Skip to main content

TIBA YA KISUKARI NA USHAURI WA KITAALAMU

Kati ya watu watatu basi mmojawapo tayari ana ugonjwa wa kisukari ama atapata ugonjwa huu hivi karibuni: je wewe ni mmojawapo, na hufahamu hili???
Tafiti iliyofanyika mwaka 2015, inasema gharama zinazotumika kwenye kutibu ugonjwa wa kisukari kwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara zinafikia dola bilioni 19.5, hapo utaona jinsi gani tatizo linavoongezeka miaka hadi miaka na kuharibu afya za wapendwa wetu. Sasa leo tutafahamu kisukari ni nini, aina za kisukari, nini chanzo cha kisukari, aina ya vyakula unachotakiwa kula ili kujikinga na tatizo hili na mwisho kama tayari umeugua na unateseka na ugonjwa wa kisukari ufanye nini. Fuatana nami katika Makala hii ukisoma taratibu upate maarifa kwa kina.


What is diabetes?? Kisukari ni nini??
Kisukari ni ugonjwa wa kiutendaji (metabolic disorder) unaopelekea kupanda kwa kiwango cha sukari kwenye damu na mwili kushindwa kustahimili tena ngezeko la sukari.
AINA ZA KISUKARI
Kuna aina kuu 2 za kisukari, aina ya kwanza ambayo kisukari cha utotoni na aina ya pili ya kisukari ambacho ni kisukari cha ukubwani.
1.       KISUKARI CHA UTOTONI
Aina hii ya kisukari huanza pale mtoto anapozaliwa hadi kufkia umri wa miaka 18 au 20, husababishwa na mpambano kati ya kinga ya mwili dhidi ya seli za beta ambazo hutengeneza homoni ya insulin (homoni inayorekebisha kiwango cha sukari kwenye damu), sasa mpambano huu hupelekea kupungua kwa uzalishaji wa insulini ama kukosekana kabisa kwa insulin kwene kongosho, na kwasababu miiili yetu imeubwa kutumia insulini wagonjwa hawa huhitaji kudungwa sindano za insulin kila siku ili kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu.
DALILI ZA KISUKARI CHA UTOTONI( TYPE 1 DIABETES)
1.       Wagonjwa wenye aina hii ya kisukari huwa wamekonda na kudhoofu sana afya zao
2.     Seli za kutengeneza kichocheo cha insulin zinakuwa zimeangamizwa kwa kiasi kikubwa kutokana na mpambano na kinga ya mwili.
3.   Kiwango cha insulin kwenye damu huwa kipo chini sana kutokana na uwezo mdogo wa kongosho kutengeneza insulin.

KISUKARI CHA UKUBWANI (type 2 diabetes)
Aina hii ya kisukari nafahamika sana na imekuwa janga la dunia nzima likiathiri mamia ya watu kila siku. Kinyume na kisukari cha utotoni, aina hii ya kisukari husababishwa na kiasi kikubwa cha insulin kwenye damu. Hivo ukiwa na kisukari cha ukubwani ni kwamba insulin io nyingi kwenye damu na mwili hauwezi kuitumia vizuri hali hii kitalamu ni INSULINI RESISTENSE, ama kongosho yako inatengeneza insulini nyingi lakini imezidiwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu. Kupanda kupita kiasi kwa kiwango cha insulin kwenye damu huweza kuletekeza ama kupelekea matatizo mengine ya kiafya  kama


Hivo magonjwa haya huambatana na tatizo la kisukari na kadri ugonjwa unavokomaa na kufkia hatua mbaya ndivyo magonjwa haya ambatanishi yanavojitokeza Zaidi, najua unaweza kuwa ni muhanga wa ugonjwa huu na umeteseka kwa miaka mingi umetumia madawa mengo bila mafanikio, napenda kukupa tumaini kuwa suluhisho lipo, ni kurekebisha lishe yako tu na kutumia virutubisho muhimu. Ebu futa kwanza elimu za nyuma ulizopewa na hazijakusaidia kisha pokea ushauri mpya ambao umeleta matunda kwa wagonjwa wengie tunaowahudumia kila kukicha.

