Skip to main content

KUKOSA CHOO KWA MDA MREFU AMA KUPATA CHOO KIGUMU ( CONSTIPATION) NA MADHARA YAKE KIAFYA




Maelezo ya utangulizi

Mwili wako ni mfano wa silinda kubwa ambayo ndani yake kuna tube inayoanzia mdomoni mpaka chini  kwenye puru pale unakotolea uchafu, silinda hii ndio mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Hivyo mfumo wa chakula upo ndani ya mwili na umesheheni kemikali mbalimbali ambazo husaidia usagaji na uchkataji wa chakula ili kupata virutubisho vinavyohitajika na mwili. Mfumo wa chakula unachangia karibu asilimia 80 ya utimamu wa afya yako . usagaji  wa chakula huanzia mdomoni pale unapotafuna chakula na kikachanganyika na mate.

Usagaji na uchakataji wa chakula huishia kwenye utumbo mpana baada ya mwili kufyonza virutubisho muhimu na maji na kuacha takataka ambazo hazitumiki, virutubusho ambavyo vinavyonzwa ili kutoa energy ambazo ndio tunaita kalori. Kalori kiasi gani unakula na pia ubora na chanzo cha kalori ama chakula unachokula ni sababu za msingi ambazo zinaathiri afya yako aidha chanya au hasi. Sababu nyingine ambayo inaleta matokeo kwenye  afya yako na hatari ya kupata cho kigumu ni kiasi na aina ya bacteria waliopo katika mfumo wako wa chakula. 
Bacteria hawa wamegawanyika sehemu mbili kuna bacteria wazuri ambao husaidia usagaji wa chakula na bakteria wabaya ambayo ndio chanzo cha matatizo ya tumbo na utumbo, kusababisha  aleji, uzito mkubwa na kitambi pamoja na matatizo mengine mengi. Watafiti waligundua kwamba pale ambapo msongo wa mawazo huleta athari katika mfumo wa chakula basi ndivyo pia mfumo wako wa chakula unavoweza kuleta athari katika ubongo ikiwemo kumfanya mtu kuwa na hasira, kwa maneno mengine tunaweza kusema hivi mfumo wako wa umeng ‘enyaji chakula siyo tu unahishwa na matatizo kama kukosa choo/choo kigumu, kuharisha, uzito mkubwa na kitambi ni zaidi ya hapo hata maamuzi yako yantegemea pia vyakula unavyokula.


MAKUNDI YA WATU WALIOPO KATIKA HATARI YA KUPATA CONSTIPATION NA KWANINI??

Baadhi ya visababishi vya kukosa choo ama kupata choo kigumu ni kama matumiz ya muda mrefu ya vidonge mfano vidonge vya kupunguza tindikali tumboni,  ufanyaji kazi mdogo wa tezi ya thairodi (hypothyroidism), magonjwa ya mfumo wa chakula kama irritable bowel syndrome(IBS), kuchelewa kutoa haja mfano mtu anapojizuia kutumia vyoo vya umma. Cha kukumbuka ni kwamba moja ya chanzo cha haya yote ni lishe, sanasana kama lishe yako inategemea zaidi vyakula vilivyosindikwa na vyenye nyuzinyuzi kidogo. Yafuatayo ni magroup ya watu waliopo katika hatari zaidi ya kupata constipation
1.      WANAWAKE, zaidi wanawake wenye ujauzito na baada tu ya kujifungua. Uzito wa mtoto hukandamiza utumbo na hivo kupunguza usafirishaji wa choo kwenye utumbo na hivo kupelekea maji mengi kufyonzwa. Nb napenda msomaji ufahamu kuwa maji hufyonwa kwenye utumbo mpana ambako choo kinakaribia kutoka, hivo choo kinavokaa zaidi bila kutolewa ndivo maji yake hufyonwa zaidi na kukifanya kiwe kigumu kama cha mbuzi.
2.       WAZEE wapo katika hatari zaidi ya kupata constipation kwa sabau ya kupungua kwa kasi ya kazi za mwili na hvo kupunguza kasi ya usafirishaji katika mfumo wa chakula.
3.      WATU WENYE KIPATO KIDOGO kutokana na kutokuwa na uwezo wa kununua vyakula salama na asili visivyosindikwa
4.      Waliofanyiwa upasuajikutokana na kwamba hawafanyi kazi mda mwingi wametulia na hivo kupelekea kasi ya usafirishaji wa choo pia kupungua.

