Skip to main content

NAMNA YA KUTUMIA TUNDA LA TOFAHA (APPLE ) KATIKA KUPUNGUZA KITAMBI/UZITO MKUBWA NA KUBORESHA KINGA YA MWILI WAKO


Leo napenda tuangalie kuusu manufaa ya tunda hili ambalo linapendwa sana na watu na pia lina gharama sana kununua hapa kwetu, kutokana tu na upekee wake

1.      Tunda hili ni miongoni mwa matunda yenye vitamin nyingi sana na viondoa sumu mwilini (ant oxidants) na mbali zaidi apple ni miongoni mwa tunda tunaloshauriwa kula na maganda yake kwani viondoa sumu hivi na vitamini vingi vinapatikana na ganda la tunda hili la apple.
Unapotaka kuwa mlaji mzuri wa tunda hili hakikisha unachagua tunda ambalo una uhakika limelimwa kienyeji kabisa kwani tunda hili ni miongoni mwa matunda yanayo ongoza duniani kwa kumwagiwa dawa za viua watududu na kemikali mbali mbali. Na kumbuka dawa nyingi za viua wadudu ni LIPOPHILIC (Ni marafiki na mafuta yapatikanayo kwenye tunda) hivyo basi dawa za wadudu huwa zinapenya ganda la matunda haya na kuingia ndani haraka sana hivyo unakiwa kuwa makini na kuhakikisha tunda lako ni asili kabisa (organic).
CHAGUA APPLE ZENYE SIFA HIZI
·         Haina kabisa kemikal
·         Apple yenye mng'ao mzuri asili sio yenye rangi iliyofifia(Dull color)
·         Chakua apple ambayo haina michubuko yoyote,shimo  na ngumu (firm)
Nina imani utafurahia utafurahia ulaji wa tunda hili kwani ni tunda ambalo limeonesha kukulinda dhidi ya maradhi mbali mbali nitakayo kwenda kuelezea.

2.      Tunda la apple ni miongoni mwa matunda ambayo yana nyuzi (fiber) nyingi sana ndani yake.
Basi kwa sababu hio napenda nikwambie kuwa aina ya fiber ipatikanayo katika tunda hili ni adimu.

KAZI YA FIBERS(NYUZI) KATIKA MIILI YETU
i. Inafanya shughuri za umeng'enyaji chakula kufanyika katika kiwango kinachostahili.
Unapokula fibers kwa wingi zinakusaidia mfumo wa umeng'enyaji chakula kufanyika polepole na hivyo hii hali itakufanya ukae muda mrefu ukiwa huna njaa kabisa tumbo limejaa.
Hivyo kwa wale wanaopenda kupunguza uzito, na wale ambao ni sugar addicted (walevi wa vyakula na vinywaji vya sukari) basi tunda hili linaweza kukata kabisa tatizo hilo na kufurahia. Watu wengi wanaotumia tunda hili sambamba na mlo wao huwasaidia sana kupunguza ulaji sana na kuwafanya muda wote wameshiba na kuwasaidia kupunguza uzito kiasi na kumaintain miili yao.

ii. Vyakula vya fibers (nyuzi) husaidia kuondoa sumu mbali mbali za vyakula mfano lead na mercury kwenye kuta za utumbo wa chakula na kukuzuia kupata magonjwa kama kansa ya utumbo mpana na mengineyo.

ii.Pia tunda hili linasaidia kuondoa constipation (choo kigumu) na kukuepusha kupata magonjwa ya mfumo wa chakula kama bawasili (vinyama sehemu za siri) kutokana na constipation ya muda mrefu.

Hivyo furahia aina hii ya fiber yani pectin katika tunda hili la apple utakuwa umejiepusha na magonjwa yafutayo
~Uzito mkubwa kupita kiasi
~Kitambi na magonjwa ya moyo
~Kiharusi yani stroke
~Bawasiri
~Mzunguko mbaya wa hedhi
~Ulevi wa vinywaji na vyakula vyenye sukari na vionjo vya kemikali
~Kisukari


