Skip to main content

KUVIMBA KWA TEZI DUME (PROSTATE GLAND) NA TIBA

Kwanini Tezi Dume inavimba, Je Kuna Tiba ya Tezi Dume?

Ili kujibu maswali haya na mengine mengi tuanze kwanza kwa kufahamu nini maana ya tezi dume.

Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra). 
         Tezi hii ina sifa zifuatazo.
                 ·     Ina umbo kama yai (oval shape)
          · Ina ukubwa wenye vipimo hivi, upana 4cm na unene 3cm ingawaje hivi vipimo      vinatofautiana kwa kila mwanaume.
          ·   Tezi hii hua yenye ukubwa wa kawaida lakini huongezeka ukubwa kadri ya umri unavoongezeka.
    ·   Tezi hii hutengeneza majimaji yenye rutuba ya mbegu za kiume(shahawa) yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ngono. Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa (semen). Aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya fallopian tayari kwa utungisho na yai la kike. Vilevile husaidia kupunguza hali ya kitindikali (acidic condition)  iliyopo katika uke, ambayo kama isiporekebishwa, huweza kuua mbegu nyingi za kiume na kufanya utungisho kuwa wa shida.


     


                                       KUVIMBA TEZI DUME (BPH)

               



Kwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la kawaida pia kwa tezi dume kuongezeka ukubwa na kuvimba. Hali hii kitabibu huitwa Benign Prostate Hyperplasia au wengine hupenda kutumia maneno Benign Prostate Hypertrophy kwa kifupi BPH. Hivyo tezi inaweza ikawa kubwa sana lakini haina dalili hii ni kutokana na sehemu gani ya tezi iliyovimba au kuongezeka. Tezi inapoonesha dalili jua tatizo hilo ni sugu na liko ktk hali mbaya. Kwenye makala hii tutautumia sana ufupisho huu wa BPH ili kurahisisha kuelewa.


Ukuaji wa tezi dume hupitia hatua kuu mbili. Hatua ya kwanza hutokea kipindi cha balehe wakati tezi dume linapoongezeka ukubwa na kuwa mara mbili ya lilivyokuwa hapo awali. Baada ya hapo ukuaji husimama kwa muda mpaka kijana anapofikisha miaka 25 hadi 30 ndipo hatua ya pili ya ukuaji huanza tena. Ukuaji huendelea kwa viwango na kasi tofauti kati ya mtu na mtu na hatimaye kusababisha BPH katika umri wa utu uzima.


Wakati tezi dume linapokua na kutanuka, utando wa tishu unaozulizunguka hutanuka pia. Hata hivyo ingawa tezi dume huendelea kukua, hufikia wakati utando wake huacha kutanuka na kufanya tezi dume kubana mrija wa kutolea mkojo kutoka kwenye kibofu. Hali hii husababisha kibofu cha mkojo kuwa na ngozi ngumu. Hali hii hufanya kibofu cha mkojo kuhisi kutaka kutoa mkojo nje hata kama kiasi cha mkojo ndani yake ni kidogo sana. Hufikia wakati, kibofu huwa dhaifu na kupoteza uwezo wake wa kuhisi kutoa mkojo na hivyo kufanya mtu anapokojoa kushindwa kutoa mkojo wote na badala yake hubakiza kiasi fulani cha mkojo kwenye kibofu.


kuvimba kwa tezi dume husababishwa na nini?

Chanzo halisi cha BPH au vihatarishi vyake (risk factors) havijulikani kwa uhakika. Kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa kuwa BPH hutokea kwa wanaume watu wazima na wazee tu. Aidha imewahi kuonekana huko nyuma kuwa PBH haitokei kwa wanaume ambao wamewahi kufanyiwa operesheni ya kuondoa korodani au wale ambao walizaliwa bila korodani. Hali imepelekea baadhi ya watafiti kuamini kuwa BPH ina uhusiano mkubwa na umri wa mtu pamoja na uwepo wa korodani.