UHUSIANO KATI YA CONSTIPATION NA AFYA YA MWILI

Kupata choo kigumu ambako kunapelekea mtu kutumia nguvu nyingi kujikamua ili kutoa kinyesi kunaweza kukusababishia kupata ugonjwa wa bawasiri ama Hemorrhoids ambapo ni matokeo ya kutanuka kwa mishipa ya damu, kutanuka kwa mishipa hii ya damu hupelekea kinyama kuota aidha ndani au nje ya sehemu ya haja kubwa na kupelekea maumivu makali. Pia constipation ya mda mrefu inaweza kupelekea kulegea kwa via vya uzazi kwa mwanamke, hii ni kutokana na kwamba sehemu ya uzazi na ile ya haja kubwa zipo karibu sana, presha inayotengenezwa baada ya kusukuma choo kwa nguvu basi inaweza kupelekea kulegea kwa mishipa na kuweza kuleta matatizo kama kurudi kwa  mkojo kwenye figo ambayo inaweza kuleta matatizo ya moja kwa moja ya figo. Hivo unapopata haja basi usikawie kutoa maana kukaa mda mrefu kutasababisha uchafu mwingi kukusanyika  na hivo ukatumia nguvu nyin haja gi kusukuma uchafu, ambapo wakati mwingine hii inaweza kuleta shida na utumbo ukatoka nje ya njia ya haja kubwa.
MTINDO WA MAISHA UTAKAOKUSAIDIA KUTIBU TATIZO
Kwa ambaye tatizo limekufikia hatua mbaya basi suluhisho lako ni kubadili mfumo wa maisha ikiwemo kwenye lishe, hatua ya kwanza na rahisi ni kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha.Pili matumizi ya vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi husaidia katika kuleta shape ya choo na kuepuka choo kigumu,hakikisha kila siku unakula vyakula gramu 30 mpaka 32 vyenye nyuzi nyuzi mfano mboga za majani.
mazoezi ya mwili husaidia kurahisisha usafiri na utoaji wa takamwili kiurahisi hivo weka ratiba walau mara 3 kwa week kufanya mazoezi na Nne vyoo vya kukalia ni hatari kwa afya yako kwani vinakusababishia matumizi makubwa ya nguvu wakati wa kujisaidia na hivo kupelekea constipation na matatizo mengine kama bawasiri, tumia vyoo vya kawaida vya kuchuchumaa kama miili yetu ilivoumbwa. Kama tatizo ni kubwa basi unaweza kutujulisha ukafika ofsini kwetu na ukajipatia dawa za mimea.

Mafuta ya Ginseng


Faida na matumizi ya mafuta ya ginseng
1. Kuimarisha uchakataji wa chakula
2. kutibu tatizo la kukosa choo na gesi tumboni na 
3. Kusafisha tumbo

Gharama ya mafuta ni Tsh 60,000/= 
Tupigie kwa namba 0762336530 au


Bofya hapa Kuchati na muhudumu kwa Whatsapp


 ambapo tutakupatia dawa na kirutubisho pamoja na ushauri wa kitaalamu juu ya tatizo lolote la mfumo wa chakula.
Kama upo mkoani basi usihofu maana utatumiwa dawa baada ya kufanya malipo
Ofisi zetu zipo Magomeni Mwembechai.

