Skip to main content

ANGINA PECTORIS NI NINI??

Haya ni maumivu ambayo huyapata kifuani na kukunyima amani kutokana na misuli ya moyo kukosa kiasi cha damu yenye oxygen. Kwa kawaida huu sio ugonjwa bali ni dalili ya magonjwa ya coronary heart diseases.
DALILI ZA MTU MWENYE ANGINA PECTORIS
Dalili ya kwanza ya mtu mwenye tatizo la moyo{coronary heart disease} ni angina pectori. Maumivu ya kifua kuanzia katikati kuelekea mkono wa kushoto, maumivu ya shingo na hatimaye kwenye taya bila kusahau mgongo, dalili nyingine ni kichefuchefu, kutapika,moyo kwenda mbio sana kuvuja jasho kwa wingi baada ya mwendo kasi wa moyo.
AINA ZA ANGINA PECTORIS
Stable angina pectoris: aina hii ndio ujitokeza mara nyingi zaidi ya zingine. Hali huwa mbaya tu unapokuwa unafanya kazi au mazoezi au kitu chochote kinachoweza sababisha moyo kufanya kazi kwa nguvu. Hali hutulia au kurudi katika hali ya kawaida unapopumzika. haina maana kwamba kuna shambulio la moyo bali ni taarifa kuwa wakati wowote hali inaweza kuwa mbaya.
Unstable angina: hali hii haina mpangilio na hujitokeza wakati wowote. Haiwezi kutulizwa na kupumzika kama ilivyokuwa kwa stable angina, Na hata dawa haiwezi kutuliza hali hii. Aina hii ni hatari sana kwani hali hii inapojitokeza huduma ya haraka inahitajika. kwani huwa ni ashirio la shambulio la moyo ambalo linaweza kutokea wakati wowote.
Variant angina: Aina hii hutokea mara chache sana na haswa asubuhi, ukiwa umepumzika na usiku wa manane. Tatizo hili haliwezi kutatuliwa na pumzika au kutumia dawa.
Microvascular angina: aina hii ni hatari sana maumivu makali sana na ya muda mrefu. Kwa hali hii huwa ni vigumu sana kutulizwa na dawa.
Kumbuka kuwa sio kila maumivu unayoyasikia kifuani ni angina bali unaweza kuwa na matatizo mengine kama vile
Pulmonary ambolism{kuzba kwa artery za mapafu}
Maambukizi kwenye mapafu.
Aortic dissection{kuchanika kwa mishipa mikubwa}
Hypertrophic cardiomyopathy{kuathirika kwa misuli ya moyo}
Pericarditis{kuvimba nyama iuzungukayo moyo kwa ndani}
Panic attack
Angina ni ishara tosha kuwa damu inaenda kiasi kidogo sana. Na mtiririko wake kwenye misuli ya moyo haukidhi mahitaji. Shambulio la angna huongezewa na mazoezi au hali inaosababisha moyo kufanya kazi zaidi na hata misongo pia huchangia. Coronary heart disease inawezapelekea shambulio la moyo. Kutokana na damu kuzuiwa eidha kwa mishipa kupungua kipenyo au kuganda kwa damu. Shambulio la damu ambalo husababishwa na kufa kwa misuli ya moyo myocardium muscles kutokana na hawe ya oxygen na viinilishe kufika kiasi kidogo sana. Ifahamike kuwa moja ya tatu ya watu wenye shambulio la moyo hufariki dunia kutokana na kupuuzia dalili za awali.
CHANZO
Chanzo kikuu cha matatizo haya ni mrundikano mkubwa wa mafuta ya cholesterol kwenye damu na mishipa ya moyo. Hali hii utokana na matumizi makubwa ya vyakula vyenye mafuta{saturated fat}nyama, maziwa na mayai ni chanzo kikuu bila kusahau dawa za mpango wa uzazi. Hali ya kurithi pia imekuwa chanzo, uvutaji wa sigara, shinikizo la damu, uzito mkubwa na watu wasiofanya mazoezi au kazi za kukaa kwa muda mrefu. Mwanzoni ilifahamika kuwa ugonjwa huu ulikuwa unawashambulia wanaume zaidi lakin tafti za hivi karbuni idadi iko sawa japokuwa wanawake uchelewa kuupata mpaka hormone ya estrogen itakapopungua kuzalishwa.
USHAURI
Kama unapata dalili zisizo za kawaida basi muone dactari mapema kwa ushauri na tiba.
Imetolewa na Mkumbo health.
Kama tayari unasumbuliwa na tatizo na umejaribu tiba bila manufaa, hakikisha unafika ofsini kwetu hapa Dar es salaam , Magomeni Mwembechai upate huduma ya tiba ya mimea kwa gharama ya sh 120,000/= laki 1 na elfu ishirini tu

