Skip to main content

UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE

 FAHAMU TATIZO LA UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE (OVARIAN CYST )



Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovary) hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana kama ovarian cyst.
Uvimbe huu unaweza kumtokea mwanamke wa umri wowote ingawa mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito.

MAYAI YA MWANAMKE

 Kwa kawaida mwanamke anakuwa na mayai mawili katika mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto. Mayai haya hupatikana pembezoni mwa mfuko wa uzazi (uterus).
Mayai haya huanza kuzalisha mayai ya uzazi yanayojulikana kama ovum  ambapo mayai hayo ya uzazi hukuwa ndani ya mayai ya mwanamke (ovary) kwa kuchochewa na baadhi ya homoni.
 Katikati ya mwezi, siku ya kumi na nne, saa 24-36 baada ya kiwango cha kichocheo aina ya Luteinizing Hormone kuwa juu, mayai ya uzazi hutolewa katika kila ovari na hii ndio hujulikana kama ovulation au upevukaji mayai. Mayai haya ya uzazi huishi kwa saa chache hadi saa 24 ikiwa hayatorutubishwa na mbegu za kiume.
 Mabaki ya mfuko wa mayai ya uzazi yanayojulikana kama follicle ndani ya ovari, hugeuka na kuwa corpus luteum ambao huhusika na utoaji wa kichocheo au homoni aina ya progesterone kwa wingi.
Homoni hii ya progesterone ndio inayosababisha mfuko wa uzazi kujiandaa kwa kujikita yai (implantation) lililorutubishwa kwa mbegu ya kiume ndani ya mfuko wa uzazi kwa kuongeza unene kwenye kuta zake. Yai hili husafiri hadi kwenye mfuko wa uzazi ambako hukua na kuwa mtoto. Kama upachikwaji wa yai liliorutubishwa hautafanyika, basi ndani ya wiki mbili, corpus luteum huanza kusinyaa na kupotea na kusababisha kushuka kwa kiwango cha homoni aina ya progesterone na estrogen.
 Kushuka kwa kiwango cha vichocheo hivi ndio husababisha mfuko wa uzazi kuanza kutoa mabaki ya kuta zake pamoja na yai la uzazi na ndipo pale mwanamke anapoanza kuona siku zake za hedhi(kutokwa na damu ukeni).


UVIMBE KWENYE MAYAI.

 Kuna aina nyingi za uvimbe kwenye mayai ya mwanamke ila  aina hizi saba ndio huonekana sana kwa wanawake wengi.

1~ Aina ya kwanza ni Follicular cyst ambayo uvimbe hutokea wakati ovulation isipotokea au baada ya corpus luteum kuanza kusinyaa na kupotea yenyewe baada ya kutopachikwa kwa yai kwenye kuta za mfuko wa kizazi.
Uvimbe huu unakuwa na wastani wa inchi 2.3 kwa upana. Upasukaji wa uvimbe huu husababisha maumivu makali sana katikati ya mzunguko wa hedhi yaani siku ya ovulation.
Kwa kawaida uvimbe huu hauna dalili zozote na hupotea wenyewe baada ya miezi kadhaa.

2~Aina ya pili ni Corpus Luteum cyst- ambao ni uvimbe unaosababishwa na kutopachikwa kwa yai la uzazi lililorutubishwa na mbegu ya kiume kwenye mfuko wa kizazi. Kwa kawaida corpus luteum husinyaa na kupotea yenyewe, au wakati mwengine inaweza ikajaa maji na hivyo kusababisha uvimbe.
Uvimbe huu huonekana kwenye upande mmoja (kushoto au kulia) wa mwanamke na hauna dalili zozote zile.

3~Uvimbe wa tatu ni  Hemorrhagic cyst- Uvimbe huu hutokea wakati kukiwa na uvujaji wa damu ndani ya uvimbe wa aina yoyote ule ambao umeshajitengeneza tayari. Huambatana na maumivu makali kwenye upande mmoja wa ubavu wa mwanamke.

