Skip to main content

MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO AU URINARY TRACT INFECTION (U.T.I)



Njia ya mkojo ni eneo linalojumuisha eneo la nje la utupu hadi katika kibofu cha mkojo mpaka katika figo.

U.T.I ni  maambukizi katika njia ya mkojo yanayosababishwa na bacteria waitwao Escherichia coli ( E.coli)  mara nyingi bacteria hawa hupatikana katika utumbo mpana au katika haja kubwa (Gastro intestinal tract GI) na bacteria wengine kama staphylococcus,saprophyticus, enterobacter n.k wakifanikiwa kuingia, kusambaa, kuushambulia na kuuathiri mfumo wa mkojo. Pia U.T.I huweza kusababishwa na magonjwa ya zinaa kama herpes,gonorrhea,chlamydia n.k

Kutokana na kuwa urethra ya wanawake (njia ya mkojo) kuwa karibu na njia ya haja kubwa  wanawake huathirika au hupatawa na U.T.I zaidi Kuliko wanaume, makundi mengine ambayo wako katika Atari ya kuambukizwa ugonjwa huu ni watoto wadogo na wanaume wasio tahiriwa.

AINA ZA U.T.I


Aina hizi za U.T.I  hutegemea ni katika  eneo gani katika njia ya mkojo iliyo athiriwa hivyo kuna ;
~MAAMBUKIZI KATIKA KIBOFU CHA MKOJO(CYSTITIS)/ INFECTION OF THE BLADDER
~ MAAMBUKIZI KATIKA URETHRA (AU NJIA YA MKOJO KUTOKA KATIKA KIBOFU MPAKA NJE YA ENEO LA UTUPU KUPITIA UKE AU UUME)

VISABABISHI VYA KUUGUA UTI


Kuna vitu au mazingira mbali mbali yanayoweza sababisha mtu kupatwa na ugon
jwa wa U.T.I kama ifuatavyo;

1.Kufanya mapenzi hasa  bila kinga hii nikwasababu wakati wa tendo la ndoa bacteria ni rahisi sana kusambaa ktk urethra

2. Kubana mkojo yani kutokwenda haja wakati umebanwa na mkojo kwa muda mrefu ambapo husababisha misuli ya kibofu kupunguza uwezo wake na hivyo nirahusi kuambukizwa U.T.I

3.Upungufu wa hormoni za oestrogens kwa wanawake, husababisha bacteria kuzaliana kwa urahisi

4.Ujauzito na ukomo wa hedhi

5.kisukari

6.Kutokunywa maji mengi ya kutosha

7.uchafu(vyoo, nguo za ndani,kuingiza vidole vichafu)

8.matumizi ya dawa za antibacteria kwa muda mrefu.

9. Matumizi ya vitu vya kemikali ukeni (pads,sabuni,manukato n.k)

10.maambukizi katika via vya uzazi( uke na vulva)


DALILI  ZA UGONJWA WA U.T.I


1.Maumivu makali au kuwaka moto wakati wa kukojoa

2.Kukojoa mkojo kidogo sana na wakati mwingine ukiwa umechanganyika na damu

3.kubanwa sana ghafla na mkojo

4.maumivu ya Mgongo,Tumbo la chini na katika nyonga

5.kuchoka ovyo,kukosa hamu ya kula na kukosa hamu ya kufanya mapenzi

6.Kukojoa mara kwa Mara kama mara sita au zaidi kwa siku

7.kukojoa mkojo wenye harufu mbaya

8.Matatizo ya figo endapo vijidudu vitasambaa mpaka kwenye figo na kusababisha; homa,kichefuchefu,kutapika n.k

NAMNA YA KUJIKINGA ILI USIPATE UTI MARA KWA MARA

[i] kunywa maji mengi, kiasi cha lita 3 kwa siku, maji husaidia kuflashi bacteria mara kwa mara ambao wanakuwa wamesalia katika njia ya mkojo hvyo kuepusha maambukizi.
[ii] kwa wanawake haikisha unaenda haja ndogo baada ya tendo la ndoa, ili kuodoa bacteria kwenye njia ya mkojo na kupunguza kasi ya kusambaa kwa bacteria.
[iii] kwa wanawake pia hakikisha unapotumia tissue ama wipes baada ya kwenda haja unajifuta kutoka mbele kwenda nyuma(front to back wiping) ili kuzuia kuhamisha bacteria kutoka kwenye njia ya haja kubwa kwenda kwenye njia ya mkojo.
[iv] Pia epuka matumizi ya maji kwenye vyoo vya umma ama jumuiya.

MATIBABU

Matibabu yapo na watu hupona ninakushauri upate vipimo na ushauri wa madakitari au na washauri wa afya kabla haujapata tiba.
1.Mara nyingi tiba za mahospitali huwa hazimalizi tatzo kutokana na kwamba hazitibu chanzo cha tatzo, hvo hupelekea watu wengine tatzo kuwa sugu na kujirudiarudia baada ya mda mfupi.
Tatzo hili huweza kumalizwa vzuri kama mgonjwa akitumia tiba ya mimea na matunda ambayo imetengenezwa kwa technologia  rafiki.

