Skip to main content

MATUMIZI SAHIHI YA MAJI KWA AFYA YA MWILI WAKO.


“KUNYWA MAJI MENGI” ni msisitizo ambao umekuwa ukipewa mara nyingi labda na mama nyumbani, ama na Daktari wako au rafiki wako wa karibu, lakini ambacho hukuambiwa ni kwanini maji ni muhimu kwa afya yako na pia kiasi cha maji unachotakiwa kunywa na ubora wa maji vyote ni muhimu kufahamu. Najua swali la watu wengi ni kwamba Je ni kiasi gani cha maji unachotakiwa kunywa kila siku?? . Maji ni muhimu sana kwa afy zetu ni dhahiri kwamba unaweza kuishi bila chakula kwa siku nyingi lakini bila maji utaishi mud mfupi sana. Miili yetu kiujumla imetengenezwa kwa maji ambayo
1.      Ni muhimu katika kurahisisha umeng’enyaji wa chakula, uvyonzwaji wa virutubisho na pia utoaji wa takamwili.
2.      Kusaidia usafirishaji wa vitu mbalimbali kwenye mwili.
3.      Kurekebisha joto la mwili
4.      Kulainisha joint ili kupunguza msuguano wa mifupa na
5.      Kusafisha ngozi ya mwili
KIASI GANI CHA MAJI NATAKIWA KUNYWA??
Japo kila siku unapoteza maji kwa njia ya mkojo na jasho, maji yanayopotea yanatakiwa kufidiwa. Cha kufurahisha ni kwamba mwili umeumbwa na njia inayokwambia ni muda gani ufidie hayo maji yaliyopotea, njia hii huitwa “KIU”. Inawezekana ushauri mwingi ulopata ukikwambia kunywa lita 2 ama 3 ama 4 za maji kila siku japo ni vizuri lakini siyo ushauri sahihi. UKWELI ni kwamba hakuna kiwango kimoja ambacho kinaweza kutumika na watu wote, chukulia mfano Mcheza mpira ambaye kila siku asubuhi na jioni anapiga mazoezi kipindi cha kiangazi,na mzee wa miaka 50 ambaye hafanyi mazoezi, na mama mwenye kilo 100 wakati wa kipindi cha baridi, ni dhahiri kwamba watu hawa watatu watakuwa na ujazo tofauti kabisa katika kunywa  maji.
Hivo nashauri kwamba usikilize mwili wako unasemaje katika kuamua kiwango cha maji yanayotakiwa, pale unapopata kiu basi kunywa maji kukata kiu na usinywe soda. Njia nyingine ya kugundua uhitaji wa maji kwenye mwili ni kuangalia rangi ya mkojo, mkojo ukiwa na rangi ya Njano ilokolea basi inaonyesha kwamba una uhitaji mkubwa wa kunywa maji, ;lakini kama ni njano nyepesi basi upo sawa. NB kama unameza vidonge vya vitamin B2 basi hutaweza kufanya jaribio hili maana vidonge hivi huweza kubadilisha mkojo na kuwa njano nyepesi isiyokolea. Inashauriwa pia kunywa maji kidogo kidogo na siyo kubugia glas nyingi kwa mara moja, kutokana na ukubwa wa mwili miili yetu ina uwezo wa kutumia maji kidogo kidogo, hivo ukinywa maji mengi kwa mara moja yatatumika kidogo na mengine yatatolewa nje kama uchafu.
FANYA KIU KUWA NI MWONGOZO WAKO WA KUNYWA MAJI
Mwili unapokuwa umepoteza maji asilimia 2 mpaka 3 basi hutoa alam ambayo ni kwa njia ya kiu kukwambia kwamba unatakiwa kunywa maji. Kam una afya njema basi hakikisha unakunywa maji kila unapopata kiu na hiyo ndo itakuwa mwongozo wako wa kiasi gani cha maji uweze kunywa. Ni dhahiri kwamba kama unaishi kwenye maeneo ya joto mfano maeneo ya pwani au unafanya sana mazoezi au shughuli nzito utahitaji kunywa maji mara nyingi zaidi.

