Skip to main content

Posts

Showing posts from October, 2016

KUKOSA CHOO KWA MDA MREFU AMA KUPATA CHOO KIGUMU ( CONSTIPATION) NA MADHARA YAKE KIAFYA

Maelezo ya utangulizi Mwili wako ni mfano wa silinda kubwa ambayo ndani yake kuna tube inayoanzia mdomoni mpaka chini   kwenye puru pale unakotolea uchafu, silinda hii ndio mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Hivyo mfumo wa chakula upo ndani ya mwili na umesheheni kemikali mbalimbali ambazo husaidia usagaji na uchkataji wa chakula ili kupata virutubisho vinavyohitajika na mwili. Mfumo wa chakula unachangia karibu asilimia 80 ya utimamu wa afya yako . usagaji   wa chakula huanzia mdomoni pale unapotafuna chakula na kikachanganyika na mate. Usagaji na uchakataji wa chakula huishia kwenye utumbo mpana baada ya mwili kufyonza virutubisho muhimu na maji na kuacha takataka ambazo hazitumiki, virutubusho ambavyo vinavyonzwa ili kutoa energy ambazo ndio tunaita kalori. Kalori kiasi gani unakula na pia ubora na chanzo cha kalori ama chakula unachokula ni sababu za msingi ambazo zinaathiri afya yako aidha chanya au hasi. Sababu nyingine ambayo inaleta matokeo kwenye  afya ...

UZITO MKUBWA NA KITAMBI VINABABISHA KARIBU WATU NUSU MILIONI KUUGUA SARATANI DUNIANI KOTE

MAELEZO YA UTANGULIZI KUHUSU TATIZO LA UZITO MKUBWA NA KITAMBI Karibu 30% ya watu wote duniani wana uzito uliopitiliza na vitambi na hii imepelekea matokeo makubwa katika ugonjwa wa saratani ama kansa. Repoti  moja inasema kwamba inakadiriwa kuwa uzito mkubwa na kitambi vinachangia karibu watu 500,000 wenye saratani kila mwaka. Theluthi mbili ya kesi hizi za saratani zinatokea Ulaya na Amerika ya kaskazini. Wanawake wakiwa kwenye hatari kubwa zaidi ukilinganisha na wanaume, aina hizi za saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya utumbo mpana, na saratani ya matiti. Kutokana na tafiti hizi inaonesha kwamba ifikapo mwaka 2030 basi karibu nusu ya watu wazima duniani watakuwa na uzito mkubwa na vitambi. Kansa au saratani siyo tatizo moja tu linaloletekezwa na uzito mkubwa na vitambi bali kuna magonjwa mengine mengi yanayoambatana ikiwemo, kisukari aina ya 2, matatizo ya kupata usingizi na kukoroma usingizini, uvimbe kwenye kizazi, ngiri, Matatizo katika njia ya mkojo, Stroke, Up...

MATUMIZI SAHIHI YA MAJI KWA AFYA YA MWILI WAKO.

“KUNYWA MAJI MENGI” ni msisitizo ambao umekuwa ukipewa mara nyingi labda na mama nyumbani, ama na Daktari wako au rafiki wako wa karibu, lakini ambacho hukuambiwa ni kwanini maji ni muhimu kwa afya yako na pia kiasi cha maji unachotakiwa kunywa na ubora wa maji vyote ni muhimu kufahamu. Najua swali la watu wengi ni kwamba Je ni kiasi gani cha maji unachotakiwa kunywa kila siku?? . Maji ni muhimu sana kwa afy zetu ni dhahiri kwamba unaweza kuishi bila chakula kwa siku nyingi lakini bila maji utaishi mud mfupi sana. Miili yetu kiujumla imetengenezwa kwa maji ambayo 1.       Ni muhimu katika kurahisisha umeng’enyaji wa chakula, uvyonzwaji wa virutubisho na pia utoaji wa takamwili. 2.       Kusaidia usafirishaji wa vitu mbalimbali kwenye mwili. 3.       Kurekebisha joto la mwili 4.       Kulainisha joint ili kupunguza msuguano wa mifupa na 5.       Kusafi...