Dawa ya Garlic oil Capsule

Kazi na faida ya Garlic oil capsule kwa Mgonjwa wa UTI

  • Kupambana na bacteria wabaya na fangus kwenye mwili na 
  • Kuimarisha Afya ya mwili kwa kuimarisha kinga.
  • Yafaa zaidi kutumiwa na wenye magonjwa kama UTI,TB, PID, fangasi na pneumonia

Tupige kwa namba 

0714206306

 huduma ya dawa zetu za asili

Tiba ni Tsh 75,000/=  

Bofya hapa Kuchati na Daktari kwa whatsapp


Kumbuka kushare makala hii ili watu waelimike zaidi.

Usiache kupitia somo letu linalofuata: Maambukizi kwenye njia ya uzazi husababisha ugumba na kutokwa na uchafu ukeni

Comments

Popular posts from this blog

KUTOKWA NA UCHAFU UKENI, CHANZO NA TIBA YAKE

Uke wa mwanamke hufanya kazi ya kutoa njia kati ya sehemu ya nje ya mwili na viungo vya uzazi vya ndani vya mwanamke. Hali ya kawaida ya majimaji yaliyomo katika uke wa mwanamke huwa ni ya tindikali ili kuzuia maambukizi ya vijidudu wa kuleta maradhi. Hali hii ya utindikali huletwa na bacteria waishio katika uke wa mwanamke. Bacteria hawa ni wa kawaida na hawana madhara kwa mwili. Uke ulio katika hali nzuri hutoa majimaji haya ili kujisafisha. Majimaji haya yanayotengenezwa katika uke na kwenye eno la cervix hufanya kazi ya kuondoa seli zilizokufa na bacteria waharibifu nje ya mwili na huu ndio uchafu wa kawaida ambao mwanamke hutoa ukeni. Kutoa uchafu huu sehemu za siri ni njia ya kuusafisha uke na kuzuia maambukizi ya magonjwa. Kitu cho chote ambacho kitaharibu uwiano wa utengeneaji wa majimaji haya ndani ya uke kinaweza kujenga mazingira ya maambukizi katika uke. Uchafu Wa Sehemu Za Siri  Wa Kawaida Wanawake wote hutoa uchafu sehemu za siri. Kiwango cha uchafu unaotoka, ra

JINSI YA KUONGEZA UFANISI WA VICHOCHEO VYA KIUME (TESTOSTERONE) NA KUKINGA DHIDI YA MATATIZO YATOKANAYO NA KUKUA KWA TEZI DUME KWA KUTUMIA VYAKULA HIVI VI 5

Maelezo ya utangulizi. Kichocheo cha testosterone, japo huusishwa zaidi na upande wa mwananume ni muhimu kwa afya ya pande zote mbili yaani mwanamke na mwanamme pia.kadiri umri unavoenda mbele basi kiwango cha uzalishaji wa kichocheo cha testerone kupungua, kupungua kwa kichocheo hiki kunaambatana na ukuaji wa tezi dume (prostate gland),kupotea kwa nywele na pia saratani mfano saratani ya tezi dume. .KAZI KUBWA YA KICHOCHEO HIKI NI KUONGEZA MSUKUMO NA HAMU YA TENDO LA NDOA , KUIMARISHA MISULI NA MIFUPA MWILINI. NINI KINAHITAJIKA ILI KUZALISHA KICHOCHEO CHA TESTOSTERONE? Ili kuhakikisha uzalishaji wa kichocheo cha kiume unafanyika, mwili unahitaji virutubisho au viini lishe mbalimbali, baadhi ya viini lishe hivyo ni madini ya ZINC na vitamin D3,  vitamini D inaweza kuzalishwa na mwili pale ngozi yako inapokutana na mwanga wa jua, hapa nazungumzia mwanga wa asubuhi wakati jua ndo linachomoza na pia lile jua la jion karibia na kuzama, hivyo utakubaliana na mimi kuwa wengi wet

MADHARA YA PUNYETO NA TIBA YAKE

MAELEZO  YA AWALI KUHUSU TATIZO LA UPIGAJI PUNYETO Watu wengi sana wanataka kufahamu jinsi gani wafanye ili kuachana na kitendo cha upigaji punyeto. Punyeto ni tendo la mtu la kuamsha hisia za mapenzi au msisimko ambao unampelekea mtu huyu kufikia kilele cha kujimalizia tamaa zake! Bila kufanya tendo halisi, hutumia fikra zake katika picha za zinazoitwa za ngono au picha zozote zinazoweza kulifanikisha tendo hilo, movie n.k. Kilele cha yote anafikia mahali anajimalzia tamaa zake mwenyewe!. Nimekuwa nikiona baadhi ya watu wanaosema wameelimika wakipingana wao kwa wao katika suala zima la kupiga punyeto! Wako wanaotetea kutokana na elimu yao na wanasema kwa ujasiri mkubwa kwamba "kupiga punyeto ni sehemu ya maisha ya mwanadamu" Ina maana katika maisha ya mwanadamu upigaji punyeto inaelezwa ni kama tendo la lazima mpaka inafikia mahali wanasema ni sehemu ya maisha (Maisha) ya mwanadamu. Nimekuwa nikipata kesi nyingi sana juu ya madhara yatokanayo na punyeto. Aslimia 60