Tupigie namba 0762336530.
 kama upo mkoani basi ondoa shaka maana utatumiwa dawa baada ya kufanya malipo.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUGUNDUA NA KUTHIBITI VIDONDA VYA TUMBO( PEPTIC ULCER)

MAELEZO YA UTANGULIZI KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO Tunashukuru kwa kuendelea kufatilia makala zetu, kwa maoni na ushauri ama uhitaji wa kufika ofisini basi endelea kutuandikia kwa namba  0714206306 .  Kupata ufahamu mpana juu ya vidonda vya tumbo ni vema kuelewa kwanza mfumo unaohusika na tumbo ambao ni umen'genyaji wa chakula. Sehemu kuu zinazohusika katika umen'genyaji huo ni kinywa,umio ambayo ni misuli wenye urefu wa sentimeta 23 ambao huunganisha koromeo na tumbo'esophagus',mfuko wa nyongo na sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo'duodenum',utumbo mdogo,kongosho,utumbo mpana na sehemu ya mwish oni ya utumbo'rectum'. Mfumo wa mmen'genyo wa chakula hasa kuta za umio,tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na tindikali inayotumika kumen'genya chakula inaposhambulia kuta hizo, hii ndiyo vidonda vya tumbo'Peptic Ulcers',vidonda vya mfumo wa umen'genyaji chakula vikiwa kwenye tumbo ni 'Gastric Ulcer'vikiwa kati...

Kisonono ni nini ?, je kuna Tiba ya kisonono ?

Nini maana ya kisonono, je naweza kupata tiba sahihi ya kisonono?  Soma makala jii upate kujifunza na kupata ueewa juu ya tatizo la kisonono ambalo limeathiri watu wengi sana kwa sasa hasa vijana wa kiume. Kisonono au kwa lugha ya kitaalamu Gonorrhea ni moja ya ugonjwa wa ngono ambao huambukizwa baada ya mtu mmoja mwenye ugonjwa kukutana kimwili mtu mwingine mzima. Kisonono mara nyingi husababisha maumivu makali na dalili zingine mbaya kwenye via vya uzazi na sehemu zingine kama, sehemu ya haja kubwa, macho na pia maumivu ya viungo. Ugonjwa huu wa kisonono huweza kuwapata watu wa jinsia zote wanawake kwa wanaume huku tafiti zikionesha kwamba wanaume ndio wanaoongoza kuambukizwa kuliko wanawake. Nnini husababisha kinonono au Gonorrhea?? Ugonjwa huu wakuambukizwa kwa njia ya ngono husababishwa na bacteria wanaoitwa Neisseria gonorrhoeae. Na hivo pale watu wanapokutana kingono bacteria hawa huweza kusambaa kwenda kwa mtu mwingine kutokana na msuguano wa viungo laini vya uza...

UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE

 FAHAMU TATIZO LA UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE (OVARIAN CYST ) Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovary) hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana kama ovarian cyst. Uvimbe huu unaweza kumtokea mwanamke wa umri wowote ingawa mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito. MAYAI YA MWANAMKE  Kwa kawaida mwanamke anakuwa na mayai mawili katika mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto. Mayai haya hupatikana pembezoni mwa mfuko wa uzazi (uterus). Mayai haya huanza kuzalisha mayai ya uzazi yanayojulikana kama ovum  ambapo mayai hayo ya uzazi hukuwa ndani ya mayai ya mwanamke (ovary) kwa kuchochewa na baadhi ya homoni.  Katikati ya mwezi, siku ya kumi na nne, saa 24-36 baada ya kiwango cha kichocheo aina ya Luteinizing Hormone kuwa juu, mayai ya uzazi hutolewa k...