Zinc ni elementi muhimu mno katika afya ya
binadamu hivi kwamba ukosefu kidogo unaweza kuleta madhara makubwa. Zinc ni ya
muhimu sana kwa sababu inapatikana ndani ya kila kiungo cha mwili cha binadmu
na inahusika kwa karibu sana na kugawanyika kwa seli za mwili. Ni antioxidant
yenye nguvu sana, inayosaidia kuzuia kansa, na pia inahusika moja kwa moja
katika ufanyaji kazi wa tezi mbalimbali za kutengeneza homoni na kuweka sawa
viwango vya homoni katika mwili. Makadiridio yasiyo rasmi yanaonyesha kuwa
asilimia 25 ya watu duniani wanakabiliwa na upungufu wa zinc na kwa sababu
mwili wa binadamu hauhifadhi zinc, tunalazimika kupata zinc kila siku.
Vyanzo vya madini ya zinc
Kwa msomaji wa makala hii, tambua kwamba huhutaji kwenda
mbali zaidi kupata madini haya muhimu kwa afya yako, maana hupatikana kwenye
vyalula vinavyotyuzunguka kiurahisi kama
1.Maini
2. Mboga za spinach
3. mbegu za maboga na karanga
4. nyama nyekundu
5. maharage na maziwa na
6. Uyoga na Parachichi
Baadhi ya dalili ambazo zitakusaidia kutambua kuwa una upungufu wa madini ya zinc ni pamoja na
- Kupungua kwa uweo wa tendo la ndoa
- Kupoteza hamu ya kula
- Kujiskia vibaya na huna mood mara kwa mara
- Kupungua kwa uwezo wa kutambua ladha ama harufu ya kitu
Kama unatambua una dalili zote hizi hapo
juu basi hakikisha unaonana na dactari wako ili uweze kupata vipimo na ushauri
wa kitaalamu.
Faida za madini ya zinc mwilini
- Kusawazisha kiwango cha sukari katika mwili
- Kusaidia utengenezwaji wa protini kwenye mwili
- Kusaidia kusapoti mfumo wa upumuaji
- Kuongeza ufananyaji kazi wa seli za mwili
- Kupunguza sumu mwilini na kusaidia mmengeyo wa chakula
UPUNGUFU ZA ZINC NA AFYA YA UZAZI
Upungufu wa zinc husababisha ugumba kwa jinsia zote, wanaume
na wanawake na kuwasababishia tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.
Kiwango kidogo cha zinc katika mwili hukuza madhara ya msongo wa mawazo katika
mwili na kuchochea uzeekaji wa haraka.
Isije ikafikiriwa kuwa upungufu wa zinc upo zaidi kwa watu wenye lishe duni au wale katika nchi zinaendelea tu. Ukweli ni kuwa tatizo hili lipo Marekani na Ulaya kwa wanaume, wanawake na watoto.
Isije ikafikiriwa kuwa upungufu wa zinc upo zaidi kwa watu wenye lishe duni au wale katika nchi zinaendelea tu. Ukweli ni kuwa tatizo hili lipo Marekani na Ulaya kwa wanaume, wanawake na watoto.
Upungufu wa zinc hubadili namna ya kusikia ladha na
kusababisha kupenda chumvi zaidi, chakula kitamu zaidi. Inaweza kujidhihirisha
kwa kuharisha, upungufu wa nguvu za mwili, uchovu sugu, ugumba, upungufu wa
kinga za mwili, kukosa kumbukumbu, kushindwa kutuliza mawazo, kuchelewa kupona
vidonda, neva kutofanya kazi vizuri, na kuunguruma kwa sauti kwenye masikio.