NINI KINASABABISHA UGONJWA WA KISUKARI CHA UKUBWANI.
Kwanza kabisa ni vyema kufahamu kwamba ugonjwa wa kisukari syo ugonjwa wa kuwa na sukari nyingi hapa, kisukari ni ugonjwa wa homoni, homoni ya insulin, kumbuka kwamba mwili unahitaji kiwango kidogo tu cha glucose kukibadilisha kuwa nishati ili kuendesha shuguli zake, kiwango kingine kinachozidi huwa hakipotei bali huhifadhiwa katika seli za mwili kwenye mfumo wa mafuta, hivo kazi ya insulin ni kusukuma sukari iliyozidi kwenda kwenye seli ili ibadilishwe kuwa mafuta. Sasa inapotokea mwili hausikii uwepo wa insulin kwenye damu yaani insulin inamwagwa lakini kiwango cha sukari kwenye damu kipo pale pale hao ndipo hatari ya kuugua kisukari huanza.

Sasa ni wakati wa kutambua kwamba aina ya chakula unachokula kinachangia kwa kiasi kikubwa kupata magonjwa haya kama kisukari na uzito mkubwa,vyakula kama wanga na sukari hupandisha insulin kwenye damu kwa kasi sana huku vyakula vya protini na mafuta vikithibitika kupandisha insulin kwa kiasi kidogo sana. Kula wanga na sukari nyingi na kufanya mazoezi sana haikusaidii kuepuka magonjwa haya ya kisukari na uzito mkubwa badala yake kula vyakula vya mafuta kama parachichi, samaki, nyama, mayai , nazi na mboga za majani kwa wingi muhimu.

KWANINI KUWA MWEMBAMBA SIYO KIASHIRIA CHA AFYA NJEMA
Tafiti zinasema watu wembamba wapo katika hatari Zaidi ya kufa endapo wakiugua kupita kiasi tofauti na watu wanene, na mara nyingi watu wembanba hupatikana na mrundikano wa mafuta mabaya {trigleycrides} kwenye viungo  kama moyo, ini na figo ambayo huhatarisha ufanyaji kazi wa viungo husika, Kwa bahati mbaya ni vigumu sana kugundua hatua za mwanzo za ugonjwa wa kisukari , hii ni hutokana na kwamba upimaji unaotumika mara nyingi ni ule wa kuangalia kiwango cha sukari kwenye damu ambacho mara zote kinakuwa sawa mpaka pale mgonjwa anapofikia hatua mbaya ya kuanzishiwa dozi ya kudungwa insulin.

JE KISUKARI NI UGONJWA WA KURITHI??
Nafahamu kundi kubwa la watu na wataalamu wa afya wanaimani kubwa kwamba kisukari huambukizwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine, yawezekana mpenzi msomaji wa Makala hii baada ya kushihudia wazazi wako wote wawili wakiugua ugonjwa huu sasa una mashaka kwamba nawe utaugua kisukari, la hasha kama ukirekebisha tu lishe yako basi nakuhakikishia hutaugua ugonjwa wa kisukari,  nadhari hii  ya kurithi haina mashiko kabisa hasa ukizingatia kwamba mpangilio wa gene hubadilika kwa 0.2% kila baada ya miaka elfu 20, sasa iweje kuwepo na kuongezeka kwa magonjwa haya ya kisukari ukilinganisha na enzi za mababu zetu, jibu ni kwamba mazingira na lishe tunazokula ndizo zinabadili namna hizi gene zinavofanya kazi. Namna tunavyokula, kiasi gani miili yetu inashugulishwa, namna tunacontrol msongo wa mawazo, na jinsi mazingira yanayotuzunguka ikiwemo sumu na kemikali zilizopo haya yote yanachangia kwa kiasi kikubwa kukua na kuongezeka kwa janga la kisukari.  


