIDI VYAKULA VYENYE NYUZINYUZI
Chakula chenye nyuzinyuzi kwa wingi hupunguza hatari ya vifo vya mapema kutoka kwenye ugonjwa wowte, kwa sababu husaidia kupunguza hatari ya baadhi ya magonjwa kama kisukari, magonjwa ya moyo,  na saratani. Zingatia chanzo kikubwa cha nyuzinyuzi kitoke kwenye mboga mboga, jamii za karanga na mbegu, na siyo nafaka


Comments

Popular posts from this blog

Kisonono ni nini ?, je kuna Tiba ya kisonono ?

Nini maana ya kisonono, je naweza kupata tiba sahihi ya kisonono?  Soma makala jii upate kujifunza na kupata ueewa juu ya tatizo la kisonono ambalo limeathiri watu wengi sana kwa sasa hasa vijana wa kiume. Kisonono au kwa lugha ya kitaalamu Gonorrhea ni moja ya ugonjwa wa ngono ambao huambukizwa baada ya mtu mmoja mwenye ugonjwa kukutana kimwili mtu mwingine mzima. Kisonono mara nyingi husababisha maumivu makali na dalili zingine mbaya kwenye via vya uzazi na sehemu zingine kama, sehemu ya haja kubwa, macho na pia maumivu ya viungo. Ugonjwa huu wa kisonono huweza kuwapata watu wa jinsia zote wanawake kwa wanaume huku tafiti zikionesha kwamba wanaume ndio wanaoongoza kuambukizwa kuliko wanawake. Nnini husababisha kinonono au Gonorrhea?? Ugonjwa huu wakuambukizwa kwa njia ya ngono husababishwa na bacteria wanaoitwa Neisseria gonorrhoeae. Na hivo pale watu wanapokutana kingono bacteria hawa huweza kusambaa kwenda kwa mtu mwingine kutokana na msuguano wa viungo laini vya uza...

JINSI YA KUGUNDUA NA KUTHIBITI VIDONDA VYA TUMBO( PEPTIC ULCER)

MAELEZO YA UTANGULIZI KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO Tunashukuru kwa kuendelea kufatilia makala zetu, kwa maoni na ushauri ama uhitaji wa kufika ofisini basi endelea kutuandikia kwa namba  0714206306 .  Kupata ufahamu mpana juu ya vidonda vya tumbo ni vema kuelewa kwanza mfumo unaohusika na tumbo ambao ni umen'genyaji wa chakula. Sehemu kuu zinazohusika katika umen'genyaji huo ni kinywa,umio ambayo ni misuli wenye urefu wa sentimeta 23 ambao huunganisha koromeo na tumbo'esophagus',mfuko wa nyongo na sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo'duodenum',utumbo mdogo,kongosho,utumbo mpana na sehemu ya mwish oni ya utumbo'rectum'. Mfumo wa mmen'genyo wa chakula hasa kuta za umio,tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na tindikali inayotumika kumen'genya chakula inaposhambulia kuta hizo, hii ndiyo vidonda vya tumbo'Peptic Ulcers',vidonda vya mfumo wa umen'genyaji chakula vikiwa kwenye tumbo ni 'Gastric Ulcer'vikiwa kati...

UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE

 FAHAMU TATIZO LA UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE (OVARIAN CYST ) Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovary) hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana kama ovarian cyst. Uvimbe huu unaweza kumtokea mwanamke wa umri wowote ingawa mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito. MAYAI YA MWANAMKE  Kwa kawaida mwanamke anakuwa na mayai mawili katika mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto. Mayai haya hupatikana pembezoni mwa mfuko wa uzazi (uterus). Mayai haya huanza kuzalisha mayai ya uzazi yanayojulikana kama ovum  ambapo mayai hayo ya uzazi hukuwa ndani ya mayai ya mwanamke (ovary) kwa kuchochewa na baadhi ya homoni.  Katikati ya mwezi, siku ya kumi na nne, saa 24-36 baada ya kiwango cha kichocheo aina ya Luteinizing Hormone kuwa juu, mayai ya uzazi hutolewa k...