Afya Ya Uzazi Ya Mwanaume:
Zinc ni madini ya lazima katika kuweka testosterone kwenye
kiwango kinachotakiwa, na seli za tezi dume ya mwanamme zinahitaji kiwango cha
zinc ambacho ni mara 10 zaidi ya mahitaji ya seli nyingine za mwili ili ziwe na
afya na zifanye kazi kwa kiwango kinachotakiwa. Upungufu wa zinc kwa wanaume
huathiri uzalishaji wa testosterone, na hivo kupelekea ugumba kwa mwanaume kushindwa kumpa ujauzito mke wake, huwaweka wanaume kwenye mazingira
hatarishi ya kupata saratani ya tezi dume,. Upungufu
wa zinc umehusishwa na kukosa hamu ya kufanya mapenzi.
Afya Ya Uzazi Ya Mwanamke:
Kwa wanawake, zinc inahusika katika ukuuaji wa yai (oocyte).
Kama mwanamke atakuwa na upungufu wa zinc, yai halitakomaa vizuri na utolewaji
wa yai (ovulation) utazuiliwa , na kusababisha ugumba. Kiwango cha zinc cha
kutosha kunamwezesha mwanamke kutumia estrogen na progesterone vizuri.
Faida zingine za madini ya zinc ni pamoja na
Kuboresha Kinga Za Mwili:
Upungufu wa Zinc unaathiri kwa kiwango kikubwa mfumo wa
kinga za mwili kwa sababu upungufu huo husababisha kudorora kwa haraka kwa
ufanyaji kazi wa T cell. T cells huinua kinga za mwili wakati virusi, bakteria
, au changamoto nyingine zinapotokea. watu wenye umri mkubwa huwa kwenye hatari
ya kuwa na upungufu, sababu kubwa ikiwa ni kukosa zinc ya kutosha kutoka kwenye
milo yao. Kuna ushahidi wa kuonyesha kuwa mahitaji ya zinc huongezeka na umri
ili kuzuia uvimbe, kusaidia kinga za mwili , na kuhakikisha ufanyaji kazi wa
seli unaotakiwa.
Kulinda Mfumo Wa Mishipa Ya Moyo:
Zinc ni muhimu katika kuweka sawa afya ya seli za mishipa ya
moyo na endothelium. Endothelium ni tabaka jembamba la seli zinazotanda juu ya
mishipa ya damu na zina mchango mkubwa katika mzunguko wa damu. Kiwango kidogo
cha zinc kinaweza kusababisha kuzuiwa kwa endothelium na kusababisha kuongezeka
kwa cholesterol na uvimbe. Cholesterol na uvimbe huongeza uwezekano wa kutokea
magonjwa ya moyo.
Kupunguza hatari ya kupata Kisukari
Zinc huhitajika katika kuhakikisha homoni nyingi zinafanya
kazi vizuri, pamoja na insulin. Zinc hunata kwenye insulin na kusababisha
insulin kuhifadhiwa kwa wingi ndani ya kongosho na kutolewa pale glucose
inapoingia kwenye mfumo wa damu. Pili, zinc inaisaidia insulin kunata kwenye
seli na kufungua mlango ili glucose iweze kuingia. Ikiwa seli hazitataka
kuipokea insulin, glucose itabakia ndani ya mfumo wa damu, itasababisha kiwango
cha sukari kuwa juu, na kusababisha kuongezeka kwa mafuta. Kiwango cha zinc
kinaposhuka, utolewaji wa insulin utapungua na pia upokewaji wa insulin hiyo,
ambapo hali ikiendelea, tatizo la kisukari hutokea. Utafiti wa hivi karibuni
huko Hispania uliohusisha wanafunzi ulionyesha uhusiano wa moja kwa moja kati
ya upungufu wa zinc, uwingi wa mafuta mwilini, na mwili kutoipokea insulin.