  KWA NINI NAKUSHAURI UPUNGUZE WANGA NA SUKARI KIAFYA?
Unapokuwa umepunguza wanga na sukari au kuacha kabisa ulaji wa vyakula vyenye wanga nyingi, mfano mikate,ugali,wali,tambi nk na hakikisha kitendo hicho kiendane na kuongeza kiwango cha mafuta na vyakula vya protini mwilini mwako katika lishe yako. Hii itaufanya mwili wako kuanza kutumia mafuta kama nishati ya mwili ya kwanza kujitengenezea nishati. Na viungo vya binadamu kama Ini na figo vinapokuwa vinatumia mafuta kuzalisha nishati ya mwili hutenegeneza viini vya nishati viitwavyo KETONE BODIES, ambavyo hivi ndivyo hutumiwa na seli za mwili kujitengenezea nishati kwa wingi.
Hivyo basi unapokuwa unajizuia kutumia vyakula vya wanga mwili wako utatumia karibia siku 5 hadi wiki kuanza kutumia mafuta kama nisharti ya mwili na hicho kitendo tunaita KETO ADAPTATION. Ningependa kusema kwamba KETO ADAPTATION ni ile hali mwili wako kujenga mazoea ya kutumia mafuta kama chanzo cha nishati ya mwili na hapo ndipo utaanza kuona mabadiriko katika mwili wako makubwa sana.
Utakuwa unajisikia mwenye nguvu na unatashangaaa dalili mbalimbali zilizokuwa zinakusumbua zinapotea hii ni kwa sababu ya uwezo mkubwa wa ketone bodies katika mwili wako dhidi ya glucose.
Sote tunajua kwamba ulaji wa vyakula vya wanga kwa wingi na vyakula vyenye sukari nyingi vinaongeza kiwango cha sukari kwenye damu Zaidi ya kiwango ambacho mwili wako unaweza kuhimili.
Mfano, Kiwango cha kawaida cha sukari kinachohitajika mwilini mwako ni kijiko kimoja cha chai, hiki ni kiwango ambacho hakiwezi kukuletea matatizo. Basi kama binadamu anaishi kwa sukari inayokadiriwa kuwepo kwenye damu kama kijiko kimoja tu cha chai. Unywaji wa soda moja unaweza kuongeza Zaidi ya vijiko 10 hivyo basi mwili wako unakuwa unashindwa kuhimili sukari iliyozidi. Na ulaji wa Baga inakadiliwa kuwa baga moja ya kati inaweza kutoa sukari Zaidi ya vijiko 16 kwenye damu. Swali la kujiuliza mwili unapeleka wapi sukari iliyozidi wakati miili yetu inahitaji sukari kiwango kidogo sana kama kijiko kimoja tu kuishi?
Mwili hutengeneza maji kutoka kwenye seli za  kongosho ziitwazo beta seli,maji haya ni homon iitwayo INSULIN
Kama nilivoandika hapo juu kazi kubwa ya insulin ni kutunza glucose hii katika damu kwa matumizi ya baadae, na inatunza katika kiasi maalumu katika mfumo wa Glycogen na kiasi kikubwa katika mafuta. Na hivyo basi mafuta haya huhifadhiwa katika sehemu mbalimbali kama tumboni,shingoni,mikononi,kifuani,kiunoni nk. Na mafuta haya huhifadhiwa katika mfumo wa TRYGLYCERIDES ambayo haya ni miongoni vya mafuta mabaya mwilini mwako. Sasa mtu anayekwambia wanga nyingi katika chakula chako ni salama anakudanganya kwa kiasi kikubwa kwani tunaona jinsi gani ulaji wa kiwango kingi cha vyakula vya wanga na sukari vinavyo sababisha sukari kupanda kupita kiasi na insulinkuanza kuhifadhi katika mafuta.

HATUA ZINGINE MUHIMU ZA KUZINGATIA ILI KUREKEBISHA KIWANGO CHA SUKARI KWENYE DAMU, na kuepuka magonjwa kama kisukari, kitambi, presha kubwa ya damu, mvurugiko wa homoni, na upungufu wa nguvu za kiume.
1.      Ongeza kiwango cha vyakula vya nyuzinyuzi au kambakamba (fibers) kwenye mlo wako kila siku. Vyakula hivi husaidia kupunguza kasi ya usagaji wa chakula kwenye mwili kwa kunyonya maji kwenye utumbo na hivo kusaidia kupunguza umwagaji wa insulin kila mara kwenye damu, maana muda mwingi utajihisi umeshiba na hutahitaji kula kilamara, rejea maelezo ya juu kuhusu madhara ya umwagaji wa insulin nyingi kwenye damu, faida nyingine za vyakula vya kambakamba ni kupunguza hatari ya kupata kansa ya utumbo mpana na tumbo kujaa gesi. Chanzo kizuri cha vyakula hivi ni mboga za majani, na siyo ugali wa dona wala nafaka isiyokobolewa kama ulivoelekezwa.
2.      Punguza wanga na sukari maana ni vyakula vinavyopandisha, kiwango cha insulin kwa kiasi kikubwa kwenye damu, kumbuka wanga inapoingia kwenye mwili hubadilishwa kuwa sukari na kisha uchakataji wake kuendelea kama sukari.
3.      Kula kwa wingi  vyakula vya fats au mafuta, hivo mbadala wako wa wanga na sukari uwe vyakula vya mafuta kama na protini, kama parachichi, nazi, samaki, nyama na maziwa kutoka kwa Wanyama walifugwa kwa kula nyasi na siyo nafaka, mafuta ya mawese, mafuta ya mizeituni, mayai ya kienyeji, na karanga (jamii zote za karanga mbichi).
FAIDA YA MWILI KUTUMIA FATS (VYAKULA VYA MAFUTA) KUZALISHA NISHATI YA MWILI
1. Mwili unakuwa una nguvu za kutosha unapokuwa unatumia fats au ketone bodies kuzalisha nguvu
2. Mwili unapokuwa unatumia mafuta kuzalisha nishati hupunguza kiwango cha cha FREE RADICALS MWILINI
3. Vyakula vya Protini,mafuta vinaonesha kutopandisha kiwango cha insulin (Kihifadhi mafuta) kwa kiwango kikubwa kama ilivyo vyakula vya wanga
4. Utajitibu magonjwa mengi sana kwani utazuia utenegenzwaji wa FREE RADICALS na Advanced Glycated End Products ambavyo ni vyanzo vya magonjwa mengi ambapo chanzo chake ni ulaji wa vyakula vya wanga kwa wingi kupita kiasi.