4~Uvimbe mwingine ni Dermoid cyst- ambao sio saratani na pia hujulikana kama mature cystic teratoma, huathiri wanawake wadogo walio katika umri wa kushika mimba na huweza kukua na kufikia inchi 6 kwa upana na ndani huweza kuwa na mchanganyiko wa nywele, mfupa, mafuta na cartilage.
 Uvimbe wa aina hii huweza kuwa mkubwa zaidi au kujizungusha na hivyo kuathiri usambazaji wa damu kwenda kwenye uvimbe huu na hivyo kusababisha maumivu makali sana maeneo ya tumboni.

5~Aina ya 5ni Polycysitic appearing cyst- ambao unakuwa mkubwa sana na huwa umezungukwa na vijivimbe vingine vidogo vidogo na huonekana hata kwa wanawake wenye afya njema au wale wenye matatizo ya homoni.

6~Aina ya sita ya uvimbe ni Cystedenoma-Ni aina ya uvimbe unaotokana kwenye tishu za ovari na hujazwa na majimaji yenye kuvutika. Uvimbe wa aina hii huweza kuwa mkubwa sana hata kufikia inchi 12 au zaidi kwa upana.
7~Aina ya mwisho ya uvimbe unaowapata wanawake ni Endometriomas /Endometrial.

SABABU ZA UVIMBE.

 Vihatarishi vya tatizo la uvimbe kwenye mayai ya mwanamke nipamoja na
historia ya awali ya ovarian cyst. Kwa wanawake ambao wazazi wao au watu wao wa karibu wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huo kuna uwezekano mkubwa nao wakapatwa na tatizo hilo.
Sababu nyingine inayoweza kusababisha uvimbe katika mayai ya mwanamke ni kuwa na mzunguko wa hedhi usiokuwa na mpangilio maalum. Kihatarishi kingine ni kuwa na mafuta mengi kwenye sehemu ya juu ya mwili na hii ni kwa wale wanawake wanene.
Ugumba na kuvunja ungo mapema ni sababu nyingine ambapo mtoto wa kike hasa anayevunja ungo  akiwa na miaka 11 au chini ya hapo huweza kupatwa na uvimbe katika mayai yake.

DALILI ZA OVARIAN CYST

 Maumivu makali, ambayo hayana mwanzo maalum na yanayochoma, ambapo maumivu hayo yanaweza yakawa yanakuja na kupotea au yakawepo moja kwa moja.
Kuhisi tumbo kuwa zito, kujaa au kuvimba, maumivu kwenye matiti na hedhi isiyokuwa na mpangilio maalum, maumivu ya muda mrefu kwenye nyonga wakati wa hedhi na ambayo huweza kuhisiwa sehemu ya chini mgongoni. Maumivu haya yanaweza kuanza muda mfupi tu baada ya kuanza hedhi, wakati wa hedhi au mwisho wa hedhi.
Maumivu ya nyonga baada ya kufanya kazi ngumu, mazoezi au baada ya kukutana kimwili, kuhisi kichefuchefu, kutapika na kutokwa na matone ya damu ukeni. Dalili nyingine ni ugumba na kuhisi uchovu, mabadiliko ya haja ndogo yaani kukojoa mara kwa mara, kujikojolea au kushindwa kutoa mkojo wote kutoka kwenye kibofu cha mkojo wakati wa kupata haja ndogo.


VIPIMO

Mgonjwa kufanyiwa Endovaginal Ultrasound ambayo hufanywa kwa kuingiza mpira maalum kupitia ukeni na kuangalia mfuko wa uzazi na mayai ya mwanamke. Kwa kutumia kipimo hiki, ni rahisi kwa daktari kugundua kama uvimbe kwenye mayai ni wa aina gani na kujua kama ni maji tu (fluid filled sac), au ni maji pamoja na mchanganyiko wa vitu vigumu kwa maana ya complex, au ni vitu vigumu pekee ambapo huitwa completely solid.

Matibabu ya Ovarian Cyst

1.Wanawake wengi wanafibroids ndogo ndogo lakini kwa sababu hazina dalili hahawezi kwenda hospitali na hawa ndo siku wakibeba ujauzito uvimbe unaongexeka sababu ya vichocheo kuongezeka hvyo hawa watu wabainika wanapofanyiwa ultrasound ndipo wanakutwa navyo.lkn kitalamu hospitali hawatibu uvimbe wa namna hii.