Kiondoa Sumu Chenye Nguvu
Kudorora kwa afya ya neva na ugonjwa wa Alzheimer's
huchochewa na kujikusanya kwa metal nzito katika ubongo. Zinc husaidia kuondoa
sumu hizi na kusaidia katika kuboresha ufanyaji kazi wa seli za ubongo
(cellular homeostasis). Zinc ina mchango mkubwa sana katika shughuli za
mawasiliano baina ya neva na husaidia kuweka sawa afya na umbo la ubongo. Pia,
zinc ni sehemu ya kimeng'enya kinachohusika katika kuvunjavunja mafuta katika
ngozi nyembamba inayofunika ubongo. Hii ni kazi muhimu sana kwa sababu katika
kutunza afya ya ubongo na ufanyaji wake kazi, inatakiwa kuhakikisha kuwa ngozi
hii nyembamba inapata virutubisho inavyovihitaji.
Kuzuia kutoka kwa saratani
Kuweka viwango vizuri vya zinc katika miili yetu kumeonyesha
kuwa kunaweza kusaidia kuponya matatizo mengi sugu ya kiafya, hasa kansa na
upungufu wa kinga za mwili. Pamoja na kansa ya tezi dume, upungufu wa zinc
umeonyesha kuhusika sana katika kujenga karibu aina zote za kansa. Utafiti wa
hivi karibuni umehusisha upungufu wa zinc na kansa za maziwa, utumbo mkubwa,
ovari, mapafu , ngozi, na leukemia.
NB, kama una matatizo ya ugumba na kutopata motto basi
nashauri mke na mume wafike kituo cha afya wote wawili waweze kupata vipimo ili
kujua chanbzo cha tatizo hapo ndipo wanaweza kuanza kutumia dawa.
Kwa wale akina mama wenye matatizo ya homoni, kuvurugika kwa hedhi na kukosa ujauzito kwa mda mrefu basi tumewaandalia programme ya week 3 ambayo itakusaidia kubalansi homoni zako na kurejesha uwezo wa kushika ujauzito. Tunashauri wanandoa wote kufanya vipimo ili kujua chanzo cha tatizo lako la kushindwa kushika ujauzito. karibu nawe upate huduma hii ya virutubisho na dawa zetu za asili ili uwe mmoja wa mashuhuda na mwenye furaha kama baadhi ya hawa wagonjwa tuliokwisha kuwapa huduma.
UTAFITI UNASEMAJE KUHUSU TIBA NA VIRUTUBISHO VYA KUSAWAZISHA HOMONI ZA KIKE.
1. Zinc capsules
Kwa wanawake, MADINI YA ZINC yanahusika katika ukuuaji wa yai (oocyte). Kama mwanamke atakuwa na upungufu wa zinc, yai halitakomaa vizuri na utolewaji wa yai (ovulation) utazuiliwa , na kusababisha ugumba. Kiwango cha zinc cha kutosha kunamwezesha mwanamke kutumia estrogen na progesterone vizuri. hakikisha unapata virutubisho kutoka kwenye vyanzo vilivyothibitishwa.
2. Soy capsules
vidonge hivi vilivyotengenezwa kiasili kwa kutumia viambata vya mimea ya Semen Glycine, Radiz Paeoniae Alba Eztractum na Ganoderma husaidia: kuongeza ufanyaji kazi wa mfuko wa mayai (ovaries), kuzuia Saratani ya matiti, kuimarisha afya ya mifupa kwa wanawake waliokoma hedhi.(menopause).
Shuhuda za Wagonjwa Kushika Ujauzito baada ya Kutumia Zinc, Vig power na Soy power
Naamini nawe unatamani kufikia malengo haya na umehangaika hospitali nyingi bila msaada, basi anza kurejesha tumaini lako.
Unaweza kuwa wewe ni mzima hivo mfahamishe na mwingine kuhusu huduma hii. karibu.
Maelezo ya mwisho
Kwa wagonjwa wenye shida katika kushika ujauzito, tunawashauri kufanya vipimo wote wawili mke na mume ili kujua chanzo cha tatizo. Baada ya hapo tunaweza kuwaanzishia huduma yetu
Comments
Post a Comment
TUANDIKIE UJUMBE MFUPI, JUU YA TATIZO LAKO, JINSIA, UMRI, NA MAHALI UNAKOPATIKANA