Skip to main content

GOUT, USHAURI NA TIBA

MAELEZO YA UTANGULIZI KUHUSU UGONJWA WA GOUT

Gout ni aina ya ugonjwa wa arthrits ambao anaambatana na maumivu makali kwenye joint, kuvimba kutokana na mrundikano wa uric asidi ambayo hujikusanya na kufanya kama jiwe gumu kwenye joint. Hapo zamani gout ulijulikana kama ugonjwa wa wafalme (a disease of Kings) kutokana na unywaji wao wa pombe na vyakula vya kukidhi raha zao. Mfalme Henry wa VIII wa Uingereza ni mmoja ya wafalme waliougua ugonjwa huu. Alexander the great, Christopher columbus, Sir Isaack newton ni baadhi ya watu maarufu ambao waliugua ugonjwa wa Gout.kibaya zaidi ni kwamba namba ya watu wanaougua ugonjwa huu kwa sasa inaongeza taratibu haijalishi unatoka familia ya kitajiri ama laa.

GOUT NI NINI HASA
Huu ndio ugonjwa wa joints ambao huwashambulia sana na kuwapa maumivu makali wanaume. Wanawake pia huweza kuathirika na ugonjwa huu hasa baada ya kukoma hedhi. Ugonjwa huu huleta maumivu makali ya ghafla, hasa kwenye sehemu linapoanzia dole gumba la mguu. Dalili za ugonjwa huanza kuonekana pale uric acid, tindikali ambayo huzalishwa na mwili katika ufanyaji kazi wake (ambayo haina manufaa kwa mwili) hubakia katika viungo vya mwili na katika majimaji ya mwili. Uric acid iliyoganda (tophi) huweza kujikusanya na kubaki chini ya ngozi inayozunguka joints, huweza pia kujikusanya ndani ya figo na kusababisha kidney stones (namna ya kokoto ndogo ndani ya figo)
Gout inaweza kusababisha madhara ya kudumu kwenye maungio ya mifupa na figo. Endapo hatua za kuutibu ugonjwa huu hazitachukuliwa kwa muda mrefu (miaka 10 au zaidi), madhara ya kudumu humtokea mgonjwa


Chanzo Cha Gout Ni Nini?


 Gout kutokea kimsingi pale tindikali aina ya uric (uric acid) inapozidi kiwango katika mwili wa binadamu hali ambayo kiutaalamu huitwa hyperuricemia. Tindikali hii ni matokeo ya kuvunjwavunjwa na mwili kwa aina fulani za chakula kama nyama, nyama ya kuku na chakula cha baharini. Tindikali hii kwa kawaida huchanganyika na damu na mwisho hutolewa nje ya mwili pamoja na mkojo kupitia figo. Tindikali hii ikitengenezwa kwa wingi mno au isipotolewa nje ya mwili kwa kiwango kinachosatahili, ile inayobakia huganda na kukaa kwenye maeneo ya joints na kusababisha maumivu kwenye joints hizo na maeneo yaliyo karibu. Kuna mazingira ambayo hupelekea hali hii ya uzidifu wa tindikali ya uric katika mwili na mwishowe gout kutokea nayo ni:
·         Jinsia: Wanaume huzalisha tindikali ya uric kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko wanawake, viwango vya uzalishaji kwa wanawake vikikaribia vile vya wanaume pale tu wanapokoma hedhi.
·         Urithi: Kuzaliwa kwenye familia yenye historia ya gout kunakufanya uwe kwenye hatari kubwa zaidi ya kuupata ugonjwa huu.
·         Mtindo wa maisha: Unywaji wa pombe huzuia utolewaji wa uric acid   nje ya mwili na ulaji wa chakula chenye purine kwa wing  husababisha kiwango cha tindikali ya uric kuwa kikubwa mwilini.
·         Madini ya lead: Kuwa karibu na madini haya kwa muda mrefu  kumeonyesha kuhusika na aina fulani za gout.
·         Madawa: Baadhi a madawa yameonekana kuongeza kiwango cha uric acid mwilini.
·         Uzito kupita kiasi: Unene umedhihirika kuongeza hatari ya kupatwa na gout.
·         Matatizo ya kiafya: Kama figo hazifanyi kazi vizuri kiwango cha  uric acid mwilini kitapanda. Matatizo mengine ya kiafya  yanayochangia ni high blood pressure (hypertension), kisukari na  hypothyroidism.

DALILI ZA GOUT
Ugonjwa wa gout huanza ghafla na mara nyingi katikati ya  usiku. Ugonjwa huanza kwa kuleta maumivu makali kwenye maungio ya mifupa na mara nyingine kuambatana na uvimbe. Gout mara nyingi hushambulia maungio makubwa ya dole gumba la mguu lakini pia huweza kushambulia maungio ya mikono, ankles, viwiko vya mikono na vidole.