4.      Mazoezi ya viungo, kama bado upo kwenye hatua ya kwanza ya kisukari, lakni kama umefikia hatua mbaya basi tunashauri mazoezi yaanze baada ya mwili kutengemaa
5.     Pata usingizi wa kutosha kuanzia masaa 8 mpaka 9 kila siku na Epuka msongo wa mawazo ambao hupelekea uchovyaji kwa wingi wa homoni za glucagon na cortisol mabazo zote huchangia katika kiwango cha sukari kwenye damu.
6.  Usitumie vyakula wala vinywaji vilivyokobolewa na kusindikwa badala yake kula vyakula asili ulichoandaa jikoni mwako.
7.      Tumia virutubisho vya omega 3 na vitamin kutoka kwenye vyanzo vilivyothibitika unaweza kupata virutubisho hivi ofsini kwetu pia.
8.      Mwisho kabisa hakikisha unafatilia matokeo yako kwa kufanya vipimo kila awamu, hii itakusaidia kfikia malengo yako ya kupunguza kiwango cha sukari haraka, hasa ukiwa kwenye program yetu ya diabetes reverse.


     HUDUMA YETU YA DIABETES REVERSE PROGRAMME

Huduma hii itawalega watu wote wenye ugonjwa wa kisukari, cha mwanzo ama cha kati,bila kujali maumivu na mateso unayopata sasa ya kisukari. huduma hii imegawanywa katika siku 60. Kila awamu itachukua siku 20. Baadhi ya huduma muhimu utakazofaidi kupitia programme hii,

1.      Utaongea moja kwa moja na muhudumu wetu na kupata maelekezo namna ya kuanza safari yako ya kurekebisha tatizo la kisukari
2.      Ushauri hatua kwa hatua jinsi ya kupangilia mlo wako na kuepuka magonjwa makubwa kama presha kisukari, upungufu wa nguvu za kiume, na mvurugiko wa homoni kwa wanawake
3.  Utapata Kirutubisho kimoja kilicho kwenye mfumo wa chai cha kukusaidia katika safari yako ya kurekebisha sukari kwa Sh 50,000/= pekee
4.      Utaweza kupata ushauri kila siku na majibu juu ya maswali yako ya kiafya.kumbuka hata kama upo mbali na ofisi yetu ya hapa Dar maeneo ya Mwembechai, kwa wale wa mikoani na nje ya nchi huduma itakufikia kwa njia ya mtandao.


Basalam pear tea


BASALM PEAR TEA ITAKUSAIDIA
  • Kukarabati Beta cells za kongosho linalohusika na utoaji wa insulin,
  • Kupunguza sukari na lipids kwenye damu,
  • Kuzuia ufyonzwaji wa sukari katika utumbo mdogo, na kupunguza sukari kwenye mzunguko wa damu na
  • Kuepusha madhara ya kisukari kama kiu na kukauka mate

Ebu fikiria kuepuka mateso ya ugonjwa wa kisukari kama upofu, kukatwa viungo, kushindwa kuhimili tendo la ndoa, kupungua uwezo wa kufikiri kwa kudhoofu mwili, kwa progam fupi ya siku 60 tu. Progamu hii ikiwa imefanyiwa  utafiti na kuleta matokeo makubwa kwa wagonjwa wetu.  Hakikisha unamshirikisha na mwingine habari hizi njema

Tiba yetu inagarimu Tsh 50,000/= tu 

Bofya hapa Kuchati na Daktari kwa whatsapp


Usiache Kusoma Makala Hii ya afya inayofuatia: Uzito mkubwa na kitambi ni chanzo cha kisukari