.>>Uvimbe ambao ni mkubwa wenyewe hutibiwa kwa namna zifuatazo (hospital)

~.Dawa ambazo ni gharama sana mfano donazol wengi masikini hawawez kumudu kununua

~.Vidonge vya maumivu

~.Vidonge vya kuzuia damu kama tranexamic acid na dawa za uzazi wa mpango(COCs)

2.Njia ya pili ni operation nazo zipo operation aina nyingi inategemea na uvimbe ukubwa na wingi wake.

~.Myomectomy hii ni operation ya kuondoa uvimbe mmoja mmoja bila kuondoa kizazi kwa wale wenye uvimbe mmoja uko sehemu nzuri

~.Total abdominal hysterectomy. Hii operation unaondoa kizazi chote kama uvimbe umekaa vibaya na viko vingi.
Swali la kujiuliza kwa nini mpaka upate dalili ndo utaanza kushughulikiwa kutibiwa???? Kwa nini ubebe ujauzito huku una uvimbe kisa bado mdogo???

Kumbuka uvimbe huu sio kansa hivyo ondoa hofu. Mbali na donazole ambayo ni ya gharama na haishauliwi itumiwe kwa mda mrefu ina sababisha mwanamke anakua na sifa za kiume.UKIFANYIWA OPERATION USIDHANI UVIMBE UMEISHA UNAOTA PEMBENI HADI UTAKAPOWEKA VICHOCHEO SAWA.
 Sasa suluhisho lako lipo tuna dawa ambao imetengenezwa kitalamu katika mfumo wa vidonge na vimetengenezwa kwa mimea baada ya utafiti na majaribio ya kutosha na viwanda vya madawa vikubwa hapa duniani.
Utapata suluhisho lako bila madhara kwani ni mimea 100%.
Hii dawa inapunguza uvimbe wa fibroid bila madhara kama donazol. Kama una ndugu au rafiki mwambie suluhisho lipo na mshirikishe kuokoa afya yake.



 Kwa wale akina mama wenye matatizo ya homoni, kuvurugika kwa hedhi na kukosa ujauzito kwa mda mrefu basi tumewaandalia programme ya week 3 ambayo itakusaidia kubalansi homoni zako na kurejesha uwezo wa kushika ujauzito. Tunashauri wanandoa wote kufanya vipimo ili kujua chanzo cha tatizo lako la kushindwa kushika ujauzito. karibu nawe upate huduma hii ya virutubisho na dawa zetu za asili ili uwe mmoja wa mashuhuda na mwenye furaha kama baadhi ya hawa wagonjwa tuliokwisha kuwapa huduma.

UTAFITI UNASEMAJE KUHUSU TIBA NA VIRUTUBISHO VYA KUSAWAZISHA HOMONI ZA KIKE.
1. Zinc capsules
Kwa wanawake, MADINI YA ZINC yanahusika katika ukuuaji wa yai (oocyte). Kama mwanamke atakuwa na upungufu wa zinc, yai halitakomaa vizuri na utolewaji wa yai (ovulation) utazuiliwa , na kusababisha ugumba. Kiwango cha zinc cha kutosha kunamwezesha mwanamke kutumia estrogen na progesterone vizuri. hakikisha unapata virutubisho kutoka kwenye vyanzo vilivyothibitishwa.
2. Soy capsules
vidonge hivi vilivyotengenezwa kiasili kwa kutumia viambata vya mimea ya Semen Glycine, Radiz Paeoniae Alba Eztractum na Ganoderma husaidia: kuongeza ufanyaji kazi wa mfuko wa mayai (ovaries), kuzuia Saratani ya matiti, kuimarisha afya ya mifupa kwa wanawake waliokoma hedhi.(menopause). 



     Naamini nawe unatamani kufikia malengo haya na umehangaika hospitali nyingi bila msaada, basi anza kurejesha tumaini lako. unaweza kutupigia namba 0762336530. upate maelekezo ya dawa kwa gharama nafuu na namna ya kufika ofsini.
      unaweza kuwa wewe ni mzima hivo mfahamishe na mwingine kuhusu huduma hii. karibu.
VIRUTUBISHO VYOTE HIVI VINAPATIKANA OFSINI KWETU MWEMBECHAI,  DAR ES SALAAM KWA GHARAMA YA SH 90,000/= kwa jumla. hivo huhitaji kuagiza nje ya nchi, tayari tumefanyia vipimo na vimethibitishwa kutibu matatizo ya ugumba na homoni.