 TIBA YA GOUT

Matatizo yaliyo mengi ya gout huondolewa kwa kutumia dawa. Nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs), colchicine au corticosteroids hutumika kuondoa maumivu kwenye eneo lililoathirika na gout, japo mgonjwa atakuwa mteja wa dawa hizi mika yote.
Upande wa pili ni dawa za asili zinafanya vizuri sana katika kutibu tatizo hili bila kukuletea madhara kwenye mwili. Ila hakikisha tu unatafuta kituo sahihi chenye dawa zenye ubora mkubwa. Mtindo wa maisha unaweza kusaidia katika kupunguza makali ya ugonjwa huu au kuzuia usikupate. Yafaa kufanya yafuatayo:
– Kunywa maji mengi, lita 2-4 kwa siku
– Kutokunywa pombe
– Kuweka uzito wa mwili kwenye kiwango kinachofaa
– Kupata mlo uliokamilika (balanced diet)
– Kutotumia vyakula vyenye purines kwa wingi ama nyama nyekundu (vinavyozalisha uric acid kwa wingi). Vyakula vya kula kwa kiasi kidogo ni maharage na njegele zilizokaushwa, nyama pori, uyoga na maini.
Kama tayari unaumwa basi usipate hofu unaweza kufika ofsini kwetu ukapata huduma kwa kutumia vidonge vya mimea na ushauri pia namna ya kutibu tatizo hili.  

Gharama za dawa na virutubisho ni Tsh 150,000/=  Pekee.

Bofya hapa Kuchati na Daktari kwa whatsapp

Upate maelekezo ya kufika ofisini Ambapo utapata huduma ya dawa za mimea zisizo na kemikali .
kama upo mkoani basi usihofu maana utatumiwa dawa baada ya kufanya malipo.

Usiache kupitia makala inayofuata: Mgonjwa wa gout anaweza kuwa na mawe kwenye figo, fahamu zaidi


Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUGUNDUA NA KUTHIBITI VIDONDA VYA TUMBO( PEPTIC ULCER)

MAELEZO YA UTANGULIZI KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO Tunashukuru kwa kuendelea kufatilia makala zetu, kwa maoni na ushauri ama uhitaji wa kufika ofisini basi endelea kutuandikia kwa namba  0714206306 .  Kupata ufahamu mpana juu ya vidonda vya tumbo ni vema kuelewa kwanza mfumo unaohusika na tumbo ambao ni umen'genyaji wa chakula. Sehemu kuu zinazohusika katika umen'genyaji huo ni kinywa,umio ambayo ni misuli wenye urefu wa sentimeta 23 ambao huunganisha koromeo na tumbo'esophagus',mfuko wa nyongo na sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo'duodenum',utumbo mdogo,kongosho,utumbo mpana na sehemu ya mwish oni ya utumbo'rectum'. Mfumo wa mmen'genyo wa chakula hasa kuta za umio,tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na tindikali inayotumika kumen'genya chakula inaposhambulia kuta hizo, hii ndiyo vidonda vya tumbo'Peptic Ulcers',vidonda vya mfumo wa umen'genyaji chakula vikiwa kwenye tumbo ni 'Gastric Ulcer'vikiwa kati...

Kisonono ni nini ?, je kuna Tiba ya kisonono ?

Nini maana ya kisonono, je naweza kupata tiba sahihi ya kisonono?  Soma makala jii upate kujifunza na kupata ueewa juu ya tatizo la kisonono ambalo limeathiri watu wengi sana kwa sasa hasa vijana wa kiume. Kisonono au kwa lugha ya kitaalamu Gonorrhea ni moja ya ugonjwa wa ngono ambao huambukizwa baada ya mtu mmoja mwenye ugonjwa kukutana kimwili mtu mwingine mzima. Kisonono mara nyingi husababisha maumivu makali na dalili zingine mbaya kwenye via vya uzazi na sehemu zingine kama, sehemu ya haja kubwa, macho na pia maumivu ya viungo. Ugonjwa huu wa kisonono huweza kuwapata watu wa jinsia zote wanawake kwa wanaume huku tafiti zikionesha kwamba wanaume ndio wanaoongoza kuambukizwa kuliko wanawake. Nnini husababisha kinonono au Gonorrhea?? Ugonjwa huu wakuambukizwa kwa njia ya ngono husababishwa na bacteria wanaoitwa Neisseria gonorrhoeae. Na hivo pale watu wanapokutana kingono bacteria hawa huweza kusambaa kwenda kwa mtu mwingine kutokana na msuguano wa viungo laini vya uza...

UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE

 FAHAMU TATIZO LA UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE (OVARIAN CYST ) Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovary) hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana kama ovarian cyst. Uvimbe huu unaweza kumtokea mwanamke wa umri wowote ingawa mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito. MAYAI YA MWANAMKE  Kwa kawaida mwanamke anakuwa na mayai mawili katika mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto. Mayai haya hupatikana pembezoni mwa mfuko wa uzazi (uterus). Mayai haya huanza kuzalisha mayai ya uzazi yanayojulikana kama ovum  ambapo mayai hayo ya uzazi hukuwa ndani ya mayai ya mwanamke (ovary) kwa kuchochewa na baadhi ya homoni.  Katikati ya mwezi, siku ya kumi na nne, saa 24-36 baada ya kiwango cha kichocheo aina ya Luteinizing Hormone kuwa juu, mayai ya uzazi hutolewa k...