Dhana (theories) kadhaa zinazojaribu kuelezea chanzo cha BPH. Dhana hizo ni pamoja na



Uhusiano kati ya BPH na homoni ya estrogen: Wanaume huzalisha testosterone, homoni ya muhimu sana katika mwili wa mwanaume. Hali kadhalika huzalisha pia estrogen ambayo ni homoni ya kike kwa kiwango kidogo sana. Kadiri jinsi mtu anavyozeeka, ndivyo uzalishaji wa testosterone unavyokuwa mdogo na kufanya kiwango chake katika damu kupungua kulinganisha na kiwango cha estrogen ambacho huongezeka kwa kiasi fulani. Pamoja na kazi nyingine, estrogen pia huchochea ukuaji wa chembe hai za mwili. Tafiti zilizofanywa kwa wanyama zimeonesha kuwa BPH hutokea kwa sababu kiwango kikubwa cha estrogen katika damu huchochea ukuaji wa seli za tezi dume na hivyo kufanya tezi dume kuvimba.




Uhusiano kati ya BPH na Dihydrotestosterone (DHT): DHT ni kiasili kinachozalishwa kutokana na testosterone kwenye tezi dume, ambacho husaidia kuthibiti ukuaji wa tezi dume. Ingawa wanyama wengi hupoteza uwezo wa kuzalisha DHT wanapofikia umri wa uzee, baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa, kwa binadamu, hata kama kiwango cha testosterone kitapungua sana katika




damu, wanaume watu wazima bado wana uwezo wa kuzalisha kiasili hiki cha DHT katika tezi dume zao. Uzalishaji huu wa DHT huchochea kwa kiasi kikubwa ukuaji wa seli za tezi dume na kusababisha BPH. Wanasayansi wamegundua kuwa wanaume watu wazima wenye.

Kiwango kidogo cha DHT hawapati BPH. Uhusiano kati ya BPH na maelekezo ya seli.

Dhana nyingine inasema kwamba baadhi ya seli kutoka katika sehemu fulani ya matezi yanayohusika na ukuaji mwilini hupewa maelekezo wakati mtu anapokuwa bado mdogo. Seli hizi hutunza maelekezo hayo na baada ya miaka kadhaa maelekezo haya huanzwa kutekelezwa na seli za matezi mengine. Mojawapo ya melekezo hayo ni kuchochea ukuaji wa tezi dume na kusababisha BPH.


Dalili za kuvimba kwa tezi dume


1. Kukojoa mara kwa mara

2. Kubakiza mkojo kwenye kibofu

3. Kukujoa sana usiku

4. Maumivu wakati wa kukojoa


6. UTI ya mara kwa mara

7. Mawe kwenye kibofu kutokana na mrundikano wa mkojo.

8. Figo kujaa maji. Hii sababu mkojo huo unarudi nyuma kuelekea figo (hydronephrosis)

9. Kupoteza fahamu(uremia)


Madhara ya kuvimba kwa tezi dume.


BPH kama ilivyo saratani ya tezi dume, inaweza kumletea mgonjwa madhara (complications) kadhaa. Madhara hayo ni pamoja na

·         Mkojo kushindwa kutoka (retention of urine)
·         Mgandamizo kwenye kibofu cha mkojo
·         Vijiwe kwenye kibofu cha mkojo
·         Uambukizi katika njia ya mkojo (UTI)
·         Madhara katika figo au kibofu
·         Shinikizo la damu kupanda
·         Kushindwa kutoa shahawa kwenye uume (retrograde ejaculation)
·         Nimonia (Pneumonia)
·         Damu kuganda


Baada ya mgonjwa kujihisi dalili zilizotajwa hapo juu, daktari atamfanyia uchunguzi wa mwili kabla ya kumfanyia vipimo zaidi. Vipimo vyaweza kutofautiana kati ya mgonjwa namgonjwa, lakini baadhi ya vipimo ni pamoja na




1.KUCHUNGUZA TEZI DUME KUPITIA NJIA YA HAJA KUBWA AU DIGITAL        RECTAL EXAMINATION (DRE):

        

Hiki ni kipimo cha kwanza kabisa ambacho mgonjwa hufanyiwa na daktari wake. Ni kipimo kinachoweza kumpa daktari picha ya tatizo na kufahamu kuhusu ukubwa na hali ya tezi dume. Daktari akiwa amevaa glovu huingiza kidole chake cha shahada katika njia ya haja kubwa au puru (rectum) ya mgonjwa kasha kuzungusha zungusha ili kufahamu kama tezi limevimba ama la na pia hali yake kama ni gumu kuliko kawaida ama lina utando na nyama laini.
2.KIPIMO CHA DAMU CHA PROSTATE-SPECIFIC ANTIGEN (PSA):
PSA husaidia kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH. PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume na kiwango chake huongezeka iwapo kuna saratani ya tezi dume.