3. Apple ni tunda ambalo lina aina ya sukari ambayo hutumika kuzalisha nishati ya mwili ambayo inaitwa FRUCTOSE.
Kutokana na tafiti mbali mbali hapa duniani aina hii ya sukari imeonesha kuwa chanzo kikubwa kinacho sababidha UZITO MKUBWA KUPITA KIASI, MAGONJWA YA MOYO, KISUKARI nk hivyo basi tunda hili linatakiwa liliwe katika kiwango ambacho sio hatari kwa afya yetu. Ulaji wa tunda hili bila mpangilio ni kisababishi kikubwa cha uzito mkubwa, insulini(kichocheo kinasawazisha sukari mwilini) kutofanya kazi, na kisukari cha ukubwani.
KUTOKANA NA KIWANGO KINGI CHA AINA HII YA SUKARI AMBAYO IMEKUWA NI HATARI KWA AFYA YETU AMBAYO INAKADIRIWA KUWA NI GRAMU 9.5 KWA APPLE LENYE UMBO SAIZI YA KATI.

NOTE: KAMA WEWE NI MGONJWA WA KISUKARI, UZITO MKUBWA, UNA BELLY FATS (NYAMA UZEMBE AMBAZO NI ISHARI INSULINI IMEANZA KUPATA KIPINGAMIZI KWENYE UTENDAJI)

Nakunashauri kwa siku moja kiwango cha tunda hili usizidishe gramu 15 kwa siku ambayo ni sawa APPLE MOJA NA KIGANJA CHA ZABIBU (Kumbuka apple na zabibu yote ni matunda yenye chachu unaweza kula katika mlo mmoja)

LAKINI KAMA WEWE NI MZIMA MWENYE AFYA NJEMA  yani hauna kisukari, huna uzito mkubwa, huna nyama uzembe (belly fats) ,huna mafuta mabaya kwenye moyo na mishipa ya damu (bad cholesteral)
Nakushauri kuwa unaweza kula mpaka apple 2-4 kwa siku lakini hakikisha UNAFANYA MAZOEZI YAKUTOSHA AU KUJIHUSISHA NA SHUGHURI NGUMU ZA KIMAISHA. UKIFANYA HIVYO HUWEZI KUPATA MARADHI YASABABISHWAYO NA AINA HII YA SUKARI NDANI YA TUNDA LA APPLE.

Nina IMANI KUBWA UMEJIFUNZA NAMNA GANI UNAWEZA KUANDAA TUNDA LAKO KIKUBWA NI KUZINGATIA KUWA MATUNDA MAZURI NI ORGANIC.

Hakikisha UNAFUATA SHERIA KUU SABA ZA UOASHAJI WA MATUNDA KULINGANA NA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA
1. Osha mikono yako kwa sekunde 20 kwa maji ya uvugu vugu na sabuni kabla ya kuandaa tunda lako.
2. Ondoa kipande chochote ambacho kimeharibika kwenye tunda lako
3. Osha kwa kusafisha kwa nguvu kwa kutumia maji yanayo safisi (tape water) au maji yanayotiririka.
4. Osha tunda lako vizuri kabla ya kumenya /kula kwa kutumia maji yanayotiririka
5. Kama ni matunda /mboga tumia brashi maalumu safi yenye kuondoa wadudu na kemikali mbali mbali.
6. Chukua kitambaa chako SAFI KAUSHA MATUNDA YAKO.
7. KAMA NI MBOGA KAMA KABEJI TUPA MAGANDA YA NJE NA UBAKIZE YA NDANI( Hupunguza kiwango cha kemikali, wadudu na madawa mbali mbali)

NOTE: KUMBUKA NJIA HIZO ZIMETOLEWA NA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA DUNIANI, ZINASAIDIA KUPUNGUZA DAWA ZILIZOPULIZIWA KWENYE MATUNDA, ZINASAIDIA KUONDOA WADUDU (VIMELEA) NA KUKUFANYA ULE TUNDA LAKO SALAMA.

Imeandaliwa na
Elphas Mkumbo
Inapatikana pia moja kwa moja kupitia page  yetu ya afya kwenye facebook
mkumbohealthcareproducts.

Kwa maoni na ushauri tuandikie kwa email. elifasimkumbo@gmail.com
Pia whatsap  0678626254, usisahau kushare Makala hii na marafiki zako ili tuzidi kuelimishana..

