Skip to main content

Kisonono ni nini ?, je kuna Tiba ya kisonono ?

Nini maana ya kisonono, je naweza kupata tiba sahihi ya kisonono? 

Soma makala jii upate kujifunza na kupata ueewa juu ya tatizo la kisonono ambalo limeathiri watu wengi sana kwa sasa hasa vijana wa kiume.

Kisonono au kwa lugha ya kitaalamu Gonorrhea ni moja ya ugonjwa wa ngono ambao huambukizwa baada ya mtu mmoja mwenye ugonjwa kukutana kimwili mtu mwingine mzima. Kisonono mara nyingi husababisha maumivu makali na dalili zingine mbaya kwenye via vya uzazi na sehemu zingine kama, sehemu ya haja kubwa, macho na pia maumivu ya viungo. Ugonjwa huu wa kisonono huweza kuwapata watu wa jinsia zote wanawake kwa wanaume huku tafiti zikionesha kwamba wanaume ndio wanaoongoza kuambukizwa kuliko wanawake.


Nnini husababisha kinonono au Gonorrhea??

Ugonjwa huu wakuambukizwa kwa njia ya ngono husababishwa na bacteria wanaoitwa Neisseria gonorrhoeae. Na hivo pale watu wanapokutana kingono bacteria hawa huweza kusambaa kwenda kwa mtu mwingine kutokana na msuguano wa viungo laini vya uzazi, hapa utafahamu ya kwamba aina zote za ngono husambaza maambukizi ya kisonono aina hizi ni kama
·         Ngono ya kawaida kupitia uke (vaginal intercourse)
·         Ngono kupitia njia ya haja kubwa (anal sex)
·         Na ngono kupitia mdomo (oral sex)


Baceteria hawa wa Neisseria Gonorrhoeae huwa kuambukizwa pia kwa kugusa mahali au kiungo kilichoathirika mfano kugusa uke, uume, mdomo au sehemu ya haja kubwa ambayo tayari imeathirika na kisonono. Habari njema ni kwamba Bacteria hwa hawawezi kuishi nje ya mwili wa binadamu kwa Zaidi ya sekunde kadhaa, hivo hutaweza kupata maambukizi haya kwa kutumia vyoo vya uma au kuchangia nguo na mgonjwa wa kisonono, Lkini wanawake wenye kisonono huweza kuwaambukiza watoto wanaozaliwa wakati wa kujifungua.

 DALILI ZA KISONONO

Kwa mtu kuanza kuugua kisonono huchukua walau siku 2 mpaka 5 tangu kuambukizwa ili kuanza kuona dalili mbaya, lakini wakati mwingine yaweza kuchukua mpaka siku 30 hasa kwa wanawae kuanza kuona dalili za ugonjwa, Dalili hizi zinaonesha una kisonono na unahitaji kumwona dactari mapema


Dalili za kisonono kwa wanawake ni kama


v  Maumivu wakati wa kukojoa
v  Kuwasha kwa sehemu ya haja kubwa, na kutoa majimaji mazito kila mara
v  Kutokwa na uchafu ukeni kusiko kawaida wakati na baada ya tendo la ndoa
v  Kuvurugika kwa hedhi ama hedhi kuchukua siku nyingi Zaidi
v  Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
v  Kupata homa mara kwa mara na kujisikia mwili kuchoka sana

Dalili za kisonono kwa wanaume;  


kwa upande wa wanaume dalili hujitokeza mapema Zaidi na hivo wanakuwa wa kwanza katika kutafuta tiba na ushauri wa kiafya, maana tatizo husababisha kuumwa sana homa kali, dalili zingine ni kama
v  Kutokwa na uchafu mithili ya maziwa na njano
v  Maumivu makali wakati wa kukojoa na mkojo wa mara kwa mara
v  Kuwasha kwa sehemu za uume na haja kubwa
v  Kwa wagonjwa wachache hutokea macho kuwa mekundu.

Namna gani unaweza kujizuia kupata kisonono?

Hili ni swali ambao yawezekana kila mmoja wetu anajiuliza   jinsi gani ajikinge ii kuepuka madhara ya kisonono ambayo ni makubwa Zaidi. Njia rahisi za ya uhakika kutoapata kisonono ni kuacha kabisa kujiusisha na ngono. Najua ni vigumu kwa watu wote lakini ndio njia ya uhakika Zaidi, watu wasioshiriki ngono mara kwa mara pia wapo kwene hatari ndogo Zaidi ya kupata kisonono. Kuepuka ngono kabisa ni jambo gumu kutokana na kwamba mahusiano mengi hasa ya mke na mume yanaimarika  kwa kufanya Ngono, ngono ni kiungo muhimu katika kuimarisha mahusiano ya mke na mume. Hivo ili kupunguza hatari ya kupata kisonono hakikisha unafanya ngono salama na kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu.