3.UTRASOUND YA PURU (RECTAL ULTRASOUND):

Kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa saratani ya tezi dume badala ya BPH. Utrasound ya puru pamoja na kuonesha taswira ya tezi dume ilivyo, pia humuwezesha daktari kuchukua kinyama (biopsy) kwenye tezi dume kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kutofautisha kati ya saratani na BPH.



4.KIWANGO CHA UTOKAJI WA MKOJO (URINE FLOW STUDY): Ni kipimo kinachotumika kufahamu kasi ya utokaji wa mkojo. Mkojo unaotoka kwa kasi na kiwango kidogo huashiria kuwepo kwa BPH.

5. KIPIMO CHA KUCHUNGUZA KIBOFU CHA MKOJO (CYSTOSCOPY): Kipimo hiki husaidia kuweza kufahamu ukubwa wa tezi, sehemu tezi lilipobana njia ya mkojo na kiwango cha kubana huko. Aidha huwezesha pia kutambua hali ya kibofu cha mkojo ikoje.

MATIBABU YA TEZI DUME




Matibabu ya BPH yameganyika katika sehemu mbili, yale yanayofanywa kwa kutumia dawa na yale yanayofanywa kwa kutumia upasuaji mdogo. Aidha matibabu hufanywa kwa watu wenye BPH kubwa zaidi na dalili zinazowaletea usumbufu na kuathiri maisha yao, wakati wale wenye dalili ndogo ndogo hawalazimiki sana kuhitaji matibabu.




MATIBABU KWA NJIA YA DAWA

Dawa hizi hutumika kwa lengo la kulifanya tezi dume kusinyaa na kupungua ukubwa wake.




MATIBABU KWA NJIA YA UPASUAJI)



·         Upasuaji mdogo husaidia kuondoa dalili za BPH na hufanyika pale ambapo matibabu kwa njia ya dawa yameshindwa kuonesha mafanikio yeyote. Njia hizo niTiba ya kutumia mawimbi ya joto (Transurethral microwave procedures, TUMT): Tiba hii hutumia kifaa kinachotoa mawimbi ya joto (microwave) yanayochoma na kuharibu tishu zilizovimba za tezi dume.
·         Matibabu huchukua chini ya saa moja na yanaweza kufanyika bila mgonjwa kuhitaji kulazwa.Tiba ya kutumia sindano maalum (Transurethral needle ablation, TUNA): Njia hii hutumia visindano vidogo ambavyo huunganiswa kwenye chombo chenye kutoa nishati ya joto kuunguza tishu zilizovimba za tezi dume.
·         


Tiba ya kutumia joto la maji (Water-induced thermotherapy): Tiba hii hutumia maji ya moto yaliyochemshwa kwa kifaa maalum kuunguza na kupunguza tishu zilizovimba za tezi dume.


Madaktari wengi hushauri kuondolewa kabisa kwa tezi dume iwapo itathibitika kuwa mgonjwa ana BPH. Zipo njia nyingi za upasuaji wa BPH, nazo ni pamoja na upasuaji kwa kupitia kwenye mrija wa mkojo (Transurethral surgery, TURP), upasuaji mkubwa wa wazi (Open surgery), upasuaji wa kutumia nishati kuondoa tishu za tezi dume Laser surgery), na upasuaji wa kutumia joto la fibreoptic probe kuchoma tishu za tezi dume (Interstitial laser coagulation).


MADHARA YA TIBA HIZI

1. Kukosa uwezo wa kufikia kishindo yani hutoi shahawa(RETROGRADE EJACULATION) wazee wengi hulalamika sana baada ya hizi operation hivyo ushauri nasaha lazima utolewe ili mgonjwa ajue nini madhara yake kabla ya operation.

2. Kuziba kwa njia ya mkojo kutoka na kuumia kwa njia hizo wakati wa kitendo hicho. Panapokua panapona hilo kovu linaziba njia ya mkojo.

3. Operation kubwa ya kuondoa tezi hio hufanyika kwa kufungua kibofu cha mkojo na kutoa hio tezi. Madhara ni mengi sana kuhusu njia hii.

4. Shida ya kuthibiti mkojo usitoke ovyo (Incontinence): Ni kawaida kwa mgonjwa kushindwa kuthibiti kutoka kwa mkojo katika siku za mwanzo baada ya operesheni. Hata hivyo hali hii hujirekebisha baada ya siku kadhaa kupita.Kutokwa na damu: Katika siku za wali mara baada ya TURP, kidonda kwenye tezi dume kinaweza kuvuja damu ambayo itaonekana katika mkojo. 