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUONGEZA UFANISI WA VICHOCHEO VYA KIUME (TESTOSTERONE) NA KUKINGA DHIDI YA MATATIZO YATOKANAYO NA KUKUA KWA TEZI DUME KWA KUTUMIA VYAKULA HIVI VI 5

Maelezo ya utangulizi. Kichocheo cha testosterone, japo huusishwa zaidi na upande wa mwananume ni muhimu kwa afya ya pande zote mbili yaani mwanamke na mwanamme pia.kadiri umri unavoenda mbele basi kiwango cha uzalishaji wa kichocheo cha testerone kupungua, kupungua kwa kichocheo hiki kunaambatana na ukuaji wa tezi dume (prostate gland),kupotea kwa nywele na pia saratani mfano saratani ya tezi dume. .KAZI KUBWA YA KICHOCHEO HIKI NI KUONGEZA MSUKUMO NA HAMU YA TENDO LA NDOA , KUIMARISHA MISULI NA MIFUPA MWILINI. NINI KINAHITAJIKA ILI KUZALISHA KICHOCHEO CHA TESTOSTERONE? Ili kuhakikisha uzalishaji wa kichocheo cha kiume unafanyika, mwili unahitaji virutubisho au viini lishe mbalimbali, baadhi ya viini lishe hivyo ni madini ya ZINC na vitamin D3,  vitamini D inaweza kuzalishwa na mwili pale ngozi yako inapokutana na mwanga wa jua, hapa nazungumzia mwanga wa asubuhi wakati jua ndo linachomoza na pia lile jua la jion karibia na kuzama, hivyo utakubaliana na mimi kuwa wengi...

KUTOKWA NA UCHAFU UKENI, CHANZO NA TIBA YAKE

Uke wa mwanamke hufanya kazi ya kutoa njia kati ya sehemu ya nje ya mwili na viungo vya uzazi vya ndani vya mwanamke. Hali ya kawaida ya majimaji yaliyomo katika uke wa mwanamke huwa ni ya tindikali ili kuzuia maambukizi ya vijidudu wa kuleta maradhi. Hali hii ya utindikali huletwa na bacteria waishio katika uke wa mwanamke. Bacteria hawa ni wa kawaida na hawana madhara kwa mwili. Uke ulio katika hali nzuri hutoa majimaji haya ili kujisafisha. Majimaji haya yanayotengenezwa katika uke na kwenye eno la cervix hufanya kazi ya kuondoa seli zilizokufa na bacteria waharibifu nje ya mwili na huu ndio uchafu wa kawaida ambao mwanamke hutoa ukeni. Kutoa uchafu huu sehemu za siri ni njia ya kuusafisha uke na kuzuia maambukizi ya magonjwa. Kitu cho chote ambacho kitaharibu uwiano wa utengeneaji wa majimaji haya ndani ya uke kinaweza kujenga mazingira ya maambukizi katika uke. Uchafu Wa Sehemu Za Siri  Wa Kawaida Wanawake wote hutoa uchafu sehemu z...

MADHARA YA PUNYETO NA TIBA YAKE

MAELEZO  YA AWALI KUHUSU TATIZO LA UPIGAJI PUNYETO Watu wengi sana wanataka kufahamu jinsi gani wafanye ili kuachana na kitendo cha upigaji punyeto. Punyeto ni tendo la mtu la kuamsha hisia za mapenzi au msisimko ambao unampelekea mtu huyu kufikia kilele cha kujimalizia tamaa zake! Bila kufanya tendo halisi, hutumia fikra zake katika picha za zinazoitwa za ngono au picha zozote zinazoweza kulifanikisha tendo hilo, movie n.k. Kilele cha yote anafikia mahali anajimalzia tamaa zake mwenyewe!. Nimekuwa nikiona baadhi ya watu wanaosema wameelimika wakipingana wao kwa wao katika suala zima la kupiga punyeto! Wako wanaotetea kutokana na elimu yao na wanasema kwa ujasiri mkubwa kwamba "kupiga punyeto ni sehemu ya maisha ya mwanadamu" Ina maana katika maisha ya mwanadamu upigaji punyeto inaelezwa ni kama tendo la lazima mpaka inafikia mahali wanasema ni sehemu ya maisha (Maisha) ya mwanadamu. Nimekuwa nikipata kesi nyingi sana juu ya madhara yatokanayo na punyeto. Aslimia 60...