Comments

Popular posts from this blog

KUTOKWA NA UCHAFU UKENI, CHANZO NA TIBA YAKE

Uke wa mwanamke hufanya kazi ya kutoa njia kati ya sehemu ya nje ya mwili na viungo vya uzazi vya ndani vya mwanamke. Hali ya kawaida ya majimaji yaliyomo katika uke wa mwanamke huwa ni ya tindikali ili kuzuia maambukizi ya vijidudu wa kuleta maradhi. Hali hii ya utindikali huletwa na bacteria waishio katika uke wa mwanamke. Bacteria hawa ni wa kawaida na hawana madhara kwa mwili. Uke ulio katika hali nzuri hutoa majimaji haya ili kujisafisha. Majimaji haya yanayotengenezwa katika uke na kwenye eno la cervix hufanya kazi ya kuondoa seli zilizokufa na bacteria waharibifu nje ya mwili na huu ndio uchafu wa kawaida ambao mwanamke hutoa ukeni. Kutoa uchafu huu sehemu za siri ni njia ya kuusafisha uke na kuzuia maambukizi ya magonjwa. Kitu cho chote ambacho kitaharibu uwiano wa utengeneaji wa majimaji haya ndani ya uke kinaweza kujenga mazingira ya maambukizi katika uke. Uchafu Wa Sehemu Za Siri  Wa Kawaida Wanawake wote hutoa uchafu sehemu z...

JINSI YA KUONGEZA UFANISI WA VICHOCHEO VYA KIUME (TESTOSTERONE) NA KUKINGA DHIDI YA MATATIZO YATOKANAYO NA KUKUA KWA TEZI DUME KWA KUTUMIA VYAKULA HIVI VI 5

Maelezo ya utangulizi. Kichocheo cha testosterone, japo huusishwa zaidi na upande wa mwananume ni muhimu kwa afya ya pande zote mbili yaani mwanamke na mwanamme pia.kadiri umri unavoenda mbele basi kiwango cha uzalishaji wa kichocheo cha testerone kupungua, kupungua kwa kichocheo hiki kunaambatana na ukuaji wa tezi dume (prostate gland),kupotea kwa nywele na pia saratani mfano saratani ya tezi dume. .KAZI KUBWA YA KICHOCHEO HIKI NI KUONGEZA MSUKUMO NA HAMU YA TENDO LA NDOA , KUIMARISHA MISULI NA MIFUPA MWILINI. NINI KINAHITAJIKA ILI KUZALISHA KICHOCHEO CHA TESTOSTERONE? Ili kuhakikisha uzalishaji wa kichocheo cha kiume unafanyika, mwili unahitaji virutubisho au viini lishe mbalimbali, baadhi ya viini lishe hivyo ni madini ya ZINC na vitamin D3,  vitamini D inaweza kuzalishwa na mwili pale ngozi yako inapokutana na mwanga wa jua, hapa nazungumzia mwanga wa asubuhi wakati jua ndo linachomoza na pia lile jua la jion karibia na kuzama, hivyo utakubaliana na mimi kuwa wengi...

MADHARA YA PUNYETO NA TIBA YAKE

MAELEZO  YA AWALI KUHUSU TATIZO LA UPIGAJI PUNYETO Watu wengi sana wanataka kufahamu jinsi gani wafanye ili kuachana na kitendo cha upigaji punyeto. Punyeto ni tendo la mtu la kuamsha hisia za mapenzi au msisimko ambao unampelekea mtu huyu kufikia kilele cha kujimalizia tamaa zake! Bila kufanya tendo halisi, hutumia fikra zake katika picha za zinazoitwa za ngono au picha zozote zinazoweza kulifanikisha tendo hilo, movie n.k. Kilele cha yote anafikia mahali anajimalzia tamaa zake mwenyewe!. Nimekuwa nikiona baadhi ya watu wanaosema wameelimika wakipingana wao kwa wao katika suala zima la kupiga punyeto! Wako wanaotetea kutokana na elimu yao na wanasema kwa ujasiri mkubwa kwamba "kupiga punyeto ni sehemu ya maisha ya mwanadamu" Ina maana katika maisha ya mwanadamu upigaji punyeto inaelezwa ni kama tendo la lazima mpaka inafikia mahali wanasema ni sehemu ya maisha (Maisha) ya mwanadamu. Nimekuwa nikipata kesi nyingi sana juu ya madhara yatokanayo na punyeto. Aslimia 60...