5. Wanaume kuwa  wagumba yaani wasioweza kupata watoto. Kwa kawaida, wakati wa tendo la ngono, mbegu za kiume kutoka kwenye korodani huingia kwenye urethra

karibu na kijitundu cha kibofu cha mkojo. Wakati wa tendo la ngono, misuli maalum hufunga kijitundu hicho ili kuzuia mbegu zisiingie kwenye kibofu badala yake zielekee kwenye urethra ya katika uume. Hata hivyo, upasuajiwa BPH huondoa misuli hiyo na kufanya mbegu kuingia kwenye kibofu cha mkojo badala ya kuendelea kwenye urethra ya uume. Shahawa hizo hatimaye hutolewa nje ya kibofu pamoja na mkojo.Kufika kilele UTAFITI UNASEMA NINI KUHUSU KUKUA KWA TEZI NA MATIBABU YAKE.



1. LYCOPENE.

-Hivi ni virutunisho vinavyotokana na nyanya. Lycopene ina uwezo wa kupenya kwenye tezi dume na kuondoa tatizo lolote na kuzuia kabisa kukua kwa tezi dume. Pia ina uwezo mkubwa wa kuzuia kansa ya tezi dume. Hivyo tunashauri kila mtu mwenye umri wa miaka 30 atumie virutubisho hivi ili kujilinda na tezi kukua. Utumiapo lycopene iliyotengenezwa kwa kiwango kingi(concentrated) kuna uwezekano mkubwa wa kutopata kabisa tezi hii dume hata kama kwenye ukoo wenu wote walipata tezi hii. Kama utahitaji hii bidhaa bora kabisa imetengezwa katika mfumo wa vidonge ni asili haina madhara kwani haina chemical imetokana na NYANYA. Tumia lycopine at least kopo mbili kwa mwaka lenye virutubisho 60 kwa mwezi mmoja ili kujiepusha kabisa na tezi tume na kansa ya tezi dume.


~Zinc ni kiondoa sumu kikubwa sana yani POWERFUL ANT OXIDANT hivyo utafiti unaonesha utumiapo virutubisho hivi saratani ya tezi dume na kuvimba kwa tezi utaviepuka kwa asilimia 80 zaidi. 

3. PROSTACARE

Dawa hii ni ya kiasili imetengenezwa kwa kutumia viambata vifuatavyo


Extractum of Radix Rehmanniae, Rhizoma Anemarrhenae, Cortex Phellodendri Chinsis, Herba Ecliptae, Fructus Ligustri Lucidi, Harba Plantaginis, Radix Paeoniae Rubra Ambavyop kwa pamoja husaidia 

·         Kuboresha mzunguko wa damu ndani ya tezi dume
·         Kuzuia kuzaliana kwa wadudu wabaya ndani ya tezi dume
·         Kuondoa dalili za matatizo ya tezi dume


Inafaa kwa mwanamme mwenye tatizo lolote la tezi dume na inawafaa Wanaume wenye umri unaozidi miaka 40 kwaajili ya kujikinga na tezi dume

Jaribu prostate care package kutoka kwetu kwa Sh 250,000/=



J

 Tutakupatia virutubisho tulivyoeleza hapo juu ili uweze kutibu tatizo lako la tezi dume na  kuilinda familia yako kwa kurudisha tendo la unyumba. Bila kusahau kingine kina ongeza nguvu,shauku ya kufanya na kurudia tendo la ndoa.

SULUHISHO LAKO LIPO DHIDI YA TEZI DUME, USIKUBALI UVIMBE KUFKIA HATUA MBAYA NA KUTENGENEZA SARATANI. CHUKUA HATUA , LINDA AFYA YAKO KABLA HUJAUGUA .

VIRUTUBISHO NA DAWA ZOTE HIZI ZA ASILI ZINAPATIKANA OFSINI KWETU HAPA DAR, MWEMBECHAI , KAMA UPO MKOANI BASI USIHOFU MAANA UTATUMIWA DAWA BAADA YA KUFANYA MALIPO.

