Skip to main content

ZIJUE FAIDA YA KUTUMIA TANGAWIZI, HUTIBU MAGONJWA

MAELEZO YA UTANGULIZI

Tangawizi Ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa Tangawizi.
Mmea huu unafanana sana na Binzari ikiwa bado haijamenywa maganda yake. Na kwa hapa Tanzania Tangawizi hulimwa sana mikoa ya nyanda za juu Kusini na baadhi ya mikoa kama Kilimanjaro, baadhi ya maeneo ya mkoa wa Manyara, Morogoro, na kwingineko nchini.
Pia kama bidhaa inapatikana nchi nzima kwa bei nafuu kabisa na kila mtu mwenye uwezo wowote wa kiuchumi anaweza kununua aidha kwa kipande kimoja, fungu au kwa kilo pia.

Tangawizi inatumikaje ?:

Mmea huu unaweza kuonekana kama mmea wa kawaida na watu kuutumia tu kama mazoea lakini Kiungo hiki kinaweza kutumiwa kama Dawa. Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kikiwa kimekaushwa na kutengenezwa unga.

Nini Faida ya Tangawizi?

Tangawizi ni mmea kati ya mimea mingi yenye maajabu, Mmea huu unaweza kutumika kama dawa na kutibu magonjwa mengi tu zaidi ya 72 yaliyo ndani ya miili yetu na kutuacha tukiwa wazima na kutekeleza majukumu yetu ya kila siku.
Pia kiungo hiki kina faida zaidi kwa Wagonjwa hasa walio athirika na Ugonjwa wa UKIMWI. Hivyo kwa wale wenye matatizo kama haya wanaweza kupata faida zaidi ya Maajabu ya Mmea huu wa Tangawizi.
Jinsi ya kuitumia kama Dawa:
Tangawizi ikiwa imesagwa au Mbichi iliyopondwa pondwa inaweza kutumika kama Kinywaji kama ilivyozoeleka kwa watu wengi.
Namna rahisi ya kuitumia Tangawizi ni katika chai, inakuwa ni mubadala wako wa majani yale meusi ya chai ambayo yenyewe huwa na kaffein ambayo hupelekea magonjwa mengi mwilini (soma kuhusu kansa na uzito kupita kiasi kuyajuwa madhara ya kutumia majani ya chai nyeusi), Pia inaweza kutumika katika vyakula hasa nyama na mbogamboga zingine, inaweza kuongezwa katikajuisi freshi pia na kuleta radha nzuri ambayo ni dawa pia.
Hutibu Magonjwa gani ?
Tangawizi husaidia yafuatayo:
Kuongeza hamu ya kula
Kupunguza kichefuchefu
Kutapika, kuharisha
Kisukari
Shinikizo la damu
Kuongeza msukumo wa damu
Kutoa sumu mwilini
Maumivu ya tumbo na
Gesi tumboni.
husaidia uyeyushwaji wa chakula tumboni.
husaidia wakati wa matatizo ya mafua au flu na magonjwa mengine mengi.
Kama utakuwa makini au kuwahi kuwahudumia wagonjwa wa UKIMWI basi magonjwa hayo hapo juu ni kati ya Magonjwa nyemelezi yanao wasumbua sana hawa ndugu zetu hivyo wakitumia Tangawizi basi wataweza kuondokana kabisa na matatizo hayo na kuishi vizuri na kutekeleza majukumu yao ya kila siku na kuepukana na kulala tu kitandani.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUGUNDUA NA KUTHIBITI VIDONDA VYA TUMBO( PEPTIC ULCER)

MAELEZO YA UTANGULIZI KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO Tunashukuru kwa kuendelea kufatilia makala zetu, kwa maoni na ushauri ama uhitaji wa kufika ofisini basi endelea kutuandikia kwa namba  0714206306 .  Kupata ufahamu mpana juu ya vidonda vya tumbo ni vema kuelewa kwanza mfumo unaohusika na tumbo ambao ni umen'genyaji wa chakula. Sehemu kuu zinazohusika katika umen'genyaji huo ni kinywa,umio ambayo ni misuli wenye urefu wa sentimeta 23 ambao huunganisha koromeo na tumbo'esophagus',mfuko wa nyongo na sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo'duodenum',utumbo mdogo,kongosho,utumbo mpana na sehemu ya mwish oni ya utumbo'rectum'. Mfumo wa mmen'genyo wa chakula hasa kuta za umio,tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na tindikali inayotumika kumen'genya chakula inaposhambulia kuta hizo, hii ndiyo vidonda vya tumbo'Peptic Ulcers',vidonda vya mfumo wa umen'genyaji chakula vikiwa kwenye tumbo ni 'Gastric Ulcer'vikiwa kati...

Kisonono ni nini ?, je kuna Tiba ya kisonono ?

Nini maana ya kisonono, je naweza kupata tiba sahihi ya kisonono?  Soma makala jii upate kujifunza na kupata ueewa juu ya tatizo la kisonono ambalo limeathiri watu wengi sana kwa sasa hasa vijana wa kiume. Kisonono au kwa lugha ya kitaalamu Gonorrhea ni moja ya ugonjwa wa ngono ambao huambukizwa baada ya mtu mmoja mwenye ugonjwa kukutana kimwili mtu mwingine mzima. Kisonono mara nyingi husababisha maumivu makali na dalili zingine mbaya kwenye via vya uzazi na sehemu zingine kama, sehemu ya haja kubwa, macho na pia maumivu ya viungo. Ugonjwa huu wa kisonono huweza kuwapata watu wa jinsia zote wanawake kwa wanaume huku tafiti zikionesha kwamba wanaume ndio wanaoongoza kuambukizwa kuliko wanawake. Nnini husababisha kinonono au Gonorrhea?? Ugonjwa huu wakuambukizwa kwa njia ya ngono husababishwa na bacteria wanaoitwa Neisseria gonorrhoeae. Na hivo pale watu wanapokutana kingono bacteria hawa huweza kusambaa kwenda kwa mtu mwingine kutokana na msuguano wa viungo laini vya uza...

UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE

 FAHAMU TATIZO LA UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE (OVARIAN CYST ) Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovary) hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana kama ovarian cyst. Uvimbe huu unaweza kumtokea mwanamke wa umri wowote ingawa mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito. MAYAI YA MWANAMKE  Kwa kawaida mwanamke anakuwa na mayai mawili katika mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto. Mayai haya hupatikana pembezoni mwa mfuko wa uzazi (uterus). Mayai haya huanza kuzalisha mayai ya uzazi yanayojulikana kama ovum  ambapo mayai hayo ya uzazi hukuwa ndani ya mayai ya mwanamke (ovary) kwa kuchochewa na baadhi ya homoni.  Katikati ya mwezi, siku ya kumi na nne, saa 24-36 baada ya kiwango cha kichocheo aina ya Luteinizing Hormone kuwa juu, mayai ya uzazi hutolewa k...