MAJI NA SIYO SODA  NDO IWE KIKATA KIU YAKO, Maji safi na salama ni kinywaji kizuri kukata kiu yako na kuujenga mwili, kama umeshakuwa mnywaji wa kupindukia wa soda basi ni vizuri ukafanya mabadiliko.

Comments

Popular posts from this blog

MADHARA YA PUNYETO NA TIBA YAKE

MAELEZO  YA AWALI KUHUSU TATIZO LA UPIGAJI PUNYETO Watu wengi sana wanataka kufahamu jinsi gani wafanye ili kuachana na kitendo cha upigaji punyeto. Punyeto ni tendo la mtu la kuamsha hisia za mapenzi au msisimko ambao unampelekea mtu huyu kufikia kilele cha kujimalizia tamaa zake! Bila kufanya tendo halisi, hutumia fikra zake katika picha za zinazoitwa za ngono au picha zozote zinazoweza kulifanikisha tendo hilo, movie n.k. Kilele cha yote anafikia mahali anajimalzia tamaa zake mwenyewe!. Nimekuwa nikiona baadhi ya watu wanaosema wameelimika wakipingana wao kwa wao katika suala zima la kupiga punyeto! Wako wanaotetea kutokana na elimu yao na wanasema kwa ujasiri mkubwa kwamba "kupiga punyeto ni sehemu ya maisha ya mwanadamu" Ina maana katika maisha ya mwanadamu upigaji punyeto inaelezwa ni kama tendo la lazima mpaka inafikia mahali wanasema ni sehemu ya maisha (Maisha) ya mwanadamu. Nimekuwa nikipata kesi nyingi sana juu ya madhara yatokanayo na punyeto. Aslimia 60...

Kisonono ni nini ?, je kuna Tiba ya kisonono ?

Nini maana ya kisonono, je naweza kupata tiba sahihi ya kisonono?  Soma makala jii upate kujifunza na kupata ueewa juu ya tatizo la kisonono ambalo limeathiri watu wengi sana kwa sasa hasa vijana wa kiume. Kisonono au kwa lugha ya kitaalamu Gonorrhea ni moja ya ugonjwa wa ngono ambao huambukizwa baada ya mtu mmoja mwenye ugonjwa kukutana kimwili mtu mwingine mzima. Kisonono mara nyingi husababisha maumivu makali na dalili zingine mbaya kwenye via vya uzazi na sehemu zingine kama, sehemu ya haja kubwa, macho na pia maumivu ya viungo. Ugonjwa huu wa kisonono huweza kuwapata watu wa jinsia zote wanawake kwa wanaume huku tafiti zikionesha kwamba wanaume ndio wanaoongoza kuambukizwa kuliko wanawake. Nnini husababisha kinonono au Gonorrhea?? Ugonjwa huu wakuambukizwa kwa njia ya ngono husababishwa na bacteria wanaoitwa Neisseria gonorrhoeae. Na hivo pale watu wanapokutana kingono bacteria hawa huweza kusambaa kwenda kwa mtu mwingine kutokana na msuguano wa viungo laini vya uza...

JINSI YA KUGUNDUA NA KUTHIBITI VIDONDA VYA TUMBO( PEPTIC ULCER)

MAELEZO YA UTANGULIZI KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO Tunashukuru kwa kuendelea kufatilia makala zetu, kwa maoni na ushauri ama uhitaji wa kufika ofisini basi endelea kutuandikia kwa namba  0714206306 .  Kupata ufahamu mpana juu ya vidonda vya tumbo ni vema kuelewa kwanza mfumo unaohusika na tumbo ambao ni umen'genyaji wa chakula. Sehemu kuu zinazohusika katika umen'genyaji huo ni kinywa,umio ambayo ni misuli wenye urefu wa sentimeta 23 ambao huunganisha koromeo na tumbo'esophagus',mfuko wa nyongo na sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo'duodenum',utumbo mdogo,kongosho,utumbo mpana na sehemu ya mwish oni ya utumbo'rectum'. Mfumo wa mmen'genyo wa chakula hasa kuta za umio,tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na tindikali inayotumika kumen'genya chakula inaposhambulia kuta hizo, hii ndiyo vidonda vya tumbo'Peptic Ulcers',vidonda vya mfumo wa umen'genyaji chakula vikiwa kwenye tumbo ni 'Gastric Ulcer'vikiwa kati...