Bofya hapa Kuchati na Daktari kwenye Whatsapp

ANGALIZO


kumbuka afya yako siyo dhamana ya mtu, afya yako ina thamani kubwa kuliko pesa unayotoa  hivo usiangalie gharama za dawa na kuamua kwenda mitaani kununua dawa za bei nafuu halafu ukaendelea kuwa muhanga na kuteseka na matatizo yako. tunakuhakikishia kwamba lazima utapona ukitumia dawa hizi pasipo na mashaka kabisa.

Soma makala inayofuatia Sababu za Misuli ya Uume Kulegea


Comments

Popular posts from this blog

MADHARA YA PUNYETO NA TIBA YAKE

MAELEZO  YA AWALI KUHUSU TATIZO LA UPIGAJI PUNYETO Watu wengi sana wanataka kufahamu jinsi gani wafanye ili kuachana na kitendo cha upigaji punyeto. Punyeto ni tendo la mtu la kuamsha hisia za mapenzi au msisimko ambao unampelekea mtu huyu kufikia kilele cha kujimalizia tamaa zake! Bila kufanya tendo halisi, hutumia fikra zake katika picha za zinazoitwa za ngono au picha zozote zinazoweza kulifanikisha tendo hilo, movie n.k. Kilele cha yote anafikia mahali anajimalzia tamaa zake mwenyewe!. Nimekuwa nikiona baadhi ya watu wanaosema wameelimika wakipingana wao kwa wao katika suala zima la kupiga punyeto! Wako wanaotetea kutokana na elimu yao na wanasema kwa ujasiri mkubwa kwamba "kupiga punyeto ni sehemu ya maisha ya mwanadamu" Ina maana katika maisha ya mwanadamu upigaji punyeto inaelezwa ni kama tendo la lazima mpaka inafikia mahali wanasema ni sehemu ya maisha (Maisha) ya mwanadamu. Nimekuwa nikipata kesi nyingi sana juu ya madhara yatokanayo na punyeto. Aslimia 60...

Kisonono ni nini ?, je kuna Tiba ya kisonono ?

Nini maana ya kisonono, je naweza kupata tiba sahihi ya kisonono?  Soma makala jii upate kujifunza na kupata ueewa juu ya tatizo la kisonono ambalo limeathiri watu wengi sana kwa sasa hasa vijana wa kiume. Kisonono au kwa lugha ya kitaalamu Gonorrhea ni moja ya ugonjwa wa ngono ambao huambukizwa baada ya mtu mmoja mwenye ugonjwa kukutana kimwili mtu mwingine mzima. Kisonono mara nyingi husababisha maumivu makali na dalili zingine mbaya kwenye via vya uzazi na sehemu zingine kama, sehemu ya haja kubwa, macho na pia maumivu ya viungo. Ugonjwa huu wa kisonono huweza kuwapata watu wa jinsia zote wanawake kwa wanaume huku tafiti zikionesha kwamba wanaume ndio wanaoongoza kuambukizwa kuliko wanawake. Nnini husababisha kinonono au Gonorrhea?? Ugonjwa huu wakuambukizwa kwa njia ya ngono husababishwa na bacteria wanaoitwa Neisseria gonorrhoeae. Na hivo pale watu wanapokutana kingono bacteria hawa huweza kusambaa kwenda kwa mtu mwingine kutokana na msuguano wa viungo laini vya uza...

JINSI YA KUGUNDUA NA KUTHIBITI VIDONDA VYA TUMBO( PEPTIC ULCER)

MAELEZO YA UTANGULIZI KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO Tunashukuru kwa kuendelea kufatilia makala zetu, kwa maoni na ushauri ama uhitaji wa kufika ofisini basi endelea kutuandikia kwa namba  0714206306 .  Kupata ufahamu mpana juu ya vidonda vya tumbo ni vema kuelewa kwanza mfumo unaohusika na tumbo ambao ni umen'genyaji wa chakula. Sehemu kuu zinazohusika katika umen'genyaji huo ni kinywa,umio ambayo ni misuli wenye urefu wa sentimeta 23 ambao huunganisha koromeo na tumbo'esophagus',mfuko wa nyongo na sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo'duodenum',utumbo mdogo,kongosho,utumbo mpana na sehemu ya mwish oni ya utumbo'rectum'. Mfumo wa mmen'genyo wa chakula hasa kuta za umio,tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na tindikali inayotumika kumen'genya chakula inaposhambulia kuta hizo, hii ndiyo vidonda vya tumbo'Peptic Ulcers',vidonda vya mfumo wa umen'genyaji chakula vikiwa kwenye tumbo ni 'Gastric Ulcer'vikiwa kati...