Comments

Popular posts from this blog

MADHARA YA PUNYETO NA TIBA YAKE

MAELEZO  YA AWALI KUHUSU TATIZO LA UPIGAJI PUNYETO Watu wengi sana wanataka kufahamu jinsi gani wafanye ili kuachana na kitendo cha upigaji punyeto. Punyeto ni tendo la mtu la kuamsha hisia za mapenzi au msisimko ambao unampelekea mtu huyu kufikia kilele cha kujimalizia tamaa zake! Bila kufanya tendo halisi, hutumia fikra zake katika picha za zinazoitwa za ngono au picha zozote zinazoweza kulifanikisha tendo hilo, movie n.k. Kilele cha yote anafikia mahali anajimalzia tamaa zake mwenyewe!. Nimekuwa nikiona baadhi ya watu wanaosema wameelimika wakipingana wao kwa wao katika suala zima la kupiga punyeto! Wako wanaotetea kutokana na elimu yao na wanasema kwa ujasiri mkubwa kwamba "kupiga punyeto ni sehemu ya maisha ya mwanadamu" Ina maana katika maisha ya mwanadamu upigaji punyeto inaelezwa ni kama tendo la lazima mpaka inafikia mahali wanasema ni sehemu ya maisha (Maisha) ya mwanadamu. Nimekuwa nikipata kesi nyingi sana juu ya madhara yatokanayo na punyeto. Aslimia 60...

Kisonono ni nini ?, je kuna Tiba ya kisonono ?

Nini maana ya kisonono, je naweza kupata tiba sahihi ya kisonono?  Soma makala jii upate kujifunza na kupata ueewa juu ya tatizo la kisonono ambalo limeathiri watu wengi sana kwa sasa hasa vijana wa kiume. Kisonono au kwa lugha ya kitaalamu Gonorrhea ni moja ya ugonjwa wa ngono ambao huambukizwa baada ya mtu mmoja mwenye ugonjwa kukutana kimwili mtu mwingine mzima. Kisonono mara nyingi husababisha maumivu makali na dalili zingine mbaya kwenye via vya uzazi na sehemu zingine kama, sehemu ya haja kubwa, macho na pia maumivu ya viungo. Ugonjwa huu wa kisonono huweza kuwapata watu wa jinsia zote wanawake kwa wanaume huku tafiti zikionesha kwamba wanaume ndio wanaoongoza kuambukizwa kuliko wanawake. Nnini husababisha kinonono au Gonorrhea?? Ugonjwa huu wakuambukizwa kwa njia ya ngono husababishwa na bacteria wanaoitwa Neisseria gonorrhoeae. Na hivo pale watu wanapokutana kingono bacteria hawa huweza kusambaa kwenda kwa mtu mwingine kutokana na msuguano wa viungo laini vya uza...

JINSI YA KUGUNDUA NA KUTHIBITI VIDONDA VYA TUMBO( PEPTIC ULCER)

MAELEZO YA UTANGULIZI KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO Tunashukuru kwa kuendelea kufatilia makala zetu, kwa maoni na ushauri ama uhitaji wa kufika ofisini basi endelea kutuandikia kwa namba  0714206306 .  Kupata ufahamu mpana juu ya vidonda vya tumbo ni vema kuelewa kwanza mfumo unaohusika na tumbo ambao ni umen'genyaji wa chakula. Sehemu kuu zinazohusika katika umen'genyaji huo ni kinywa,umio ambayo ni misuli wenye urefu wa sentimeta 23 ambao huunganisha koromeo na tumbo'esophagus',mfuko wa nyongo na sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo'duodenum',utumbo mdogo,kongosho,utumbo mpana na sehemu ya mwish oni ya utumbo'rectum'. Mfumo wa mmen'genyo wa chakula hasa kuta za umio,tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na tindikali inayotumika kumen'genya chakula inaposhambulia kuta hizo, hii ndiyo vidonda vya tumbo'Peptic Ulcers',vidonda vya mfumo wa umen'genyaji chakula vikiwa kwenye tumbo ni 'Gastric Ulcer'vikiwa kati...