Kuumwa tumbo wakati wa hedhi
Tumbo la hedhi au maumivu wakati wa hedhi (period pains) au
kitaalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au
kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo. Maumivu
hayo huweza kuwa madogo au ya wastani huku baadhi ya wanawake wakipata maumivu
makali sana. Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi huanza pale mayai yanapotoka
katika mirija (fallopian tubes) na kuteremka chini ya mirija hiyo wakati wa
Ovulation.
Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili.
Aina ya kwanza au (Primary Dysmenorrhea;
Ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Maumivu hayo huanza siku moja au mbili kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.Aina ya pili au (Secondary Dysmenorrhea)
Ni yale maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba kama vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na matatizo katika mirija ya mayai.
Takribani nusu ya wanawake wote waliopo katika umri wa kuweza
kupata mototo wanakumbana na maumvu wakati wa hedhi, maumivu ambayo huanza siku
chache kabla ya hedhi na kuendelea kwa
siku kadhaa. Baadhi ya wanawake hupata maumivu ya kawaida lakini kwa wengine
maumivu huwa makali sana hadi kupelekea kushindwa kufanya shuguli zao. Hii ni
moja ya sababu watoto wa shule kukosa vpindi kwa siku kadhaa. Ili kupata tiba
basi wanawake wengi hukimbilia kunywa dawa za kupunguza maumivu na baadhi ya
madactari hutoa ushauri wa kunywa vidonge ili kuzuia hedhi ili kupunguza makali
ya maumivu, njia zote hizi mbili zikiwa na madhara na pia kutoweza kutoa
suluhisho ala kudumu la tatizo husika.
Uchunguzi unaonyesha kuwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza
kuongeza uwezekano wa kuumwa tumbo wakati wa hedhi.
• Kuwa na umri wa chini ya miaka 20.
• Kuvunja ungo wakati wa miaka 11 au chini ya miaka hiyo.
• Kutoka na damu nyingi wakati wa hedhi. (suala hilo linaweza
kusababishwa na matatizo mbalimbali ya kitiba).
• Wanawake ambao hawajawahi kuzaa.
Maumivu ya Tumbo la Hedhi... Sehemu ya Pili
Hii inahusisha magonjwa ambayo husababisha mtu kupatwa na
maumivu ya tumbo la hedhi. Miongoni mwa magonjwa hayo ni:
• Endometriosis. Hii ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa
uzazi huanza kuota nje ya fuko hilo, au hta sehemu nyinginezo.
• Adenomyosis: Huu ni ugonjwa wa wanawake ambapo tezi au
uvimbe (tumors) zinaoota katika mfuko wa uzazi.
• PID au Ugonjwa wa uvimbe katika nyonga
• Magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya
kuambukiza ya zinaa.
• Mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu
ya hedhi isitoke kwa urahisi.
Baada ya kujua baadhi ya matatizo ya wanawake yanayoweza
kusabibisha hedhi inayoambatana na maumivu ya tumbo,
hebu sasa na tuzijue tumbo la mwezi linaumaje?
1. Maumivu mara nyingi si makali.
2. Muumivu huja na kuondoka, na kwa kiwango tofauti
3. Maumivu zaidi huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo.
4. Huchanganyika na maumivu ya sehemu ya chini ya mgongoni
ambayo husambaa mpaka mapajani.
5. Kujihisi kutapika, kichefuchefu na wakati mwingine hata
kutokwa jasho.
6. Kupata choo kilaini au hata kuharisha.
7. Kufunga choo.
8. Tumbo kuwa kubwa au kuwa gumu.
9. Kuhisi maumivu ya kichwa.
10. Kutojihisi vizuri au kujisikia kuchoka.
Inapasa kujua kuwa, kiwango cha maumivu ya tumbo la hedhi na
mchanganyiko wa dalili inategemea mtu na mtu, mtu mwingine anaweza akawa
anapata karibu dalili zote nilizozitaja hapo juu na mwingine ni baadhi tu au
hata dalili moja. Wanawake wengi hutambua wanapopata tumbo la hedhi bila hata
msaada wa daktari. Wanawake wanashauri iwapo watapata maumivu makali sana ni
bora wakamuone daktari ili wafanye vipimo kama vile Ultrasound, CT na CT-Scan,
MRI na vinginevyo ili kufahamu iwapo matatizo mengine ya kitiba yanayosababisha
maumivu hayo kuwa makali.