Comments

Popular posts from this blog

KUTOKWA NA UCHAFU UKENI, CHANZO NA TIBA YAKE

Uke wa mwanamke hufanya kazi ya kutoa njia kati ya sehemu ya nje ya mwili na viungo vya uzazi vya ndani vya mwanamke. Hali ya kawaida ya majimaji yaliyomo katika uke wa mwanamke huwa ni ya tindikali ili kuzuia maambukizi ya vijidudu wa kuleta maradhi. Hali hii ya utindikali huletwa na bacteria waishio katika uke wa mwanamke. Bacteria hawa ni wa kawaida na hawana madhara kwa mwili. Uke ulio katika hali nzuri hutoa majimaji haya ili kujisafisha. Majimaji haya yanayotengenezwa katika uke na kwenye eno la cervix hufanya kazi ya kuondoa seli zilizokufa na bacteria waharibifu nje ya mwili na huu ndio uchafu wa kawaida ambao mwanamke hutoa ukeni. Kutoa uchafu huu sehemu za siri ni njia ya kuusafisha uke na kuzuia maambukizi ya magonjwa. Kitu cho chote ambacho kitaharibu uwiano wa utengeneaji wa majimaji haya ndani ya uke kinaweza kujenga mazingira ya maambukizi katika uke. Uchafu Wa Sehemu Za Siri  Wa Kawaida Wanawake wote hutoa uchafu sehemu za siri. Kiwango cha uchafu unaotoka, ra

JINSI YA KUONGEZA UFANISI WA VICHOCHEO VYA KIUME (TESTOSTERONE) NA KUKINGA DHIDI YA MATATIZO YATOKANAYO NA KUKUA KWA TEZI DUME KWA KUTUMIA VYAKULA HIVI VI 5

Maelezo ya utangulizi. Kichocheo cha testosterone, japo huusishwa zaidi na upande wa mwananume ni muhimu kwa afya ya pande zote mbili yaani mwanamke na mwanamme pia.kadiri umri unavoenda mbele basi kiwango cha uzalishaji wa kichocheo cha testerone kupungua, kupungua kwa kichocheo hiki kunaambatana na ukuaji wa tezi dume (prostate gland),kupotea kwa nywele na pia saratani mfano saratani ya tezi dume. .KAZI KUBWA YA KICHOCHEO HIKI NI KUONGEZA MSUKUMO NA HAMU YA TENDO LA NDOA , KUIMARISHA MISULI NA MIFUPA MWILINI. NINI KINAHITAJIKA ILI KUZALISHA KICHOCHEO CHA TESTOSTERONE? Ili kuhakikisha uzalishaji wa kichocheo cha kiume unafanyika, mwili unahitaji virutubisho au viini lishe mbalimbali, baadhi ya viini lishe hivyo ni madini ya ZINC na vitamin D3,  vitamini D inaweza kuzalishwa na mwili pale ngozi yako inapokutana na mwanga wa jua, hapa nazungumzia mwanga wa asubuhi wakati jua ndo linachomoza na pia lile jua la jion karibia na kuzama, hivyo utakubaliana na mimi kuwa wengi wet

MADHARA YA PUNYETO NA TIBA YAKE

MAELEZO  YA AWALI KUHUSU TATIZO LA UPIGAJI PUNYETO Watu wengi sana wanataka kufahamu jinsi gani wafanye ili kuachana na kitendo cha upigaji punyeto. Punyeto ni tendo la mtu la kuamsha hisia za mapenzi au msisimko ambao unampelekea mtu huyu kufikia kilele cha kujimalizia tamaa zake! Bila kufanya tendo halisi, hutumia fikra zake katika picha za zinazoitwa za ngono au picha zozote zinazoweza kulifanikisha tendo hilo, movie n.k. Kilele cha yote anafikia mahali anajimalzia tamaa zake mwenyewe!. Nimekuwa nikiona baadhi ya watu wanaosema wameelimika wakipingana wao kwa wao katika suala zima la kupiga punyeto! Wako wanaotetea kutokana na elimu yao na wanasema kwa ujasiri mkubwa kwamba "kupiga punyeto ni sehemu ya maisha ya mwanadamu" Ina maana katika maisha ya mwanadamu upigaji punyeto inaelezwa ni kama tendo la lazima mpaka inafikia mahali wanasema ni sehemu ya maisha (Maisha) ya mwanadamu. Nimekuwa nikipata kesi nyingi sana juu ya madhara yatokanayo na punyeto. Aslimia 60