 Makundi ya watu waliopo katika hatari Zaidi ya kupata kisonono ni

  • ·         Wenye umri mdogo
  • ·         Wanaofanya ngono mara kwa mara na wapenzi wapya
  • ·         Wanaofanya ngono na mtu mwenye mpenzi mwingine
  • ·         Wenye wapenzi wengi (michepuko)
  • ·         Wanaume wanaofanya ngono kinyume na maumbile na wanaume wenza
  •       Kujihusisha na ngono chini ya umri wa miaka 25
  • ·         Waliowahi kuugua kisonono kwa kipindi cha nyuma
  • ·         Wenye magonjwa mengine ya ngono kama vile Ukimwi

Unataka kuishi bila ya maambukizi ya kisonono? Fuata njia hizi salama

1.      Tumia condom kwa kila tendo la ndoa: husaidia kuzuia bacteria kupenya kwa mtu mwingine wakati wa ufanyaji wa ngono
2.      Hakikisha mpenzi wako mpya anafanyiwa vipimo kabla hamjaanza mahusiano ili kpunguza hatari ya kupata maambukizi
3.      Usifanye ngono na mpenzi wako kama anaonyesha kuwa na dalili za kisonono, mfano kupata maumivu wakati wat endo, au kutoa majimaji mazito ya kijani na njano yenye harufu, au kujitokeza kwa malengelenge kwenye uume au uke,.unapoona dalili hizi basi wewe na mpenzi wako acheni kufanya ngono kwa muda mpaka mtakapofanya vipimo na kupata tiba kwa ugonjwa huu.
4.      Fanya vipimo mara kwa mara walau mara moja kwa mwaka ili kugundua maambukizi mapema na kutibu mapema

MUHIMU KWA WAJAWAZITO WENYE KISONONO

Kama wewe ni mjamzito na umegundulika una kisonono basi wasiliana na Daktari wako ili aweze kukuanzishia tiba inayofaa ambayo haitaleta madhara kwa mtoto aliyeko tumboni. Kisonono huweza kusababisha matatizo  makubwa kwa kichanga cha tumbo hivo inashauriwa kutibu ugonjwa huu mapema iwezekanavyo ili kupunguza hatari kwa mtoto.

Kisonono kinatibika vizuri kama mgonjwa atafuata utaratibu wa tiba kwa usahihi. Kumbuka ni muhimu kucheza salama na kuepuka ngono nzembe ili kujizuia na maambukizi ya kisonono

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUGUNDUA NA KUTHIBITI VIDONDA VYA TUMBO( PEPTIC ULCER)

MAELEZO YA UTANGULIZI KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO Tunashukuru kwa kuendelea kufatilia makala zetu, kwa maoni na ushauri ama uhitaji wa kufika ofisini basi endelea kutuandikia kwa namba  0714206306 .  Kupata ufahamu mpana juu ya vidonda vya tumbo ni vema kuelewa kwanza mfumo unaohusika na tumbo ambao ni umen'genyaji wa chakula. Sehemu kuu zinazohusika katika umen'genyaji huo ni kinywa,umio ambayo ni misuli wenye urefu wa sentimeta 23 ambao huunganisha koromeo na tumbo'esophagus',mfuko wa nyongo na sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo'duodenum',utumbo mdogo,kongosho,utumbo mpana na sehemu ya mwish oni ya utumbo'rectum'. Mfumo wa mmen'genyo wa chakula hasa kuta za umio,tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na tindikali inayotumika kumen'genya chakula inaposhambulia kuta hizo, hii ndiyo vidonda vya tumbo'Peptic Ulcers',vidonda vya mfumo wa umen'genyaji chakula vikiwa kwenye tumbo ni 'Gastric Ulcer'vikiwa kati...

UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE

 FAHAMU TATIZO LA UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE (OVARIAN CYST ) Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovary) hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana kama ovarian cyst. Uvimbe huu unaweza kumtokea mwanamke wa umri wowote ingawa mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito. MAYAI YA MWANAMKE  Kwa kawaida mwanamke anakuwa na mayai mawili katika mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto. Mayai haya hupatikana pembezoni mwa mfuko wa uzazi (uterus). Mayai haya huanza kuzalisha mayai ya uzazi yanayojulikana kama ovum  ambapo mayai hayo ya uzazi hukuwa ndani ya mayai ya mwanamke (ovary) kwa kuchochewa na baadhi ya homoni.  Katikati ya mwezi, siku ya kumi na nne, saa 24-36 baada ya kiwango cha kichocheo aina ya Luteinizing Hormone kuwa juu, mayai ya uzazi hutolewa k...