MAUMIVU YA TUMBO KIPINDI CHA HEDHI

Kuumwa tumbo wakati wa hedhi Tumbo la hedhi au maumivu wakati wa hedhi (period pains) au kitaalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo. Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani huku baadhi ya wanawake wakipata maumivu makali sana. Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi huanza pale mayai yanapotoka katika mirija (fallopian tubes) na kuteremka chini ya mirija hiyo wakati wa Ovulation. Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili.  Aina ya kwanza au (Primary Dysmenorrhea;  Ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Maumivu hayo huanza siku moja au mbili kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne. Aina ya pili au (Secondary Dysmenorrhea)  Ni yale maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba kama vile matatizo kat...

SULUHISHO LA NGUVU ZA KIUME

Kwanini tatizo la nguvu za kiume na unawezaje kuepuka na kutibu. Tatizo la nguvu za kiume sasa limepata suluhisho kupitia mimea ya Fructus Lycii kutoka Thailand. jipatie bidhaa hizi za asili na uepuke matumizi ya kemikali Mabadiliko ya mitindo ya maisha kama ulaji mbaya na matumizi ya kemikali yamesababisha kundi kubwa la vijana kuathirika na kutokuwa na uwezo mzuri wa nguvu za kiume. kwa kulitambua hilo basi tumewaletea  vidone vya Mimea aina ya Fructus Lycii  ni mimea maarufu sana nchini thailand,china,india,vietnam kwani hadi sasa nchi kama thailand ndiyo inayo ongoza kwa kulima aina hii ya miti ambayo imekuwa ikitumika kurudisha kabisa nguvu na kutibu hali ya kutopata mtoto kwa sababu ya mbegu chache. Mimea hii inatibu matatizo ya kushindwa kufanya tendo la ndoa kwa wanaume,kukosa shauku,kukosa mtoto pia na magonjwa yote ya njia ya mkojo yanayo ambatana na maumivu wakati wa kukojoa. Nchi hizi kama Thailand na China  hadi sasa zimetengeneza kirutubisho amb...

TATIZO LA MAWE KWENYE FIGO (KIDNEY STONES)

MAELEZO YA UTANGULIZI Figo ni kiungo muhimu katikamwili wa binadamu, hufanya kazi ya kuchuja damu huku ikiondoa sumu zote za mwili ,figo hufanya kazi ya kurekebisha kiasi cha maji mwilini (electrolyte level). Kabla damu haijapita katika figo, huwa imebeba maji na taka taka nyingi sana (urea) ,lakini inapopita katika figo huchujwa na vitu muhimu hurudishwa katika mzunguko wa damu lakini,masalia mengine ambayo hayafai tena katika mwili ikiwani pamoja na kiwango cha maji kilichozidi hupitishwa kwenye mirija miwili (ureters)kuelekea kwenye kibofu ( urinary bladder) nakisha  kutolewa nje ya mwili kupitia njia ya mkojo (urethra) Mkusanyiko wa kemikali hizi  (chemical crystals), wakati mwingine hugandamana na kutengeneza chembechembe ya vitu kama mchanga,kadri siku zinavyozidi kuendelea ndivyo vinavyozidi kukua hadiwengine hufikia hatua ya kuziba njia ya mkojo katika figo yenyewe (neprone) au kwenye mirija yakupeleka mkojo kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu (ureteter), ha...

UGONJWA WA PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE AU MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI)na jinsi ya kupata tiba sahihi

Maelezo ya awali ya ugonjwa wa PID Habari za siku ndugu zangu ni matumaini yangu mnaendea vizuri. Kutokana na kundi kubwa la wanawake wamekuwa wakiteseka na tatizo hili, bila kupata msaada wa tiba huku wakibaki na madhara makubwa kama ugumba, , basi leo hii napenda nianze na ugonjwa wa PID(PELVIC INFLAMMATORY DISEASE AU MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI ) UGONJWA WA PID NI NINI?? ~ni ugonjwa wa maambukizi unaotokea katika via vya uzazi wa mwanamke ambapo huhusisha maambukizi katika shingo ya kizazi (CERVICITIS),nyama katika mfuko wa uzazi (ENDOMETRITIS) na mirija ya uzazi (SALPINGITIS) VYANZO NA VIHATARISHI VYA KUPATA UGONJWA WA PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE) Vimelea aina ya NEISSERIA GONORHOEAE pamoja na CHLAMYDIA TRACHOMATIS ndio chanzo cha maambukizi ya ugonjwa wa PID ingawaje kuna aina kadhaa za vimelea vinahusishwa kusababisha ugonjwa wa PID hivyo nilivyotaja ndio vinaongoza Kwa umaarufu kusababisha ugonjwa wa PID ~pamoja na vimelea hao kuwa chanzo kikuu cha ugonjwa w...