FAHAMU TATIZO LA UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE (OVARIAN CYST ) Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovary) hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana kama ovarian cyst. Uvimbe huu unaweza kumtokea mwanamke wa umri wowote ingawa mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito. MAYAI YA MWANAMKE Kwa kawaida mwanamke anakuwa na mayai mawili katika mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto. Mayai haya hupatikana pembezoni mwa mfuko wa uzazi (uterus). Mayai haya huanza kuzalisha mayai ya uzazi yanayojulikana kama ovum ambapo mayai hayo ya uzazi hukuwa ndani ya mayai ya mwanamke (ovary) kwa kuchochewa na baadhi ya homoni. Katikati ya mwezi, siku ya kumi na nne, saa 24-36 baada ya kiwango cha kichocheo aina ya Luteinizing Hormone kuwa juu, mayai ya uzazi hutolewa k...
Blog hii inakupa maelezo juu magonjwa tabia(lifestyle disease) ama magonjwa ya lishe , visababishi vyake na namna ya kuepuka magonjwa haya kwa kutumia vyakula na virutubisho asili Pia utapata ushauri na tiba juu ya magonjwa ambayo yamekusumbua kwa mda mrefu. Baadhi ya magonjwa yanayotibika na dawa zetu za mimea ni Kisukari, Vidonda vya tumbo, Upungufu wa nguvu za kiume, uvimbe, ugumba na magonjwa mengine ya wanawake