MAELEZO YA UTANGULIZI KUHUSU TATIZO LA UZITO MKUBWA NA KITAMBI
Karibu
30% ya watu wote duniani wana uzito uliopitiliza na vitambi na hii imepelekea
matokeo makubwa katika ugonjwa wa saratani ama kansa. Repoti moja inasema kwamba inakadiriwa kuwa uzito
mkubwa na kitambi vinachangia karibu watu 500,000 wenye saratani kila mwaka.
Theluthi mbili ya kesi hizi za saratani zinatokea Ulaya na Amerika ya kaskazini.
Wanawake wakiwa kwenye hatari kubwa zaidi ukilinganisha na wanaume, aina hizi
za saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya utumbo mpana, na saratani ya
matiti. Kutokana na tafiti hizi inaonesha kwamba ifikapo mwaka 2030 basi karibu
nusu ya watu wazima duniani watakuwa na uzito mkubwa na vitambi.
Kansa
au saratani siyo tatizo moja tu linaloletekezwa na uzito mkubwa na vitambi bali
kuna magonjwa mengine mengi yanayoambatana ikiwemo, kisukari aina ya 2, matatizo
ya kupata usingizi na kukoroma usingizini, uvimbe kwenye kizazi, ngiri,
Matatizo katika njia ya mkojo, Stroke, Upungufu wa nguvu za kiume, Magonjwa ya
Moyo, Pumu, Magonjwa ya Joints na mifupa na mengine mengi . Uzito mkubwa
husababisha kutofanya kazi vizuri kwa mifumo ya mwili, kufeli kwa utendaji huo
ndipo unaletekeza magonjwa yaliyotajwa hapo juu.
NINI HASA KINACHOPELEKEA UWE NA UZITO MKUBWANA KITAMBI??
Kabla ya kuendelea nataka uelewe kwanza maana ya neno kalori, kalori ni kiasi cha nguvu (energy) kinachozalishwa baada ya kuunguzwa kwa chakula. Uzito mkubwa na kitambi siyo tu kwamba ni ulaji wa kalori nyingi na kutokufanya mazoezi ya kutosha. Mtindo wa maisha na mazingira yanachangia pia kwa kiasi kikubwa. Kutokufahamu kisababishi cha tatizo hili kimewapelekea wengi kuwa wahanga wa tatizo pasipo kujua mlango wa kutokea. Sababu hizi za kimazingira ni kama- . Matumizi makubwa za dawa za kuua bacteria kwenye utengengenezwaji wa chakula na madawa.
- Dawa zinazotumika kusisimua ukuaji wa wanyama wa chakula kama Ng’ombe na kuku.
- Kemikali zinazovuruga mfumo wa homoni mfano dawa za kuua wadudu kwenye nafaka.
- Sukari inayohifadhiwa kwenye vyakula vya viwandani
- Matumizi ya vyakula visivyokuwa salama mfano vyakula vilivyosindikwa kwa kiasi kikubwa
- Kama unataka kushugulikia swala lako la uzito na hivo kupunguza hatari ya kuugua saratani basi huna budi kutazama kwa makini unachoweka mdomoni kila siku.
SHERIA ZA KUFUATA ILI KUZUIA KITAMBI NA UZITO MKUBWA NA HIVYO KUZUIA HATARI YA SARATANI
Kwa
bahati nzuri ni kwamba magonjwa haya yote yanazuilika endapo utakuwa makini
kufuata sheria. Kinga pekee ndio bora kuliko tiba hii inajumuisha kuzuia
uongezekaji holela wa uzito. Kwa kufata sheria hizi basi naamini utakuwa
umepunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya kuongezeka uzito na saratani
- Hakikisha unanunua vyakula asili na uvipike mwenyewe jikoni kwako. Kwanza hii itapunguza matumizi ya sukari ambayo ndio chanzo kikubwa cha kufeli kwa insulin kufanya kazi na kuongezeka kwa uzito sababu vyakula vingi vya mtaani na supermarket vinaongezwa sukari nyingi, kama tayari una matatizo ya insulin basi nashauri kuacha kutumia aina zote za sukari. Hakikisha matumizi yako ya sukari yasizidi gram 25 kama wewe ni mzima na gram 15 kama una matatizo ya kisukari, presha, uzito mkubwa na kitambi na matatizo yote ya moyo. kama ukinunua chakula asili basi utakuwa umejiepusha na sumu za kuulia wadudu kwenye mazao na unapokula vyakula visivyosindikwa basi utakuwa umeepuka kula sukari. Punguza ulaji wa wanga na badala yake kula mafuta kwa wingi ikiwemo. Parachichi, Nazi na mafuta ya nazi, Siagi iliyotengenezwa maziwa asiili ya Ng’ombe, Karanga mbichi, Nyama kutoka ka mnyama aliyekuzwa kwa kulishwa majani na Mayai.
- Hakikisha unapika na kuandaa chakula chako jikoni; na inashauriwa kula theluthi moja ya chakula chako kiwe hakijapikwa , epuka upikaji sana wa chakula kwenye joto kali maana unaharibu virutubisho na kutengeneza sumu mwilini, pia hakikisha unajumuisha aina za vyakula vya kupambana na saratani kama Broccoli.
- Tumia zaidi vyombo vya udongo kuliko vya plastic kuhifadhia chakula ili kupunguza ulaji wa kemikali zitakazoharibu mfumo wa homoni.
- Kuvusha mlo/kufunga kula ni njia nzuri kama una matatizo ya insulin ama leptin, kisukari, shinikizo kubwa la damu, na matatizo mengine ya moyo, ila kumbuka kuvusha mlo siyo suluhisho la mda wote, pale homono zako zikiwa vizri basi unaweza kurudia hali yako ya kawaida ya kula vyakula salama.
- Tumia virutubisho ili kutunza bacteria wazuri walioko kwenye mfumo wako wa chakula ambao wanasaidia kupunguza maambukizi na kuimarisha kinga yako ya mwili.
- Mazoezi, mazoezi husaidia kupunguza kiasi cha insulin kwenye damu na hivyo kurahisisha kupunguza kwa uzito na kitambi.
- Vitamin D, husaidia kupunguza hatari ya kupata saratani. Chanzo kizuri cha vitamin D ni kwa kutumia mwanga wa jua.
- Usingizi, hakikisha pia unapata usingizi wa kutosha . wengi wetu tunahitaji masaa mpaka 8 ya usingizi. Usingizi kidogo basi husababisha uzalishaji mdogo wa homoni ya melatonin na hivyo kupelekea matatizo ya insulin na uzito mkubwa. Pia
- Epuka msongo wa mawazo
Naamini
utakuwa umejifunza vya kutosha basi usisahau kushare pia wenzako, kama una
maoni, maswali ama unapenda kupunguza uzito kupitia dawa zetu za mimea basi usisite kuwasiliana nasi kupitia 0762336530 au
Karibu upate dawa zilizotengenezwa kwa mimea na kuhifadhiwa kiutaalamu Wa hali ya huu. kwa gharama sh 110,000 tu. laki 1 na elfu kumi tu
Bofya hapa Kuchati na Daktari kwa Whatsapp
Ofisi zetu zipo Magomeni Mwembechai.Karibu upate dawa zilizotengenezwa kwa mimea na kuhifadhiwa kiutaalamu Wa hali ya huu. kwa gharama sh 110,000 tu. laki 1 na elfu kumi tu
Comments
Post a Comment
TUANDIKIE UJUMBE MFUPI, JUU YA TATIZO LAKO, JINSIA, UMRI, NA MAHALI UNAKOPATIKANA