Kuna baadhi ya tiba za mitishamba pia ambazo husadia
kupunguza muamivu ya tumbo la hedhi. Hapa namaanisha herbal, wenzetu Wachina ni
watalamu wazuri katika ujuzi huo unaweza kuagiza kutoka ofsini kwetu moja kwa
moja na ukazipata. Vilevile wanawake washauriwa kufanya baadhi ya vitendo
ambavyo hupunguza maumivu hayo, baadhi ya hivyo vimetaja kama kuoga maji moto,
kutumia hot bottle na hata kuweka kitambaa chenye joto katika sehemu ya chini
ya tumbo. Kuna baadhi husaidia kwa kufanya mazoezi kama yoga, meditation,
kusuliwa, tiba ya sindano (Acupunture), au kushituliwa mishipa ya fahamu (
Transcitaneous Electric Nerve Stimulation na hata wengine husaidiwa kwa tendo
la kujamiiana. Vilevile kutumia vidonge vya vitamin E, Thiamine na Omega 3
kumetajwa kuwa husaidia katika suala hilo. Wanawake wanaopatwa na matatizo kama
hayo ni bora wapumzike vyema na kupata usingizi wa kutosha.
Tunaelezwa kuwa tunaweza kujiepusha na kupatwa na maumivu ya
tumbo la mwezi kwa kufanya yafuatayo:
Kujitahidi kula matunda, mbogamboga na kuacha kunywa vinywaji
ambavyo ni high fructose corn syrup( juis na soda zote) pombe, caffeini, Sodium
na sukari.
Kufanya mazoezi.
Kujiepusha na wasiwasi na mawazo.
Kuepuka kuvuta sigara.
VITAMINI D
Sasa watafiti wamegundua njia ingine ambayo ni salama kwa
ajili ya kupunguza maumivu makali wakati wa hedhi ambayo ni Vitamin D kutoka
kwenye jua. Wakati wa hedhi mfuko wa mimba hujipunguza kwa kumomonyoka endapo
yai halikurutubishwa, kumomonyoka huku huletekezwa na kichocheo kinachoitwa
prostaglandin. Hvo kiasi kikubwa cha kichocheo hiki basi hupelekea ,maumivu
kuwa makubwa zaidi. Vitamin D itakusaidia kupunguza uzalishaji wa homoni hii ya
prostaglandin. Watu wengi wana upungufu wa vitamin D kutokana na kutotumia mda
mwingi kupata mwanga wa jua na hivo kupelekea
pia matatizo mengine ya kiafya kama magonjwa ya shinikizo la damu na
saratani pia. Hivo hakikisha kila siku unatumia mda wa kutosha kupata mwanga wa
jua la asubuhi ama jioni
KIRUTUBISHO CHA VITAMIN E
Kazi na faida za kirutubisho hiki cha Vitamin E kwa Mwanamke
- Kupunguza maumivu tumbo wakati wa hedhi yanayotokana na uwiano mbovu wa homoni
- Kumkinga mwanamke dhidi ya magonjwa ya matiti ikiwemo saratani
- Kuimarisha ufanyaji kazi wa ubongo na kumbukumbu
- Kukinga mwili dhidi ya magonjwa ya moyo na
- Kutoa sumu mwili.
- kupata kirutubisho hiki kwa Tsh 75,000/= pekee.
- Bofya hapa Kuchati na Daktari kwa whatsapp
Ofisi zetu zipo Magomeni Mwembechai.
Comments
Post a Comment
TUANDIKIE UJUMBE MFUPI, JUU YA TATIZO LAKO, JINSIA, UMRI, NA MAHALI UNAKOPATIKANA